Utangulizi
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika robo ya pili imetekeleza shughuli zifuatazo; Usambazaji wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali, Kutoa ushauri wa kitalaamu juu ya kanuni bora za kilimo, kuratibu na kusimamia miradi inayo husiana na kilimo, kuandaa taarifa mbalimbali za kilimo na kuziwasilisha katika ngazi zinazohusika na kushirikiana na idara nyingine (maendeleo ya jamii, maliasili ardhi na misitu) Pamoja taasisi/mashirika ya RERAI na BTC katika kutekeleza masuala mtambuka.
USAMBAZAJI WA PEMBEJEO
Usambazaji wa pembejeo zenye ruzuku ya Serikali zilifika tarehe 3/12/2016 na kuanza kusambazwa vijijini tarehe 12/12/2016 baada ya mgao kwa vijiji 44 ndani ya Wilaya ya Kakonko uliofanywa na Kamati ya Pembejeo ya Wilaya. Katika mgao huo kila kijiji kilipata mgao wa mifuko arobaini (40) isipokuwa kijiji cha Nyakayenzi na Kinonko ambavyo vilipata mifuko sitini (60) kila kimoja. Gharama ya kuchangia toka kwa mkulima ni Shs.29,500/= kwa mfuko wa kilogram 50.
Hadi Kufikia tarehe 04/01/2017 jumla ya tani 77.45 (mifuko 1549), kati ya tani 90 (mifuko 1,800) za mbolea ya kukuzia (UREA) imefikishwa katika vijiji 42 kati ya vijiji 44. Vijiji vya Njomulole na Kihomoka bado.
Kihomoka; Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo Wilaya ya Kakonko alikiondoa kijiji hiki katika kupata pembejeo kutokana na walengwa kukosa fedha za kuchangia (Shs.29,500/=) na kuamuru pembejeo hizo kupelekwa vijiji vya Kanyonza na Muganza vilivyopo ndani ya kata ya Kanyonza. Zoezi la Usambazaji bado linaendelea.
MAZAO;
Shughuli kubwa inayoendelea vijijini kwa mazao ya chakula (Mahindi, Maharage, Muhogo, Mpunga, Mtama, Karanga, Viazi vitamu, mboga na matunda) ni upandaji, palizi na kuweka mbolea ya kukuzia.
Hali ya mzao kwa kipindi hiki inatofautiana katika vijiji, kutokana na maeneo mengi kuwa na uhaba wa mvua, hivyo mazao mengi kuanza kunyauka ingawa katikati mwa mwezi Desemba mvua ilinyesha na kuleta matumaini kwa baadhi ya mazao.
Kutokana na hali hiyo, Halmashauri ilitoa tahadhari kwa wananchi juu ya uwezekano wa kuwepo kwa upungufu wa Chakula msimu huu na kuwashauri kutumia chakula kilichopo kwa uangalifu mkubwa na pia kupanda mazao yanayokomaa mapema na kuvumilia ukame kama vile Viazi vitamu, Mtama na Mihogo ili kukabiliana na upungufu huo wa chakula unaoweza kujitokeza.
S/N
|
MKULIMA MMOJA MMOJA/VIKUNDI
|
IDADI YA WAKULIMA
|
ME
|
KE
|
IDADI YA MIFUKO YENYE UJAZO WA PINGILI 1000
|
KIJIJI
|
ENEO/EKARI |
NAMBA YA SIMU
|
1 |
JUMA MAGANGA
|
1 |
1 |
|
4 |
ITUMBIKO
|
1 |
0755-906050
|
2 |
SIMON KIPARA
|
1 |
1 |
|
4 |
ITUMBIKO
|
1 |
0764-217756
|
3 |
BENARD MICHAEL
|
1 |
1 |
|
4 |
ITUMBIKO
|
1 |
0765-820592
|
4 |
DEBORA TITUS
|
1 |
0 |
1 |
4 |
ITUMBIKO
|
1 |
0753-836162
|
5 |
JAPHET.BASEKILOLA
|
1 |
1 |
|
4 |
RUYENZI
|
1 |
|
6 |
SAMWELI NTAMBALA
|
1 |
1 |
|
4 |
RUYENZI
|
1 |
|
|
JUMLA
|
6 |
5 |
1 |
24 |
|
6 |
|
|
INA LA KIKUNDI |
IDADI YA WAKULMA |
ME |
KE |
IDADI YA MIFUKO UJAZO PINGILI 1000
|
KIJIJI |
ENEO/EKARI |
NAMBA YA SIMU |
1 |
TUMAINI
|
22 |
13 |
9 |
32 |
KIYOBERA
|
4 |
0765-836998
|
2
|
KINAMAMA TUSHIKAMANE
|
12 |
0 |
12 |
32 |
KIYOBERA
|
4 |
0755-090268
|
3
|
TUJITEGEMEE
|
14 |
0 |
14 |
32 |
MUGANZA
|
4 |
0769-646459
|
4 |
MWENDO WA SAA
|
25 |
12 |
13 |
23 |
KIGA
|
3 |
0624-389646
|
5 |
TUJIKWAMUE
|
25 |
0 |
25 |
24 |
KASONGATI
|
4 |
0621-383164
|
|
Jumla
|
98 |
25 |
73 |
143 |
|
19 |
|
USAMBAZAJI WA MBEGU ZA MAHARAGE
Halmashauri kupitia idara ya Kilimo, robo hii imesambaza mbegu za Maharage kwa kushirikiana na Kampuni ya QFP (Quality Food Product) ya Arusha. Mbegu hizo ziliuzwa kwa utaratibu wa mkopo kwa kutanguliza nusu ya malipo ya fedha TSh.1000/=, ambapo bei halisi ya kilo moja ilikuwa TSh. 2000/= kwa kilo moja. Jumla ya kilo 21,200 sawa na tani 21.2 za mbegu ya maharage yaliyouzwa kwa wakulima 600 na kupandwa katika Ekari 848.
USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA MRADI WA MIVARF.
MIVARF (Markenting Infrastructure,Value addition and Rural Fainance Supporting Programme) ni Mradi unao shughulika na Mnyororo wa thamani wa zao la Mpunga katika Wilaya ya Kakonko. Mradi huu unasaidia kutoa mafunzo kwa wakulima juu ya Kuongeza thamani ya mazao (Value addition), Kuwaunganisha wakulima na Masoko (Market Linkage) na Huduma za Kifedha vijijini (Rural Finance). Utekelezaji wa mafunzo hayo hufanyika lengu kuu la Kuwajengea uwezo wakulima katika uzalishaji na kuwaunganisha na masoko. (Producer Empowerment and Market Linkage- PEML)
Kazi zilizotekelezwa katika idara ya Kilimo ni Usimamizi wa kazi zinazotekelezwa na mtoa huduma (SP) wa MIVARF ambaye ni Shirika la RERAI. Kazi hii ilifanyika kwa kushirikiana na Kamati ya Usimamizi wa Mradi ya Wilaya;- Shughuli zilizofanyika ni pamoja:-
Taarifa ilijadiliwa na kupokelewa.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa