WASIFU WA HALMASHAURI
1.0 Utangulizi
Wilaya ya Kakonko ilianzishwa kwa tangazo la Serikali GN. 287 ya mwaka 2011 baada ya kugawa Wilaya ya Kibondo na kuunda Wilaya ya Kibondo na Kakonko. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ilianzishwa tarehe 08/3/2013 na kutangazwa katika gazeti la Serikali kwa GN.42.
Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya yapo katika mji wa Kakonko uliopo umbali wa Km 48 Kaskazini mwa mji wa Kibondo katika barabara kuu ya Kigoma – Mwanza.
1.1 Jiografia ya Mahali ilipo Wilaya
Kakonko ni Halmashauri moja wapo kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Kigoma. Wilaya ipo upande wa kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na inapakana na Wilaya ya Ngara na Biharamulo (Mkoa wa Kagera) kwa upande wa Kaskazini na Magharibi inapakana na Jamhuri ya Burundi, Kusini inapakana na Wilaya ya Kibondo, Mashariki hadi Kaskazini Mashariki inapakana na Wilaya ya Bukombe (Mkoa wa Geita).
1.2 Ukubwa wa Wilaya
Wilaya ya Kakonko ina ukubwa wa kilometa za mraba 7,715.05 ambazo zimegawanyika katika makundi sita ya matumizi kama inavyo onesha kwenye jedwali 1.1 hapa chini.
JEDWALI 1.1 UKUBWA WA ENEO LA WILAYA
FUNGU
|
MATUMIZI
|
KM2 |
ASILIMIA (%)
|
1
|
Mamlaka ya vijiji
|
2,041.03 |
26.5 |
2
|
Msitu wa hifadhi
|
178.65 |
2.3 |
3
|
Ardhi inayofaa kwa kilimo (ardhi inayolimwa ni KM2 671.8 sawa na 62%)
|
1,084.2 |
14.1 |
4
|
Malisho ya mifugo
|
806.4 |
10.5 |
5
|
Hifadhi ya akiba ya wanyamapori na misitu (Moyowosi Game Reserve and Buyungu Local Authority Forest Reserve)
|
624.9 |
8.1 |
6
|
Makazi, Huduma za Jamii, Milima na Maji
|
2,979.87 |
38.5 |
JUMLA
|
7,715.05 |
100 |
Chanzo: Idara ya Ardhi
1.3 Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Wilaya ya Kakonko ilikuwa na Jumla ya Watu 178,419 ambapo idadi ya wanaume ilikuwa 86,688 sawa na asilimia 49 na idadi ya wanawake ilikuwa 91,731 sawa na asilimia 51. Kasi ya ongezeko la watu katika Wilaya ya Kakonko (Inter-censal Population Growth Rate) ni 0.6 kati ya Sensa ya watu mwaka 2012 ambapo idadi ya watu ilikuwa 167,555 na Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 ambapo idadi ya watu ni 178,419. Aidha Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ilikuwa na idadi ya Kaya 37,361 ambapo kulikuwa na wastani wa watu 4 kwa kaya. Mchanganuo wa Idadi ya watu, Kaya, Wastani wa watu kwa Kaya na wastani wa kijinsi ni kama ilivyo kwenye Jedwali 1.2 hapa chini
JEDWALI 1.2 IDADI YA WATU, KAYA, WASTANI WA IDADI YA WATU KWA KAYA NA WASTANI WA JINSI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO |
|||||||||
Na
|
KATA
|
IDADI YA WATU |
IDADI YA KAYA
|
WASTANI WA IDADI YA WATU KWA KAYA
|
WASTANI WA KIJINSI
|
||||
JUMLA
|
ME
|
%ME
|
KE
|
%KE
|
|||||
|
|
178,419 |
86,688 |
49% |
91,731 |
51% |
37,361 |
4.8 |
95 |
1.
|
Nyabibuye
|
10,162 |
4,950 |
3% |
5,212 |
3% |
2,090 |
4.9 |
95 |
2.
|
Nyamtukuza
|
20,612 |
10,362 |
6% |
10,250 |
6% |
4,030 |
5.1 |
101 |
3.
|
Muhange
|
10,246 |
5,087 |
3% |
5,159 |
3% |
2,048 |
5.0 |
99 |
4.
|
Gwarama
|
17,668 |
8,645 |
5% |
9,023 |
5% |
3,775 |
4.7 |
96 |
5.
|
Kakonko
|
14,629 |
7,080 |
4% |
7,549 |
4% |
3,245 |
4.5 |
94 |
6.
|
Kiziguzigu
|
13,025 |
6,312 |
4% |
6,713 |
4% |
2,695 |
4.8 |
94 |
7.
|
Kanyonza
|
10,608 |
5,378 |
3% |
5,230 |
3% |
2,143 |
5.0 |
103 |
8.
|
Kasuga
|
16,769 |
8,198 |
5% |
8,571 |
5% |
3,401 |
4.9 |
96 |
9.
|
Rugenge
|
11,257 |
5,330 |
3% |
5,927 |
3% |
2,297 |
4.9 |
90 |
10.
|
Kasanda
|
17,927 |
8,611 |
5% |
9,316 |
5% |
3,691 |
4.9 |
92 |
11.
|
Gwanumpu
|
14,956 |
7,043 |
4% |
7,913 |
4% |
3,214 |
4.7 |
89 |
12.
|
Katanga
|
9,701 |
4,620 |
3% |
5,081 |
3% |
2,203 |
4.4 |
91 |
13.
|
Mugunzu
|
10,859 |
5,072 |
3% |
5,787 |
3% |
2,529 |
4.3 |
88 |
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
1.4 Mgawanyo wa idadi ya watu kwa Umri, Jinsi na maeneo wanayoishi
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Mkazi ya mwaka 2022, takwimu zinaonyesha idadi kubwa ya watu ilikuwa wa umri kati ya miaka 0-4 ambapo idadi yao ilikuwa 31,121 sawa na asilimia 17% ya idadi ya watu wote. Vile vile idadi kubwa ya watu 173,113 sawa na asilimia 97 ni ambao wanaishi vijijini na watu 5,306 sawa na asilimia 3 wanaishi Mjini. Mchanganuo wa takwimu hizi upo katika jedwali 1.3 hapa chini
JEDWALI 1.3: MGAWANYO WA IDADI YA WATU KWA UMRI, JINSI NA MAENEO WANAYOISHI
Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa Umri, Jinsi na Maeneo wanapoishi |
||||||||||||
UMRI |
JUMLA |
WANAOISHI VIJIJINI |
WANAOISHI MJINI |
|||||||||
JUMLA |
% mgawanyo wa idadi nya watu kwa umri |
Me |
Ke |
Me |
Ke |
Jumla |
% ya wanaoishi vijijini |
Me |
Ke |
Jumla |
% ya wanaoishi Mjini |
|
JUMLA |
178,419 |
|
86,688 |
91,731 |
84,135 |
88,978 |
173,113 |
97 |
2,553 |
2,753 |
5,306 |
3 |
0 - 4 |
31,121 |
17 |
15,671 |
15,450 |
15,325 |
15,087 |
30,412 |
|
346 |
363 |
709 |
|
05.-09 |
28,697 |
16 |
14,171 |
14,526 |
13,863 |
14,202 |
28,065 |
308 |
324 |
632 |
||
10.-14 |
27,207 |
15 |
13,760 |
13,447 |
13,420 |
13,084 |
26,504 |
340 |
363 |
703 |
||
15 - 19 |
18,262 |
10 |
9,283 |
8,979 |
8,986 |
8,627 |
17,613 |
297 |
352 |
649 |
||
20 - 24 |
13,612 |
8 |
6,186 |
7,426 |
5,927 |
7,160 |
13,087 |
259 |
266 |
525 |
||
25 - 29 |
11,063 |
6 |
5,175 |
5,888 |
4,972 |
5,610 |
10,582 |
203 |
278 |
481 |
||
30 - 34 |
8,875 |
5 |
4,289 |
4,586 |
4,070 |
4,383 |
8,453 |
219 |
203 |
422 |
||
35 - 39 |
7,696 |
4 |
3,598 |
4,098 |
3,443 |
3,967 |
7,410 |
155 |
131 |
286 |
||
40 - 44 |
6,459 |
4 |
3,000 |
3,459 |
2,898 |
3,361 |
6,259 |
102 |
98 |
200 |
||
45 - 49 |
5,877 |
3 |
2,723 |
3,154 |
2,629 |
3,052 |
5,681 |
94 |
102 |
196 |
||
50 - 54 |
5,014 |
3 |
2,327 |
2,687 |
2,253 |
2,619 |
4,872 |
74 |
68 |
142 |
||
55 - 59 |
3,673 |
2 |
1,750 |
1,923 |
1,696 |
1,860 |
3,556 |
54 |
63 |
117 |
||
60 - 64 |
3,567 |
2 |
1,702 |
1,865 |
1,658 |
1,817 |
3,475 |
44 |
48 |
92 |
||
65 - 69 |
2,175 |
1 |
993 |
1,182 |
966 |
1,152 |
2,118 |
27 |
30 |
57 |
||
70 - 74 |
1,928 |
1 |
831 |
1,097 |
815 |
1,069 |
1,884 |
16 |
28 |
44 |
||
75 - 79 |
1,148 |
1 |
485 |
663 |
475 |
650 |
1,125 |
10 |
13 |
23 |
||
80+ |
2,045 |
1 |
744 |
1,301 |
739 |
1,278 |
2,017 |
5 |
23 |
28 |
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
1.5: Hali ya Hewa
Hali ya hewa ni nyuzi joto kati ya 150C hadi 220C na hupata mvua kati ya 800mm hadi
1,900mm kwa mwaka kuanzia mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi mwisho wa Mei.
2.0 Sekta ya Utawala
Wilaya ya Kakonko ina jumla ya Tarafa tatu (3) ambazo ni Nyaronga, Kasanda na
Kakonko ambazo zina jumla ya Kata kumi na tatu (13), vijiji 44 na Vitongoji 355.
Utawala bora na uwajibikaji ni mojawapo ya maeneo muhimu yanayopewa kipaumbele na Serikali kupitia Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, Dira ya maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Maendeleo Endelevu (SDG) na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/2022 – 2025/2026).
Kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi hutatuliwa kupitia Ofisi za Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji, Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Kata, Mkurugenzi Mtendaji, Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Aidha Halmashauri ina dawati maalumu linaloshughulikia malalamiko mbalimbali yanayoletwa dhidi ya Halmashauri au Watendaji wake na kufanya ufuatiliaji kuhakikisha kila lalamiko la mwananchi linatatuliwa au kuelekezwa kwenye mamlaka inayohusika. Baadhi ya malalamiko ama kero ni kama Migogoro ya Ardhi, Migogoro ya unyanyasaji wa Kijinsia na mingine. Kero nyingi hutatuliwa kupitia dawati la malalamiko kwa kuwasiliana ama kushirikiana na wahusika wa maeneo au idara husika. Pia masanduku ya maoni yamewekwa katika ofisi ili kubaini kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi mapema.
2.1 Hali ya Watumishi katika Halmashauri
Kwa mwaka 2022/2023, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina jumla ya Watumishi 1199 kati ya mahitaji ya watumishi 1958 ambapo upungufu wa watumishi ni 759 sawa na asilimia 39. Aidha katika watumishi waliopo idadi ya watumishi wa jinsia ya kiume ni 834 sawa na asilimia 70 na watumishi 365 ni wa jinsia ya Kike sawa na asilimia 30. Hali ya watumishi kwa miaka mitatu ni kama inavyoonekana kwenye jedwali 1.4 hapa chini.
JEDWALI 1.4: HALI YA WATUMISHI
HALI YA WATUMISHI
|
MGAWANYO WA WATUMISHI WALIOPO KIJINSI (2022/2023)
|
|||||||
MWAKA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
% UPUNGUFU
|
ME
|
%ME
|
KE
|
%KE
|
2020/2021
|
1958 |
951 |
1007 |
51 |
|
|
|
|
2021/2022
|
1958 |
988 |
970 |
50 |
|
|
|
|
2022/2023
|
1958 |
1199 |
759 |
39 |
834 |
70 |
365 |
30 |
Chanzo: Idara ya Utawala na Utumishi
2.2 Watumishi wapya walioajiriwa katika kipindi cha miaka mitatu.
Katika Kipindi cha miaka mitatu 2020/2021, 2021/2022 na 2022/2023 Halmashauri imefanikiwa kupata ajira mpya 303 kwa Kada tofauti tofauti ambapo watumishi wengi walioajiriwa ni wa Idara ya elimu msingi ambao walikuwa 122 sawa na asilimia 40.26, idara ya afya watumishi 80 sawa na asilimia 26.40, Idara ya Elimu Sekondari watumishi 60 sawa na asilimia 19.80, idara ya Utawala watumishi 40 sawa na asilimia 13.20 na idara ya Ujenzi Mtumishi 1 sawa na asilimia 0.33. Mchanganuo wa watumishi walioajiriwa ni kama ilivyo kwenye jedwali 1.5 hapa chini
JEDWALI 1.5: WATUMISHI WAPYA WALIOAJIRIWA 2020/2021-2022/2023
WATUMISHI WAPYA WALIOAJIRIWA
|
||||||
MWAKA
|
IDADI YA WATUMISHI WALIOAJIRIWA
|
IDARA YA UTAWALA
|
IDARA YA AFYA
|
IDARA YA ELIMU MSINGI
|
IDARA YA ELIMU SEKONDARI
|
IDARA YA UJENZI
|
2020/2021
|
34 |
1 |
0 |
17 |
16 |
0 |
2021/2022
|
107 |
0 |
44 |
36 |
26 |
1 |
2022/2023
|
162 |
39 |
36 |
69 |
18 |
0 |
JUMLA
|
303 |
40 |
80 |
122 |
60 |
1 |
%WATUMISHI KWA IDARA
|
|
13.20 |
26.40 |
40.26 |
19.80 |
0.33 |
Chanzo: Idara ya Utawala na Utumishi
Halmashauri imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya ajira mpya kwa kila mwaka wa fedha ili kuhakikisha Halmashauri inaweza kupata watumishi wa kutosha ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
2.3 Ujenzi wa nyumba za Watumishi
Katika kipindi cha miaka mitatu Halmashauri imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa idara 1 na inaendelea na ujenzi wa nyumba 1 ya Wakuu wa Idara ambapo mpaka kufikia mwezi Juni 2023 ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa idara umefikia hatua ya umaliziaji kwa nyumba moja na hatua ya msingi kwa nyumba ya pili.
2.4 Ujenzi wa Majengo ya Utawala
Katika kipindi cha 2019/2020 hadi 2022/2023 Halmashauri imendelea na ujenzi wa jengo la utawala ambapo mpaka kufikia Juni 2023 ujenzi wa ukumbi upo katika hatua ya kunyanyua boma. Kukamilika kwa mradi huu kutaongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi.
2.5 Mkakati wa kuwabakiza watumishi
Halmashauri ameandaa mkakati wa kuwabakiza watumishi ili kupunguza idadi ya watumishi wanaohama kwa kufanya yafuatayo:
2.5.1 Kutoa motisha kwa watumishi wapya.
2.5.2 Watumishi waliopo.
3.0 Uandikishaji wa Anwani za Makazi.
Wilaya ya Kakonko imetekeleza kikamilifu zoezi la uandikishaji wa Anwani za Makazi ambapo jumla ya nyumba 43,386 sawa na 100% ya malengo ya uandikishaji zimefikiwa na zoezi la uhakiki wa taarifa limekamilika. Zoezi la uwekaji wa namba za nyumba zilizotambuliwa limekamilika kwa asilimia 100 na zoezi la uwekaji wa majina ya Mitaa umekamilika. Zoezi hili limesaidia sana na kurahisisha utambuzi wa makazi na kufikiwa kwa urahisi tofauti na hapo awali. Jumla ya Sh.100,895,505.99 zilipokelewa kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuendesha zoezi na zimetumika.
4.0 Mapato
4.1 Mapato ya Halmashauri
Vyanzo vikuu vya mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni kutoka Serikali kuu, Fedha za wadau wa maendeleo, mapato ya ndani na wahisani mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa makusanyo ya ushuru wa soko pamoja na makusanyo kutoka mradi wa Matofali
Mwenendo wa makusanyo ya mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali pamoja na mapokezi ya fedha za ruzuku toka Serikali Kuu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023 kwa wastani ni ya kuridhisha kama inavyoonesha kwenye Jedwali 1.6 hapa chini.
JEDWALI 1.6: MUHTASARI WA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021-2022/2023
Mwaka
|
Bajeti Kiasi TZS
|
Makusanyo
|
Asilimia
|
2020/2021
|
1,031,933,256.00 |
842,746,697.00 |
82 |
2021/2022
|
1,038,636,000.00 |
1,069,058,023.00 |
103 |
2022/2023
|
1,142,499,600.00 |
1,192,450,028.45 |
104 |
Chanzo: Taarifa ya fedha
4.2 Udhibiti wa matumizi ya Fedha za Serikali
Halmashauri imeendelea kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni katika matumizi ya fedha za Serikali. Kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kipindi cha miaka mitatu (3) iliyopita Halmashauri imeweza kupata hati tofauti kama ilivyo kwenye jedwali 1.7 hapa chini:
JEDWALI 1.7: HALI YA HATI ZA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI
Mwaka
|
Aina ya Hati
|
2020/2021
|
Hati yenye mashaka
|
2021/2022
|
Hati safi
|
2022/2023
|
Ukaguzi unaendelea
|
Chanzo: Ripoti ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko inayo mikakati mbalimbali ya kuendelea kupata hati safi, ikiwa ni pamoja na:
5.0 Utekelezaji Sekta za Uzalishaji na Huduma za Kijamii
5.1.0 Sekta ya Kilimo
Wilaya ya Kakonko ina eneo linalofaa kwa kilimo jumla ya Hekta 108,420.14 sawa na 14.1% ya eneo la Wilaya, kwa msimu wa 2019/2020 eneo limwa lilikuwa hekta 67,220.49 sawa na 61.9% ya ardhi inayofaa kwa kilimo, ambapo kwa msimu wa kilimo 2021/2022 eneo limwa limeongezeka na kufikia jumla ya Hekta 98,459.5 za mazao ya chakula na biashara sawa na ongezeko la 46.47%. Mazao yanayostawi na kulimwa ni pamoja na Mahindi, Maharage, Karanga, Migomba, Mpunga, Tumbaku, Pamba, Mtama, Kahawa, Alizeti, Mhogo, Viazi vitamu na Mazao ya bustani. Aidha Wilaya ina jumla ya wastani wa kaya 31,010 za kilimo sawa na 83% ya kaya 37,361 zilizopo Wilayani. Kilimo ni shughuli kuu ya uchumi na kwa kiasi kikubwa kinategemea mvua na umwagiliaji kwa kiasi kidogo.
5.1.1 Usalama wa Chakula
Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023 Wilaya ya Kakonko imevuna wastani wa mazao ya chakula kinachotosheleza mahitaji ya watu waliopo Wilayani na kubakiwa na ziada. Jedwali 1.8 linaonesha mchanganuo wa mahitaji, mavuno na ziada kwa kipindi tajwa.
JEDWALI 1.8 MCHANGANUO WA MAHITAJI, MAVUNO NA ZIADA YA CHAKULA KWA MWAKA 2020/2021-2022/2023
Mwaka
|
Mahitaji (Tani)
|
Mavuno (Tani)
|
Ziada (Tani)
|
2020/2021
|
70,965.08 |
191,875.35 |
120,910.27 |
2021/2022
|
76,374.51 |
157,746.82 |
81,372.31 |
2022/2023
|
71,791.24 |
270,546.86 |
198,755.62 |
Chanzo: Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
JEDWALI 1.9 MCHANGANUO WA USALAMA WA CHAKULA KWA MWAKA 2023
|
IDADI YA WATU 178,419 |
||
|
mahitaji (Tani)
|
mavuno (Tani)
|
ziada (Tani)
|
wanga
|
66,907.13 |
241,552.86 |
174,645.73 |
protini
|
4,884.11 |
28,994.00 |
24,109.89 |
JUMLA YA ZIADA
|
198,755.62 |
Chanzo: Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Kwa mwaka 2023 hali ya mahitaji ya chakula imeshuka kwa sababu kwa miaka ya nyuma makadirio ya mahitaji ya chakula kufanyika kwa kutumia takwimu za makisio ya idadi ya watu ambapo makisio ya idadi ya watu yalikuwa watu 185,977 ila kwa mwaka 2023 makadirio ya mahitaji ya chakula yametumia idadi kamili ya watu ambayo kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi idadi ya watu Halmashauri ya Kakonko ni 178,419
5.1.2 Pembejeo za Kilimo
Hali ya upatikanaji wa pembejeo ni ya wastani kutokana na Kukosekana kwaWafanyabiashara wakubwa wa pembejeo ndani ya Wilaya. Msimu wa mwaka 2021/2022 kulikuwa na wauzaji wadogowadogo 7 wa pembejeo za kilimo na kwa msimu wa 2022/2023 idadi imeongezeka na kufikia 9 ambapo kati ya 1 tu ndo aliruhusiwa kufanya biashara ya mbolea ya ruzuku.
5.1.3 Miradi ya Kilimo.
Halmashauri inashirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo kupitia mashirika ya Enabel kwa Mradi wa SAKiRP na Mashirika ya Umoja wa Mataifa (FAO, WFP, UNCDF na ITC) kupitia Mradi wa Pamoja Kigoma (KJP) kuendeleza kilimo Wilayani. Kupitia Mpango huu, kwa msimu wa 2020/2021 hadi 2022/2023 jumla ya kata 10 za Gwanumpu, Gwarama, Kanyonza, Kasanda, Kakonko, Mugunzu, Katanga, Rugenge, Muhange na Kasuga zimenufaika kwa kuwapatia mafunzo juu ya Mbinu bora za kilimo, zana za kilimo, Kilimo hifadhi na kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kilimo ambayo ni Kituo cha mazao Kabingo, Ujenzi wa madaraja ya kusafirishia mazao Kata ya Kasanda, Gwarama na Kasuga na Ghala la mazau Kata ya Mugunzu
5.1.4 Umwagiliaji
Halmashauri ina jumla ya Skimu za Umwagiliaji 7 zenye eneo lililopimwa lenye ukubwa wa hekta 1,150. Aidha eneo linalolimwa ni hekta 935 na kuajiri wakulima 1,656. Pamoja na kuendelea na uzalishaji, miundombinu ya skimu hizi inatarajiwa kufanyiwa ukarabati kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa skimu nyingine mpya nne.
5.1.5 Ushirika.
Wilaya ina jumla ya vyama vya ushirika 15, ikiwa 14 ni vyama vya Msingi vya mazao na masoko (AMCOS) na 1 ni chama cha msingi cha akiba na mikopo (SACCOS). Vyama hivyo vina jumla ya wanachama 1,794.
5.2 Sekta ya Mifugo na Uvuvi
5.2.1 Mifugo
Ufugaji unaofanywa ni ufugaji huria na ufugaji wa ndani kwa kiasi kidogo. Wilaya ina jumla ya hekta 80,640.2 za eneo la malisho ambazo zinapatikana katika maeneo ya Vijiji 44 vya Wilaya ya Kakonko yaliyotengwa kwa ajili ya kuchungia. Kwa sasa Wilaya inakadiriwa kuwa na mifugo kama inavyoonesha kwenye jedwali 1.10 hapa chini: -
JEDWALI 1.10 : IDADI YA MIFUGO NDANI YA WILAYA.
Idadi na Aina ya mifugo
|
|||||||||
Mwaka
|
Ng’ombe
|
Mbuzi
|
Kondoo
|
Nguruwe
|
Bata
|
Kuku
|
Mbwa
|
Paka
|
Punda
|
2020/2021
|
24,863 |
28,219 |
694 |
2,134 |
1,230 |
68,316 |
1,527 |
81 |
31 |
2021/2022
|
26,518 |
30,311 |
859 |
2,742 |
1,596 |
79,672 |
2,059 |
89 |
35 |
2022/2023
|
27,635 |
32,918 |
933 |
2,925 |
1,640 |
81,416 |
2,063 |
85 |
41 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi.
5.2.1.1 Ujenzi na ukarabati wa miundombinu
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2021/2022, Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kujenga majosho 7 ya Nyamtukuza, Nyakayenzi, Kihomoka, Gwarama, Nyabibuye, Luhuru na Kasanda kwa gharama ya jumla ya Sh.126,000,000.00 ambapo kila josho moja limegharimu Sh.18,000,000.00 kujengwa. Majosho 7 yamejengwa na kukamilika.
Kwa mwaka 2022/23 majosho matano yako kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji katika vijiji vya Kiduduye, Ilabiro, Kikulazo, Kiziguzigu na Itumbiko kwa gharama ya Tsh. 23,000,000/= kila moja na kufanya jumla ya gharama ya majosho yote matano kuwa Tsh. 115,000,000/=
5.2.1.2 Utengaji wa maeneo ya malisho
Halmashauri imetenga eneo la malisho ya mifugo katika vijiji saba (7) kati ya Vijiji 44 lenye ukubwa wa hekta 15,338 katika Vijiji vya Kazilamihunda, Juhudi, Kabare, Gwarama, Rumashi, Nyabibuye na Churazo kwa mipango wa matumizi bora ya Ardhi ya vijiji chini ya ufadhili wa shirika la Ubelgiji la Enabel.
5.2.1.3 Kuimarika kwa Huduma za Ugani kwa Wafugaji.
Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023 Halmashauri imefanikiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za Ugani mfano utoaji chanjo (chambavu, Kideri Homa ya Mapafu ya Ng’ombe na Kichaa cha Mbwa) kwa wastani kutoka asilimia 50 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2023.
5.2.1.4 Hali ya Chanjo ya mifugo
Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, Halmashauri imekuwa ikifanyo zoezi la kutoa chanjo kwa kwa ajili ya kinga ya magonjwa mbalimbali ya mifugo kama inavyoonekana kwenye jedwali 1.11 hapa chini; -
JEDWALI 1.11: Chanjo ya mifugo Kwa kipindi cha Januari 2020 hadi Juni 2023
AINA
|
MWAKA
|
|||
Mifugo
|
Ugonjwa
|
2020/2021
|
2021/2022
|
2022/2023
|
Kuku
|
Mdondo
|
76,416 |
79,672 |
81,416 |
Mbwa
|
Kichaa cha Mbwa
|
1,675 |
1,501 |
1,615 |
Ng’ombe
|
Chambavu
|
4,819 |
3,028 |
9,450 |
Ng’ombe
|
Homa ya mapafu
|
817 |
953 |
1436 |
Ngombe
|
Ugonjwa wa kutupa mimba
|
0 |
95 |
120 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi.
5.2.1.5 Uvishaji wa hereni za kielektroniki
Katika zoezi la uwekaji hereni za Kielektroniki kwa mifugo mpaka wakati Serikali inasimamisha zoezi hili kupitia tamko la waziri Mkuu Bungeni, Halmashauri ya Wilaya Kakonko kupitia mzabuni ilikuwa imeshavalisha hereni kwa ng’ombe wapatao 1,030 na Mbuzi 442.
5.2.2 Uvuvi
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina jumla ya mabwawa ya kuchimbwa ya samaki “Digging ponds” 55.
JEDWALI 1.12: IDADI YA MABWAWA KWA MWAKA 2020/2021-2022/2023
Mwaka
|
2020/2021
|
2021/2022
|
2022/2023
|
Idadi ya mabwawa
|
48 |
55 |
55 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi.
Aidha mchanganuo wa mabwawa yaliyopo ni kama inavyoonekana kwenye jedwali 1.13 hapa chini
JEDWALI 1.13: MCHANGANUO WA MABWAWA
Na.
|
Kata
|
Idadi ya Mabwawa
|
1.
|
Mugunzu
|
10 |
2.
|
Katanga
|
5 |
3.
|
Kiziguzigu
|
4 |
4.
|
Gwarama
|
17 |
5.
|
Nyabibuye
|
6 |
6.
|
Kasanda
|
7 |
7
|
Rugenge
|
4 |
8
|
Kanyonza
|
2 |
Jumla
|
55 |
Chanzo: Idara ya Mifugo na Uvuvi.
6.1 Sekta ya Maliasili (Misitu)
Halmashauri ya Wilaya ina misitu ya asili iliyohifadhiwa na vijiji yenye jumla ya hekta 9,598.43 kati ya hiyo misitu ya hifadhi kwa ajili ya ufugaji nyuki ina jumla ya hekta 3,142.30 na matumizi mengine hekta 6,456.13 Misitu hii ya jamii ni ya aina ya Miyombo yenye mchanganyiko wa aina mbalimbali ambazo ni Mrugwe, Mtundu, Myenzi, Mrama, Mkoyoyo, Mbanga na Mkurungu.
6.2 Sekta ya Ufugaji Nyuki
Jumla ya vikundi 40 vimeungana kuunda Ushirika wa ufugaji nyuki Buyungu (Buyungu Beekeepers Co-operative Society). Wakala wa huduma ya misitu [TFS], Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Kanembwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa sasa kuna jumla ya mizinga ya kisasa 2511 na mizinga 13,690 ya asili (Mianzi) na magogo. Uhamasishaji unaendelea kwa ajili ya utengenezaji wa mizinga ya kisasa. Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na 2021/2022 jumla ya kilo 33,750 za asali zilivunwa.
6.3. Ardhi.
6.3.1 Hali ya Upimaji wa Viwanja.
Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo jumla ya viwanja 521 vilikuwa vimekamilika hatua zote za upimaji kama inavyoonekana kwenye jedwali 1.14 hapa chini
JEDWALI 1.14: HALI YA UPIMAJI WA VIWANJA
Mwaka
|
Idadi |
2020/2021
|
174 |
2021/2022
|
206 |
2022/2023
|
141 |
JUMLA
|
521 |
Chanzo: Idara ya Ardhi
6.3.2 Umilikishwaji na Uandaaji wa Hati Katika Mji wa Kakonko.
Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo jumla ya hati 313 za kimila na 128 za kisheria zimetolewa kwa wanachi kama inavyoonekana kwenye Jedwali 1.15 hapa chini:-
JEDWALI 1.15 HATI ZILIZOTOLEWA KWA MWAKA 2020/2021-2022/2023
Mwaka
|
Hati zisizo za
|
Hati za Kimila
|
Kimila
|
||
2020/2021
|
34 |
104 |
2021/2022
|
46 |
150 |
2022/2023
|
48 |
59 |
JUMLA
|
128 |
313 |
Chanzo: Kitengo cha Ardhi
6.3.3 Ukusanyaji wa kodi Ardhi.
Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, Wilaya imefankiwa kukusanya kodi ya ardhi kama inavyo onesha kwenye jedwali 1.16 hapa chini.
JEDWALI 1.16: UKUSANYAJI WA KODI YA ARDHI
Mwaka
|
Makadirio TZS
|
Makusanyo TZS
|
Makusanyo %
|
Isiyokusanywa TZS
|
2020/2021
|
93,000,000.00
|
19,668,212.00
|
21.15 |
73,331,788.00
|
2021/2022
|
40,000,000.00
|
23,272,716.00
|
58.18 |
16,727,284.00
|
2022/2023
|
50,000,000.00
|
28,105,772.00
|
56.21 |
21,894,228.00
|
JUMLA
|
183,000,000.00
|
71,046,700.00
|
38.82
|
111,953,300.00
|
Chanzo: Kitengo cha Ardhi
6.3.4 Migogoro ya Ardhi
Halmashauri imeendelea kutatua migogoro ya ardhi kila inapojitokeza ili kuhakikisha kwamba hakuna mgogoro mkubwa unaojitokeza wa kuhatarisha amani. Hata hivyo Halmashauri inaendelea na juhudi za kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji ili kuzuia kutokea kwa migogoro ya ardhi. Jedwali 1.17 hapa chini linaonyesha hali ya migogoro ya ardhi vijijini kwa mwaka 2020/2021-2022/2023
JEDWALI 1.17 IDADI YA MIGOGORO YA VIJIJI
Mwaka
|
Idadi ya
Migogoro |
Maelezo |
2020/2021
|
1 |
Eneo la malisho na makazi – Mgogoro ulitatuliwa
|
2021/2022
|
0 |
Hakuna
|
2022/2023
|
0 |
Hakuna
|
Chanzo: Kitengo cha Ardhi
6.3.5 Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi
Halmashauri kwa ufadhili wa shirika la ENABEL imeandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji saba (7) ambavyo ni Kazilamihunda, Juhudi, Kabare, Gwarama, Rumashi, Churazo na Nyabibuye. Mpango huu umefanyika kwa ngazi zote za Vijiji, Kata na Wilaya na kupitishwa na Kamishina wa ardhi.
7.0 Sekta ya Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina vituo 34 vya kutolea huduma za afya ambapo vituo 3 ni vituo binafsi, kama inavyoonesha kwenye jedwali 1.18 hapa chini
JEDWALI 1.18: MGAWANYO WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
MMILIKI
|
ZAHANATI
|
VITUO VYA AFYA
|
JUMLA
|
Serikali – Halmashauri
|
25 |
5 |
30 |
Serikali – JWTZ
|
1 |
|
1 |
Binafsi
|
2 |
1 |
3 |
JUMLA
|
28 |
6 |
34 |
Chanzo: Idara ya afya
HALI YA UHITAJI WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA YA AFYA
Malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hospitali ya Wilaya, kila Kata inakuwa na kituo cha afya na kila Kijiji kinakuwa na Zahanati ili kuwapelekea wananchi huduma kwa ukaribu Zaidi.
Mpaka kufikia Juni 30 2023, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina Hospitali ya Wilaya ambayo imeshaanza kutoa huduma, Kuna vituo vya afya 5 kati ya mahitaji ya vituo vya afya 13 sawa na upungufu wa asilimia 61.54 na Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina zahanati 25 kati ya zahanati 44 sawa na upungufu wa asilimia 31.82 kama ilivyo ainishwa kwenye Jedwali 1.19 hapa chini.
JEDWALI 1.19: HALI YA UHITAJI WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA YA AFYA VYA SERIKALI
|
UHITAJI |
VILIVYOPO |
PUNGUFU |
%UPUNGUFU |
HOSPITALI
|
1 |
1 |
0 |
0.00 |
ZAHANATI
|
44 |
30 |
14 |
31.82 |
VITUO VYA AFYA
|
13 |
5 |
8 |
61.54 |
Chanzo: Idara ya Afya
7.1 Mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamekuwa yakiendelea ambapo kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI imepungua kutoka asilimia 2.7 kwa mwaka 2021/2022 mpaka asilimia 2.02 kwa mwaka 2022/2023. Hali ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali 1.20 hapa chini;
JEDWALI 1.20: HALI YA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
MWAKA
|
2021/2022 |
2022/2023 |
Watu wanaoishi na VVU (HIV positivity rate)
|
2.7% |
2.02% |
Vituo vya kutolea huduma ya UKIMWI (refilling center)
|
14 |
14 |
Vituo vya matunzo na tiba (care and treatment center)
|
4 |
4 |
Kituo cha matunzo na tiba -TRC kambi yawakimbizi Mtendeli
|
1 |
0 |
Chanzo: Idara ya Afya
7.2 Uthibiti wa ugonjwa wa Malaria.
Kwa mwaka 2022/2023 kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria imeongeza kutoka asilimia 33 ya mwaka 2021/2022 hadi asilimia 33.2. Sababu kuu ya ongezeko hilo ni kuisha kwa mradi wa mdau wa unyunyuziaji wa dawa ya ukoko majumbani pamoja na unyunyuziaji katika vyanzo vya mazalia ya Mbu. Halmashauri bado inaendelea na jitihada za kutafuta mdau mwingine pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuweza kuendeleza zoezi la unyunyuziaji na kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Kiwango cha maambukizi ya Malaria baina ya wagonjwa wanaofika vituo vya afya ni kama inavyoonesha kwenye jedwali 1.21 hapa chini:
JEDWALI 1.21 KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA MALARIA
Mwaka
|
Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa wagonjwa
wanoafika katika vituo vya kutolea huduma za Afya. |
2020/2021
|
28% |
2021/2022
|
33% |
2022/2023
|
33.2% |
Chanzo: Idara ya Afya
7.3 Huduma za afya ya uzazi na mtoto
Huduma ya mama na mtoto inatolewa katika vituo 26 vya kutolea huduma za afya. Kwa kipindi cha miaka mitatu vifo vya akina mama vimepungua na hili ni juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama UMATI, AMREF, Marie Stoppes na THPS kupambana kuhakikisha Halmashauri inamaliza vifo vyote vya akina mama wajawazito
Vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 3 kwa mwaka 2021/2022 mpaka kifo 1 kwa mwaka 2022/2023. Hali ya vifo vya akina mama wajawazito ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali 1.22 hapa chini.
JEDWALI 1.23: HALI YA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO
Mwaka
|
Idadi ya vifo vya akina mama
|
2020/2021
|
7 |
2021/2022
|
3 |
2022/2023
|
1 |
Chanzo: Idara ya Afya
7.4 CHF iliyoboreshwa.
Halmashauri ina wanachama 3503 wa CHF iliyoboreshwa ambayo ni sawa na 11.1. Kuna baadhi ya changamoto zinapunguza kasi ya uandikishaji wa CHF changamoto kama kutokulipwa kwa wakati madai ya vituo na zahanati, bei za vipimo, dawa na baadhi ya huduma zingine kutokuwekwa wazi, pia mfumo wa madai kutolipa fomu zote za madai kama madai yalivyo.
7.5 Hali ya Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba
Hali ya upatikanaji wa dawa muhimu ni 87%. Pamoja na upatikanaji huo, maombi ya dawa yanapowasilishwa huletwa dawa baadhi tu na wakati mwingine sio kwa kiwango kilichoagizwa. Pamoja na hayo Halmashauri inaendelea kufanya mawasiliano ya karibu na MSHITIRI ili kusaidia kuleta kwa wakati dawa ambazo hazipatikani kwenye Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD).
7.6 Matibabu ya wazee
Kwa kipindi cha Miaka mitatu 2020/2021- 2022/2023Jumla ya wazee 6,073 wametambuliwa katika kata zote 13 za Wilaya 3,066 kati yao wakiwa wanaume na 3,007 wakiwa wanawake. Pia kuna jumla ya mabaraza ya wazee 58 ambapo baraza 1 ni nganzi ya halmashauri, mabaraza 13 kwa kata zote na mabaraza 44 kwa vijiji vyote. Halmashauri ya Wilaya katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo imetoa huduma za afya kwa wazee bure kulingana na sera na miongozo ya serikali kama inavyoonekana kwenye jedwali 1.24 hapa chini.
JEDWALI 1.24 WAZEE WALIOTAMBULIWA
Mwaka
|
Me |
Ke |
Jumla |
2020/2021
|
2,143 |
2,006 |
4,149 |
2021/2022
|
577 |
623 |
1,200 |
2022/2023
|
346 |
378 |
724 |
Jumla
|
3,066 |
3,007 |
6,073 |
Chanzo: Idara ya Afya
7.7 Uboreshaji wa miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Kwa kipindi cha miaka mitatu 2020/2021- 2022/2023 Halmashauri ya wilaya ya Kakonko ilitengewa kiasi cha Shilingi 4,871,401,494.00 kutoka Serikali Kuu, Mapato ya ndani ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali ya Afya katika Hospitali ya Wilaya, Zahanati na Vituo vya Afya vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.Katika fedha hizo kiasi cha Shilingi 1,342,000,000.00 sawa na asilimia 27.5 kilitengwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021, kiasi cha shilingi 2,211,000,000.00 sawa na asilimia 45.4 kilitengwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na kiasi cha shilingi 1,318,401,494.00 sawa na asilimia 27.1 kilitengwa kwa mwaka 2022/2023.
JEDWALI 1.25: UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
Na
|
Aina ya mradi
|
Chanzo cha fedha
|
Mwaka wa Mapokezi ya fedha
|
hatua ya utekelezaji
|
Kiasi cha Fedha kilichopokelewaTsh
|
1 |
ujenzi wa jengo la utawala, jengo la kufulia, pharmacy, jengo la mionzi, jengo la Maternity Hospitali ya Wilaya
|
SERIKALI KUU
|
2020/2021
|
ujenzi umekamilika
|
1,000,000,000.00 |
2 |
Ukarabati wa zahanati ya kinonko
|
SERIKALI KUU
|
2020/2021
|
ukarabati umekamilika
|
50,000,000.00 |
3 |
Ukarabati wa zahanati ya bukiliro
|
SERIKALI KUU
|
2020/2021
|
ukarabati umekamilika
|
50,000,000.00 |
4 |
Ukarabati wa zahanati ya Kiduduye
|
SERIKALI KUU
|
2020/2021
|
ukarabati umekamilika
|
50,000,000.00 |
5 |
ujenzi wa zahanati ya chilambo
|
WORLD VISION
|
2020/2021
|
ujenzi umekamilika
|
192,000,000.00 |
|
jumla ndogo 2020/2021
|
|
|
|
1,342,000,000.00 |
6 |
Ujenzi wa kituo cha afya Mugunzu
|
TOZO (SERIKALI KUU)
|
2021/2022
|
Ujenzi bado unaendelea
|
500,000,000.00 |
7 |
ujenzi wa jengo la EMD Hospitali ya Wilaya
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
300,000,000.00 |
8 |
ujenzi wa nyumba moja ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
90,000,000.00 |
9 |
Umaliziaji wa Zahanati ya Rusenga
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
Kuweka vigae na dari
|
50,000,000.00 |
10 |
Umaliziaji wa zahanati ya Luhuru
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
uko hatua ya plasta
|
50,000,000.00 |
11 |
ukarabati wa zahanati ya Rumashi
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
ukarabati umekamilika
|
50,000,000.00 |
12 |
Ujenzi wa Wodi ya kina mama zahanati ya Gwarama
|
UNFPA
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
75,000,000.00 |
13 |
Ujenzi wa Kituo cha afya Nyakiyobe
|
SERIKALI KUU
|
2021/2022
|
OPD na maabara zimekamilika maternity complex umaliziaji vyooni
|
500,000,000.00 |
14 |
Ujenzi wa Wodi ya kina mama zahanati ya nyamtukuza
|
WORLD VISION
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
85,000,000.00 |
15 |
Ujenzi wa zahanati ya churazo
|
WORLD VISION
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
200,500,000.00 |
16 |
Ujenzi wa Zahanati ya ilabiro
|
WORLD VISION
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
200,500,000.00 |
17 |
Ujenzi wa zahanati ya Kihomoka (mapato ya ndani)
|
MAPATO YA NDANI
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
55,000,000.00 |
18 |
ujenzi wa zahanati ya Njoomlole (mapato ya ndani)
|
MAPATO YA NDANI
|
2021/2022
|
ujenzi umekamilika
|
55,000,000.00 |
|
jumla ndogo 2021/2022
|
|
|
|
2,211,000,000.00 |
19 |
Umaliziaji wa Zahanati ya Luhuru
|
SERIKALI KUU
|
2022/2023
|
Upo katika hatua ya kupiga plasta
|
50,000,000.00 |
20 |
Umaliziaji wa zahanati ya Rusenga
|
SERIKALI KUU
|
2022/2023
|
Kuweka vigae na dari
|
50,000,000.00 |
21 |
Ujenzi wa wodi tatu za baba, mama na mtoto
|
SERIKALI KUU
|
2022/2023
|
uwekaji wa terazo
|
750,000,000.00 |
22 |
ujenzi wa nyumba za watumishi 2in1 zahanati ya Chilambo
|
WORLD VISION
|
2022/2023
|
ujenzi uko katika hatua ya upauaji
|
246,936,262.00 |
23 |
ujenzi wa nyumba za watumishi 2in1 zahanati ya Churazo
|
WORLD VISION
|
2022/2023
|
ujenzi uko katika hatua ya upauaji
|
221,465,232.00 |
|
jumla ndogo 2022/2023
|
|
|
|
1,318,401,494.00 |
|
JUMLA KUU
|
|
|
|
4,871,401,494.00 |
Chanzo: Idara ya Afya
(C) UJENZI WA MATUNDU YA VYOO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
Pia katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2022/2023 Halmashauri kupitia mradi wa Program ya Maji na Usafi wa Mazingira Afya unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Vimejengwa vyoo na kuweka mifumo ya maji katika vituo vya kutolea huduma za afya 16 kwa jumla ya gharama ya Shilingi 311,608,000.00 ambapo kiasi cha shilingi 176,000,000.00 kilitumika kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kiasi cha shilingi 135,608,000.00 Kilitumika kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ujenzi wa vyoo katika vituo vyote 16 umekamilika. Mchanganuo wa matundu ya vyoo yaliyotengenezwa ni kama ilivyo kwenye jedwali 1.26 hapa chini.
JEDWALI 1.26 MIUNDOMBINU YA CHOO KUPITIA WASH
Huduma
|
Hatua
ukamilishaji |
Jumla Sh.
|
Vituo vya Afya @ 22,000,000.00 kakonko,
Gwanumpu, Nyanzige, Kiduduye, Kazilamihunda, Katanga, Muhange, Nyabibuye, Gwarama, Kasanda, Nyamtukuza na Kabingo |
100% |
242,000,000.00 |
Vituo vya Afya @ 17,408,000.00 Kasongati, Kiga na
Bukirilo |
100% |
52,224,000.00 |
Kituo cha Afya Rumashi
|
100% |
17,384,000.00 |
JUMLA
|
311,608,000.00
|
Chanzo: Idara ya Afya
8.0 Sekta ya Elimu
8.1 Elimu ya Awali na Msingi
Halmashauri wa Wilaya ya Kakonko ina jumla ya shule za Msingi 67 ambapo kati ya hizo shule za Serikali ni 66 na shule binafsi ni 1. Shule zote hizi zinajumuisha wanafunzi wa Elimu ya Awali hadi darasa la VII. Mpaka kufikia Juni 2023 Halmashauri ina Jumla ya wanafunzi 50,911 kuanzia elimu ya awali hadi darasa la saba ambapo kati yao wavulana ni wanafunzi 25,355 sawa na asilimia 49.8 na wasichana ni 25,556 sawa na asilimia 50.2. Aidha idadi ya wanafunzi waliopo shule za Serikali ni 50,776 sawa na asilimia 99.73 na wanafunzi wa shule binafsi ni 135 sawa na asilimia 0.27
Katika shule za Msingi za serikali Kuna jumla ya walimu 578 kati ya mahitaji ya walimu 1189 na hivyo kuna upungufu wa walimu 611. Aidha kwa upande wa elimu ya awali kuna walimu 14 kati ya mahitaji ya walimu 224 hivyo kufanya upungufu kuwa walimu 210.
8.1.1 Hali ya uandikishaji wa wanafunzi
Kwa mwaka wa masomo wa 2023 wanafunzi 6460 wa Elimu ya Awali waliandikishwa kati ya 6123 waliotarajiwa sawa na asilimia 106 ya uandikishaji. Aidha kwa elimu ya Msingi, kwa mwaka wa masomo 2023 wanafunzi 6781 wa elimu ya masingi nwaliandikishwa kati ya wanafunzi 6,054 waliotarajiwa. Hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali imeongezeka kutoka asilimia 46 ya uandikishaji kwa mwaka wa masomo 2022 hadi asilimia 106 ya uandikishaji kwa mwaka 2023. Jedwali lifuatalo hapa chini linaonesha hali ya uandikishaji wa Elimu Awali na Msingi kwa mwaka wa masomo 2021-2023. Mchanganuo wa uandikishaji ni kama ilivyo kwenye jedwali 1.27 hapa chini
JEDWALI 1.27: HALI YA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI
MWAKA |
HALI YA UANDIKISHAJI |
|||||||||
ELIMU YA AWALI |
ELIMU MSINGI |
|||||||||
MALENGO |
Wav
|
Was
|
JUMLA
|
% ya uandikishaji
|
MALENGO
|
wav
|
was
|
JUMLA
|
%
|
|
2021 |
5937 |
1546 |
1565 |
3111 |
52 |
5,175
|
3012 |
3014 |
6026 |
116
|
2022 |
7350 |
1685 |
1696 |
3381 |
46 |
6,090
|
3486 |
3335 |
6821 |
112
|
2023 |
6123 |
3132 |
3328 |
6460 |
106 |
6,054
|
3403 |
3378 |
6781 |
112
|
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi.
8.1.2 MTIHANI WA TAIFA WA UPIMAJI WA DARASA LA NNE (SFNA) NA DARASA LA SABA (PSLE)
Hali ya ufaulu katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne (SFNA) imeshuka kutoka asilimia 78.16 mwaka 2021 hadi asilimia 65.15 mwaka 2022, aidha hali ya ufaulu wa mtihani wa kuhitimu darasa la saba (PSLE) imeshuka kutoka asilimia 73.11 kwa mwaka 2021 hadi asilimia 65 kwa mwaka 2022. Sababu kuu zilizosababisha ufaulu kushuka ni pamoja na ongezeko la Utoro wa wanafunzi ambapo Halmashuri imetoa maelekezo kuanzia kwa walimu wakuu, watendaji wa vijiji, Maafisa Elimu kata, watendaji wa kata, makatibu tawala na wasimamizi wa elimu ngazi ya Halmashauri kuhakikisha wanafuatilia suala la utoro kwa ukaribu na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Hali hii imepunguza utoro wa wanafunzi kwa kiasi kikubwa na matarajio kwa mitihani ijayo ni kuongezeka ufaulu.
Sababu nyingine ni Wazazi kuwa na mwamko mdogo katika masuala ya kielimu mfano kuwakataza watoto wao wasifanye vizuri mitihani ya Taifa ili wasigharamie mahitaji pindi wanapokuwa wamefaulu na kutakiwa kujiunga na kidato cha Kwanza. Wasimamizi wa elimu ngazi ya Halmashauri na wilaya wamekuwa wakitoa elimu kwa wazazi na jamii juu ya umuhimu wa elimu kupitia mikutano na vikao mbalimbali, wazazi ambao wamebainika kuwakataza Watoto wao wasifanye vizuri kuripotiwa kwa watendaji wa vijiji na kuwataka wajieleze kwa maandishi juu ya kutowakataza watoto wao wasifanye vizuri kwenye mitihani ya Taifa. Pia, imeanzishwa programmu ya ushirikiano wa walimu na wazazi (UWAWA) katika kusimamia na kushiriki katika kuleta maendeleo ya shule ikiwa ni Pamoja na kuinua ufaulu wa wanafunzi kwa mitihani ya Taifa. Upungufu wa walimu nao umechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa ufaulu ila matarajio kwa mitihani ijayo ni kuongezeka ufaulu kwani Serikali imeendelea kuajiri walimu wapya katika kukabiliana na changamoto hii ya upungufu wa walimu shuleni.
Katika Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA) na Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi (PSLE) kwa miaka mitatu mfululizo ufaulu ulikuwa kama inavyoonekana katika jedwali 1.28 lifuatalo hapa chini.
JEDWALI 1.28: HALI YA UFAULU SFNA NA PSLE
MWAKA |
WALIOFANYA MITIHANI |
WALIOFAULU SFNA |
WALIOFANYA MTIHANI |
WALIOFAULU PSLE |
||||||
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
%UFAULU
|
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
%UFAULU
|
|||
2020 |
5759 |
2480 |
2452 |
4932 |
85.64
|
2,768.00
|
1138 |
1014 |
2152 |
77.75
|
2021 |
5545 |
2043 |
2291 |
4334 |
78.16
|
3,782.00
|
1442 |
1323 |
2765 |
73.11
|
2022 |
6446
|
1967 |
237 |
4339 |
65.15
|
4,694
|
1655 |
1539 |
3194 |
65 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi.
8.1.3 Fedha za Elimu bila malipo
Katika kipindi kuanzia mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imepokea jumla ya shilingi 1,532,405,576.71Kwa ajili ya uendeshaji wa shule kwa shule za msingi 59 kati ya 66 zilizopo Wilayani kama ifuatavyo kwenye jedwali 1.29.
JEDWALI 1.29 MAPOKEZI YA FEDHA ZA ELIMU BILA MALIPO
Na
|
MWAKA
|
KIASI KILICHOKELEWA (TZS).
|
1
|
2020/2021
|
438,743,958 |
2
|
2021/2022
|
516,526,023 |
3
|
2022/2023
|
577,135,595.71 |
|
JUMLA
|
1,532,405,576.71 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi.
8.1.4 Ujenzi wa miundombinu
Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 – 2022/2023 kupitia fedha zinazotolewa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo, Halmashauri imetekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu kama ilivyo kwenye jedwali 1.30 na 1.31 hapa chini;-
JEDWALI 1.30: UJENZI WA MIUNDOMBINU KWA MWAKA 2021/2022-2022/2023
Na |
MWAKA |
Ujenzi vyumba vya madarasa |
Ukarabati vyumba vya madarasa shule kongwe |
Matundu ya vyoo |
Ujenzi wa nyumba za walimu |
|
|
||||||
|
||||||
1 |
2020/2021
|
19 |
6 |
126 |
0 |
|
2 |
2021/2022
|
23 |
10 |
156 |
0 |
|
3 |
2022/2023
|
11 |
7 |
188 |
7 |
|
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi.
Ujenzi wa Miundombinu ya Darasa kupitia mradi wa BOOST
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imepokea kiasi cha shilingi 1,457,800,000.00 kupitia Mradi wa BOOST kwa ajili ya kujenga miundombinu mipya ya elimu msingi na awali ambapo kiasi cha shilingi 723,000,000.00 sawa na asilimia 49.60 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa shule 2 mpya , kiasi cha shilingi 520,000,000.00 sawa na asilimia 35.67 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 20 vya madarasa, kiasi cha shilingi 71,800,000.00 sawa na asilimia 4.93 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya mfano elimu ya awali, shilingi 33,000,000.00 sawa na asilimia 2.26 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa vyoo matundu 15 na kiasi cha Shilingi 110,000,000.00 sawa na asilimia 7.55 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya walimu 2in1. Mchanganuo ni kama ulivyo kwenye Jedwali 1.31 hapa chini;
JEDWALI 1.31: UJENZI WA MIUNDOMBINU YA DARASA KUPITIA MRADI WA BOOST
Na
|
JINA LA SHULE
|
MRADI
|
IDADI
|
KIASI
|
JUMLA
|
1.00
|
KAZILAMIHUNDA
|
Ujenzi wa Shule Mpya
|
1.00 |
361,500,000.00 |
361,500,000.00 |
2.00
|
NYAMTUKUZA
|
Ujenzi wa Shule Mpya
|
1.00 |
361,500,000.00 |
361,500,000.00 |
|
|
JUMLA NDOGO
|
2.00 |
|
723,000,000.00 |
3.00
|
GWARAMA
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
4.00 |
26,000,000.00 |
104,000,000.00 |
4.00
|
BUKIRILO
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
4.00 |
26,000,000.00 |
104,000,000.00 |
5.00
|
KIGARAMA
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
4.00 |
26,000,000.00 |
104,000,000.00 |
6.00
|
Nyamwirongwe
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
4.00 |
26,000,000.00 |
104,000,000.00 |
7.00
|
Kavungwe
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
4.00 |
26,000,000.00 |
104,000,000.00 |
|
|
JUMLA NDOGO
|
20.00 |
|
520,000,000.00 |
8.00
|
GWARAMA
|
Ujenzi wa madarasa mfano elimu ya awali
|
2.00 |
35,900,000.00 |
71,800,000.00 |
|
|
JUMLA NDOGO
|
2.00 |
|
71,800,000.00 |
9.00
|
GWARAMA
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
3.00 |
2,200,000.00 |
6,600,000.00 |
10.00
|
BUKIRILO
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
3.00 |
2,200,000.00 |
6,600,000.00 |
11.00
|
KIGARAMA
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
3.00 |
2,200,000.00 |
6,600,000.00 |
12.00
|
Nyamwirongwe
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
3.00 |
2,200,000.00 |
6,600,000.00 |
13.00
|
Kavungwe
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo
|
3.00 |
2,200,000.00 |
6,600,000.00 |
|
|
JUMLA NDOGO
|
15.00 |
|
33,000,000.00 |
14.00
|
Nyakivyiru
|
Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu
|
1.00 |
110,000,000.00 |
110,000,000.00 |
|
|
|
1.00 |
|
110,000,000.00 |
JUMLA KUU |
|
|
1,457,800,000.00
|
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi
Jedwali 1.32 hapa chini linaonesha hali ya Miundombinu na samani katika shule za msingi kwa ujumla; -
JEDWALI 1.32 HALI YA MIUNDOMBINU NA SAMANI KATIKA SHULE ZA MSINGI
AINA YA MIUNDOMBINU
|
MAHITAJI
|
ILIYOPO
|
UPUNGUFU
|
OFISI YA WALIMU
|
170 |
98 |
72 |
MADARASA
|
1205 |
580 |
625 |
NYUMBA ZA WALIMU
|
1157 |
209 |
948 |
VYOO
|
2297 |
934 |
1363 |
MADAWATI
|
16142 |
12125 |
4017 |
Chanzo: Idara ya Elimu Msingi.
8.2.0 Elimu ya Sekondari.
Kwa Mwaka 2022/2023 Halmashauri ina jumla ya shule 20 za sekondari, kati ya hizo 16 ni za Serikali na 4 zisizo za Serikali zenye jumla ya wanafunzi 9,461 kati ya hao wavulana ni 4943 na wasichana 4518. Halmashauri ina shule moja ya kidato cha kwanza hadi cha sita ambayo ni Kakonko sekondari na shule 1 ya kidato cha tano na sita inayotarajia kupokea wanafunzi mwezi Julai 2023 ambayo ni shule ya sekondari Amani Mtendeli. Halmashauri ina jumla ya walimu 186 kati ya 280 wanaohitajika hivyo kuwa na upungufu wa walimu 94 kwa shule za Serikali sawa na asilimia 33.57. Kati ya walimu waliopo wanaofundisha masomo ya sayansi na hisabati ni 93 na Sanaa ni 93. Vile vile Halmashauri ina wataalam wa maabara 3 kati ya 16 ya uhitaji hali inayopelekea upungufu wa wataalam 13 wa maabara.
8.2.1 Hali ya Uandikishaji
Halmashauri inatekeleza sera ya elimu bila malipo kwa upande wa sekondari kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye sifa anadahiliwa kidato cha kwanza. Kwa mwaka 2023 Halmashauri imedahili wanafunzi 3,187 kati ya 3,198 waliolengwa sawa na asilimia 99.7. Hali ya uandikishaji ni kama ilivyo kwenye jedwali 1.33 hapa chini.
JEDWALI 1.33: HALI YA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI SHULE ZA SEKONDARI
Mwaka
|
Maoteo
|
Walioandikishwa
|
Uandikishaji %
|
2020/2021
|
1834 |
1670 |
91.05 |
2021/2022
|
2,134 |
1,941 |
91 |
2022/2023
|
3198 |
3187 |
99.7 |
Chanzo: Elimu Sekondari
8.2.2 Hali ya ufaulu
Hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha pili umepungua kutoka asilimia 90 mwaka 2021 hadi asilimia 86.8 mwaka 2022. Kwa upande wa kidato cha nne ufaulu umeshuka kutoka 88.7% mwaka 2021 hadi 85% kwa mwaka 2022. Aidha ufaulu kwa kidato cha sita umeongezeka kutoka 99% mwaka 2021 hadi 100% mwaka 2022. Sababu kuu ya kushuka kwa ufaulu wa mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne ni ongezeka la wanafunzi wanaotoroka kipindi cha masomo kuja kufanya mitihani kipindi cha mitihani. Kutokana na utafiti uliofanywa na Idara za Elimu Msingi na Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mwaka 2022 matokeo ya utafiti yalionyesha ongezeko la utoro linasababishwa na ukosefu wa chakula cha kutosha shule na ubovu wa miundombinu ya kujifunzia na ujifunzaji. Aidha Halmashauri imeshachukua hatua mbalimbali zitakazosaidia kupunguza utoro ili hali ya ufaulu iweze kupanda ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uwepo wa vyakula shuleni kuboresha miundombinu na kuwachukulia hatua kali wale wanaowasababishia wanafunzi kutoroka au kuacha shule. Sababu nyingine ni uhaba wa walimu ambapo Serikali imeendelea kuajiri walimu hivyo utatuzi wa changamoto hii itasaidia kwa kiasi kikubwa ufaulu kuongezeka. Mchanganuo wa ufaulu ni kama jedwali 1.34 linavyobainisha hapa chini:-
JEDWALI 1.34: HALI YA UFAULU WA MITIHANI KWA KIDATO CHA PILI, KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA
MWAKA
|
KIDATO
|
WALIOFANYA
|
WASIOFANYA
|
MADARAJA YA UFAULU
|
% YA
UFAUL U |
|||||||||
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
I
|
II
|
III
|
IV
|
0
|
JML
|
|||
2020
|
II
|
814 |
819 |
1633 |
65 |
38 |
103 |
146 |
137 |
225 |
965 |
156 |
1633 |
90.2 |
IV
|
562 |
526 |
1088 |
3 |
10 |
13 |
68 |
169 |
179 |
521 |
151 |
1088 |
86 |
|
VI
|
2 |
31 |
33 |
0 |
0 |
0 |
10 |
21 |
2 |
0 |
0 |
33 |
100 |
|
2021
|
II
|
784 |
717 |
1501 |
49 |
27 |
76 |
141 |
164 |
201 |
842 |
157 |
1501 |
90 |
IV
|
646 |
571 |
1217 |
7 |
7 |
14 |
48 |
194 |
202 |
636 |
137 |
1217 |
88.7 |
|
VI
|
142 |
72 |
214 |
0 |
0 |
0 |
34 |
116 |
63 |
1 |
0 |
214 |
100 |
|
2022
|
II
|
872 |
762 |
1634 |
29 |
29 |
58 |
73 |
110 |
206 |
1007 |
234 |
1630 |
86.8 |
IV
|
702 |
674 |
1376 |
5 |
10 |
15 |
52 |
133 |
211 |
762 |
203 |
1361 |
85 |
Chanzo: Idara ya Elimu Sekondari.
8.2.3 Hali ya miundombinu katika shule za sekondari
Kwa mwaka 2023 kuna miundombinu ambayo ina upungufu kutokana na mahitaji na kuna miundombinu mingine ina ziada ukilinganisha na mahitaji. Hali ya miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika shule za sekondari ni kama ifuatavyo kwenye jedwali 1.35 hapa chini
JEDWALI 1.35 HALI YA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
AINA YA MIUNDOMBINU
|
MAHITAJI
|
ILIYOPO
|
UPUNGUFU/ZIADA
|
% UPUNGUFU/ZIADA
|
MAABARA
|
45 |
17 |
28 |
62.22 |
MADARASA
|
204 |
252 |
48 |
23.53 |
NYUMBA ZA WALIMU
|
187 |
70 |
117 |
62.57 |
VYOO
|
394 |
243 |
151 |
38.32 |
MAJENGO YA UTAWALA
|
16 |
10 |
6 |
37.50 |
HOSTELI
|
69 |
21 |
48 |
69.57 |
MEZA
|
8350 |
9324 |
974 |
11.66 |
VITI
|
8350 |
9323 |
973 |
11.65 |
Chanzo: Idara ya Elimu Sekondari.
8.2.4 Mapokezi ya fedha za elimu bila malipo kwa sekondari.
Katika kipindi kuanzia mwaka 2020/2021 hadi mwezi Juni 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imepokea jumla ya shilingi 1,479,199,249 za Elimu Bila Malipo kwa shule kwa shule zote 12 za sekondari kama ifuatavyo kwenye jedwali 1.36 hapa chini:
JEDWALI 1.36 MAPOKEZI YA FEDHA ZA ELIMU BILA MALIPO
Na
|
MWAKA
|
KIASI KILICHOPOKELEWA (Shilingi).
|
1
|
2020/2021
|
401,132,422 |
2
|
2021/2022
|
476,833,333 |
3
|
2022/2023
|
601,233,494.07 |
|
JUMLA
|
1,479,199,249 |
Chanzo: Idara ya Elimu Sekondari.
9.0 Uwezeshaji Wananchi kiuchumi
9.1. Sekta ya Maendeleo ya Jamii
9.2 Uanzishaji wa vikundi vya Kiuchumi
Kwa kipindi cha mwaka 2020/2021- 2022/2023. Halmashauri imefanikiwa kusajili vikundi 242 vyenye jumla ya wanachama 2338 ambapo kati yao wanachama 628 sawa na asilimia 26.86 ni wanaume na wanachama 1710 sawa na asilimia 73.14 ni wanawake. Katika kipindi hicho idara ya Maendeleo ya Jamii imetoa mafunzo ya kuweka na kukopa kwa wanachama 1,145 ambapo kati yao wanaume ni 405 na wanawake ni 740
9.3 Utoaji wa Mikopo inayotokana na tengo la 10% ya Mapato ya ndani
Kwa kipindi cha miaka mitatu 2020/2021 – 2022/2023 jumla ya vikundi 64 vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu viliwezeshwa jumla ya shilingi 425,724,770 kama ifuatavyo kwenye jedwali 1.37 hapa chini: -
JEDWALI 1.37: UKOPESHAJI KWA VIKUNDI
Mwaka
|
Idadi ya Vikundi
|
Kiasi TZS
|
2020/2021
|
18 |
99,484,000 99,484,000 99,484,000 |
2021/2022
|
25 |
164,240,770 |
2022/2023
|
21 |
162,000,000 |
Jumla
|
64 |
425,724,770
|
Chanzo: Idara ya Maendeleo ya Jamii
9.4 Kiasi cha fedha kilichopokelewa TASAF III Awamu ya pili
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2022/2023 jumla ya shilingi 5,135,280,085.00 zilipokelewa ikiwa ni fedha kwa ajili ya Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini. Jedwali 1.38 hapa chini linaonesha mapokezi kila mwaka.
JEDWALI 1.38: MAPOKEZI YA FEDHA ZA TASAF
Mwaka
|
Mapokezi
|
2020/2021
|
1,395,313,920.00 |
2021/2022
|
2,272,600,860.00 |
2022/2023
|
1,467,365,305.00 |
JUMLA
|
5,135,280,085.00
|
Chanzo: Ofisi ya TASAF Wilaya
NB;Unaweza kupakua nakala ya wasifu wa Halmashauri hapa chini;
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa