TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA DIVISION YA ELIMU SEKONDARI
1.UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ina jumla ya shule 19, kati ya hizo 15 ni za Serikali na 4 zisizo za Serikali zenye jumla ya wanafunzi 8004 kati ya hao wavulana ni 4219 na wasichana 3785, kuna shule moja tu ya serikali yenye kidato cha kwanza hadi cha sita ambayo ni Kakonko sekondari. Taarifa hii inahusisha Ujenzi wa miundombinu ya shule, Ukusunyaji wa Takwimu kwenye Madodoso ya TSS (Takwimu Shule za Sekondari), maandalizi ya michezo ya UMISSETA, maandalizi ya mitihani ya UTAMILIFU na maandalizi ya kuwapokea watumishi wa ajira ya walimu wapya.
2. Utekelezaji wa Ukamilishaji wa maabara, na vyumba vya madarasa
2.1 Ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa kutumia nguvu za wananchi na fedha za mfuko wa Jimbo
Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na wananchi inaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kukamilisha vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari za Mugunzu na Rugenge ili kupungunza msongamano wa wanafunzi darasani. Vyumba hivyo vimefikiwa hatua mbalimbali kama ifuatavyo:-
Jedwali Na 1: Hali ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa
Na
|
Kata
|
Jina la Shule
|
Idadi ya vyumba vya madarasa
|
Gharama iliyotumika mpaka sasa
|
Hatua ya ujenzi
|
Maoni
|
1.
|
Mugunzu
|
Mugunzu
|
1 |
4,034,625 |
boma liko kwenye hatua ya ukamilishaji
|
Fedha zimekwisha
|
2.
|
Rugenge
|
Rugenge
|
2 |
3,500,000 |
Maboma yameezekwa
|
Fedha zikwisha
|
2.2 Ujenzi wa shule mpya ya Katanga kwa kutumia fedha za SEQUIP
Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa kujenga shule mpya ya Katanga kwa kutumia fedha ya progamu ya kuboresha elimu (SEQUIP) kwa ajili ya kuondoa msonamano wa wanafunzi darasani na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea kufuata shule. Mwaka wa fedha 2021/2022 mnamo mwezi Novemba 2021 Halmashauri ilipokea kiasi Tsh. 4700,000,000.00 kwa ajilia ya kujenga majengo yafuatayo; Jengo la utawala, vyumba 3 vya maabara, vyumba 8 vya madarasa, maktaba, jengo la TEHAMA na matundu 20 ya vyoo.
Jedwali na 2: Hatua za ujenzi wa shule mpya Katanga
NA |
KATA |
SHULE |
AINA YA JENGO |
IDADI YA VYUMBA |
HATUA |
1.
|
KATANGA
|
KATANGA
|
Utawala |
1 |
Upauaji
|
Madarasa |
8 |
Upauaji
|
|||
Maabara |
3 |
Upauaji
|
|||
Maktaba
|
1 |
Lenta
|
|||
TEHAMA |
1 |
Boma limekamilika.
|
|||
Vyoo |
Matundu 20 |
Ujenzi wa boma
|
|||
|
Mfumo wa maji |
6 |
Maji yamefikishwa site, matanki hayajasimikwa.
|
2.3 Umaliziaji wa vyumba 5 vya maabara
Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa kuboresha maabara za sayansi. Mwaka wa fedha 2021/2022 mnamo mwezi Februari 2022 Halmashauri ilipokea kiasi Tsh. 150,000,000.00 kama jedwali lilivyobainishwa hapa chini:
Jedwali na 3. Umaliziaji wa vyumba vya maabara
NA
|
KATA
|
SHULE
|
IDADI YA VYUMBA
|
KIASI
|
MAELEZO
|
1.
|
Mugunzu
|
Mugunzu
|
1 |
30,000,000
|
Ujenzi umekamilika
|
2.
|
Gwanumpu
|
Gwanumpu
|
1 |
30,000,000
|
Ujenzi umakamilika
|
3
|
Rugenge
|
Rugenge
|
1 |
30,000,000
|
Ujenzi umekamilika
|
4
|
Gwarama
|
Muhange
|
1 |
30,000,000
|
Ujenzi umekamilika
|
5
|
Nyamtukuza
|
Nyamtukuza
|
1 |
30,000,000
|
Ujenzi umekamilika
|
JUMLA
|
5 |
150,000,000
|
|
3. Ukusunyaji wa Takwimu kwenye Madodoso ya TSS (Takwimu Shule za Sekondari)
Ukusanyaji wa Takwimu kwa kutumia madodoso ya Takwimu Shule za Sekondari (TSS) ulianza kufanyika kuanzia tarehe 31.3.2022 katika Ngazi za Halmashauri, zoezi hili huhusisha sensa ya rasilimali vitu na watu walioko katika shule zote za sekondari. Zoezi hili limefanyika kwa kushirikisha wakuu wa shule, Maafisa Elimu Kata, Afisa Elimu Sekondari. Ofisi ya mipango kitengo cha takwimu pamoja na Afisa Tehama Wilaya. Takwimu na taarifa zote za shule za serikali na binafsi zimeingizwa kwenye Madadoso ya “Takwimu Shule za Sekondari” (TSS) na kwenye mfumo wa “Annual School Census” (ASC) unaosimamiwa na OR-TAMISEMI.
4. Ufanyikaji wa mtihani wa Taifa wa Kidato cha 6 Mei, 2022
Wilaya kupitia Kamati ya mtihani ya Wilaya imesimamia ufanyikaji wa mtihani wa Taifa wa kidato cha 6 mnamo mwezi mei, 2022 katika shule yenye kidato cha 5 na 6 ya Kakonko Sekondari kama jedwali linavyoonesha hapa chini:-
Jedwali na 4. Idadi ya watahiniwa
WALIOSAJILIWA
|
WALIOFANYA
|
WASIOFANYA
|
% YA WALIOFANYA
|
% YA WASIOFANYA
|
||||||
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
100 |
- |
142
|
72
|
214
|
142
|
72
|
214
|
0
|
0
|
0
|
5. Ufanyikaji wa mtihani Utimilifu (Mock) wa Mkoa mwezi Mei, 2021
Wilaya kupitia Uongozi wa Elimu Mkoa na Wilaya imesimamia ufanyikaji wa mtihani wa Mtihani wa mock mkoa mnamo mwezi mei, 2022 katika shule zote za Sekondari za mkoa wa Kigoma. Waliofanya Kakonko sekondari ni kama jedwali linavyoonesha hapa chini:-
Jedwali na.5 Idadi ya wanatahiniwa wa mtihani wa Taifa kidato cha 6
WALIOSAJILIWA
|
WALIOFANYA
|
WASIOFANYA
|
% YA WALIOFANYA
|
% YA WASIOFANYA
|
||||||
wv
|
ws
|
jml
|
wv
|
ws
|
jml
|
wv
|
ws
|
jml
|
100
|
-
|
142
|
72
|
214
|
142
|
72
|
214
|
0
|
0
|
0
|
9. Changamoto na Mikakakati
9.1 Changamoto
Idara imeendelea kukabiliana na changamoto zifuatazo:
9.2 Mikakati
Idara inaendelea kusimamia mikakati ya kupunguza au kuondoa changamoto kama ifuatavyo;
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa