Shirika la REDESO kwa kushirikiana na Wataalam wa kamati ya Usimamizi wa maafa wa Halmashauri wamefanya kikao wakilenga kuimarisha utayari wa Wilaya kukabiliana na maafa ili kuhakikisha jamii inakuwa salama na yenye uelewa kuhusiana na maafa yanayojitokeza.
Akieleza umuhimu wa kuimarisha utayari wa Wilaya katika kukabiliana na maafa, katika kikao kilichofanyika leo Alhamisi Novemba 20, 2025 katika Ukumbi wa Buyungu uliopo Makao makuu ya Halmashauri, Mwakilishi wa Shirika la REDESO, Ibrahim Twaib, ameeleza kuwa kikao hicho kimejikita katika kuboresha mikakati ya kuimarisha utayari wa kukabiliana na maafa.
Bwana Twaib, ameongeza kuwa moja ya mikakati ya kuimarisha utayari wa kukabiliana na maafa ni kushirikisha jamii katika kuzuia athari za maafa yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wa Mratibu wa maafa Wilaya, Festo Basugoya, amefafanua kuwa jamii imejengewa uelewa kwa kupewa elimu kuhusu namna ya kukabiliana na maafa hali iliyopelekea jamii kuweza kushiriki kikamilifu kwa kutoa taarifa kupitia kamati za maafa pindi hali hiyo inapojitokeza.
Aidha mratibu ameshukuru shirika la REDESO kwa kuwezesha kuandaa kikao cha pamoja kwani kimekuwa na mchango mkubwa na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliyojadiliwa kwa lengo la kuendelea kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza katika maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa