Timu ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Halmashauri, ikiongozwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Festo Basugoya, imetembelea miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu na Afya kwa lengo la kupima utekelezaji wa viashiria vya miradi hiyo kulingana na mikataba na muda uliopangwa.
Akizungumza majukumu ya kitengo hicho, Basugoya alisema ufuatiliaji huo unalenga si tu kupima hatua za utekelezaji wa miradi, bali pia kufanya tathmini ya matumizi ya rasilimali zilizotengwa ili kubaini kama zinatumika kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba.
Miradi iliyotembelewa ni ujenzi na ukarabati wa Zahanati ya Kasanda pamoja na ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi katika Kijiji cha Nkuba, Kata ya Kasanda.
Katika mradi wa Zahanati ya Kasanda, jengo jipya la kujifungulia (maternity) limefikia asilimia 72 ambapo tayari limeezekwa na kupigwa lipu. Jengo la OPD limefikia asilimia 51 na ukarabati unaendelea. Mradi huo unagharimu shilingi milioni 195.
Kwa upande wa ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi Nkuba, jengo la shule ya awali limeezekwa na kupigwa lipu, huku jengo la shule ya msingi likiwa tayari limeezekwa. Mradi huu una gharama ya shilingi milioni 341.
Timu hiyo inayojumuisha maafisa viungo (focal persons) kutoka idara na vitengo mbalimbali vya halmashauri ilitoa ushauri kwa wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi ikamilike kwa wakati kama ilivyopangwa.
Kwa mujibu wa timu hiyo, matarajio ni kuona changamoto zote zinazojitokeza zinatatuliwa haraka na ushauri wao kwa Menejimenti unafanyiwa kazi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa