Daraja la Ikambi linaoelekea shule ya Sekondari Ikambi Wilayani Kakonko linatarajiwa kujengwa kwa gharama ya milioni 246 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan hivyo kuwafungulia Wananchi wa Kakonko fursa za kiuchumi, kielimu na kiafya.
Kaya 263 zinazonufaika na Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF katika kata ya Kasanda Wilayani Kakonko zimechonga barabara mpya ya kilomita 3 kuelekea mashambani na kumpongeza Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha maisha yao.
Wana michezo wa UMITASHUMTA waliochaguliwa kutoka kanda ya Kasanda na Kakonko wakiwa wanasubiri kuungana na wana michezo kutoka kanda ya Nyaronga ili kuunda timu ya Wilaya wahehimziwa kuendelea kufanya mazoezi ziaidi ili kuiwakilisha Wilaya ya Kakonko katika mashindano ambayo yatafanyika ngazi ya mkoa hivi karibuni.
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa