TAARIFA YA HALI YA USAFI NA HIFADHI YA MAZINGIRA WILAYANI KAKONKO KATIKA ROBO YA PILI 2016/2017
USAFI WA MAZINGIRA NA MAENEO YA BIASHARA
Ukaguzi wa nyumba za biashara
Ukaguzi wa nyumba za bishara umefanyika katika kata ya Kasanda, Kakonko Katanga na nyabibuye na
Biashara zilizokaguliwa ni kama ifuatavyo:
USAFI WA MAZINGIRA
Ufuatiliaji na ukaguzi wa mazingira umefanyika katika kata ya Kasanda, Katanga Kakonko mjini Gwanumpu na Rugenge. Kazi hizi zimefanywa na kamati za mazingira za vijiji. Katika mji wa Kakonko ukaguzi unafanyika kila siku ya Alhamisi ambapo kila mtaalam wa afya huenda kwenye kitongoji anachokilea kuhamasisha usafi na kufanya ukaguzi.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Baada ya ukaguzi hatua zilizochukuliwa katika ngazi za vijiji zilikuwa ni kuwaita wale ambao hawana vyoo na wenye vyoo vibovu na wlitozwa faini kama ifuatavyo;
Kata ya Rugenge
Kata ya Kasanda
Mji wa Kakonko
Katika mji wa kakonko kazi ilifanyika katika vitongoji kama ifuatavyo
Katika mji wa Kakonko majina 147 ya wale wote waliokutwa ni wachafu yako ofisi ya mwanasheria yanafanyiwa upembuzi wa kisheria ili hatua muafaka zichukuliwe hasa ukizingatia kwamba sheria ndogo za halmashauri bado hazijaruhusiwa kutumika.
Aidha maafisa wa afya ambao walikabidhiwa kufanya ukaguzi wa afya katika vitongoji na hawajakamilisha kazi yao wameandikiwa barua ya kujieleza ni kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya msingi.
HALI HALISI KATIKA MAENEO YALIYOKAGULIWA ni kama inavyoonekena katika jedwali hapa linalofuata
Na
|
Jina la kata
|
Kaya zilizokaguliwa
|
Kaya zenye vyoo bora
|
Kaya zenye vyoo vya asili
|
Kaya zisizo na vyoo
|
Kaya zenye vifaa vya taka/mashimo ya taka
|
Kaya zenye vichanja
|
|
Kakonko mjini
|
451
|
269
|
161
|
21
|
327
|
131
|
|
kasanda
|
3,033
|
311
|
2363
|
359
|
2,087
|
2,417
|
|
Rugenge
|
1,677
|
24
|
1,388
|
75
|
1,180
|
1,411
|
|
jumla
|
5,161
|
604
|
3,912
|
455
|
3,594
|
3,959
|
UTEKELEZAJI WA KUFANYA USAFI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI.
Usafi umekuwa ukifanywa na wananchi katika maeneo yao. aidha viongozi na watumishi wa serikali katika jumamosi ya mwisho wa mwezi wa 10 wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko walifanya usafi katika viwanja vya Parokia ya kanisa Katoliki kakonko mjini na kuzibua mifereji ya maji ya mvua katika barabara zenye urefu wa mita 500. Jumamosi ya mwisho wa mwezi Novemba walifanya usafi katika eneo la wazi la Kakonko mjini ambako kuna kizimba cha kuhifadhia taka karibu na kanisa la Anglikana.
Jumamosi ya mwisho wa mwezi Dec walifanya usafi katika maeneo ya Ofisi za Halmashauri hasa kazi kubwa ilikuwa kufyeka nyasi na kufagia maeneo yote ya ofisai za Halmashauri. Mahudhurio katika utekelezaji yamekuwa ya kutosha wanhudhuria watumishi 45 hadi 50 kati ya 60 ambao wako makao akuu ya Halmashauri.
Kwa wananchi wa kawaida siku hiyo ni siku ya soko kuu ushiriki wao ni mdogo sana.
Uzoaji wa takataka
Idara ya usafi na mazingira imeanisha eneo muafaka ambalo litakuwa dampo kuu la mji wa kakonko .eneo hilo liko kilomita 8.5 kutoka kakonko mjini kulekea mashariki na liko kilomita 6 toka katika mto wa muhwazi katika kijiji cha itumbiko.
Taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja upimaji na upembuzi wa kimazingira zinaendelea tuna tegemea dampo hilo litaanza kufanya kazi mwezi January.
Mahali ambapo takataka zinamwagwa kwa sasa pamepigwa marufuku kwa sababu hapakidhi vigezo vya kisheria na mazingira.
Katika kutekeleza mkakati wa kufanya mji wa kakonko unakuwa msafi wakati wote ambao uliidhinishwa na baraza la madiwani lilopita idara imepanga ratiba ya kufanya mikutano ya hadhara katika ngazi za vitongoji baada ya kukutana na kamati ya maendeleo ya kata mwishoni mwa mwezi January.
Hata hivyo katika maeneo ya nje ya mji wa kakonko yaani katika kata na vjiji uzoaji wa taka na usafi hufanywa na mpango kata hasa katika masoko na centers hali ya usafi katika masoko yote upo kwa kiwango cha 50%
Katika ngazi ya kaya vijijini wananchi wanadhibiti taka kwa kuchimba mashimo ya taka na wengine kuziweka mashambani kama mbolea.
HIFADHI YA MAZINGIRA
ufuatiliaji wa hifadhi ya mazingira katika kipindi hiki umefanyika katika kufanya ukaguzi wa vyanzo vya maji na maeneo oevu katka kata ya Katanga kasanda Rugenge na Kakonko mjini imeonekana wazi kwamba katika maeneo mengi ardhi oevu na vyanzo vya maji ambavyo kisheria hairuhusiwi kutumika kwa shughuli za kibinadamu wananchi wamelima masebula ndani ya meta 60.hata hivyo kijiji cha Katanga na ilabiro vyanzo vyao vya maji vilivyo vingi wamevihifadhi vizuri.
Miti rafiki wa maji imepandwa katika vyanzo vya maji vya kata ya Kakonko, Muhange, Kasanda Katanga na maeneo yote kufuatia agizo na uzinduzi wa kuhifadhi mazingira katika vyanzo vya maji uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko tarehe 16 Desemba 2016 ufuatiliaji unaendelea.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa