TAARIFA YA SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI ZA DIVISION YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI
i. Kuratibu na kusimamia shughuli za michezo ya UMITASHUMTA kwenye ngazi ya Shule na Kata.
Michezo iliyoshindanishwa ni Mpira wa miguu, Mpira wa pete, Mpira wa wavu, Riadha, (Wenye Mahitaji Maalum) na Kwaya. Michezo hiyo ilifanyika kama ilivyokusudiwa na washiriki wenye ubora waliojitokeza walichaguliwa na kuunda timu ya Kanda kwenye maeneo yao. Pia, wanamichezo waliochaguliwa kutoka ngazi ya Kanda waliunda timu ya Halmashauri. Aidha, Michezo ngazi ya Kanda na Kambi ya timu ya Halmashauri vilikusudiwa kuanza mapema mwezi Julai na kambi ya wilaya ilipangwa kuwa Shule ya Msingi Itumbiko kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ngazi ya Mkoa.i. Kuratibu na kusimamia shughuli za michezo ya UMITASHUMTA kwenye ngazi ya Shule na Kata. Michezo iliyoshindanishwa ni Mpira wa miguu, Mpira wa pete, Mpira wa wavu, Riadha, (Wenye Mahitaji Maalum) na Kwaya. Michezo hiyo ilifanyika kama ilivyokusudiwa na washiriki wenye ubora waliojitokeza walichaguliwa na kuunda timu ya Kanda kwenye maeneo yao. Pia, wanamichezo waliochaguliwa kutoka ngazi ya Kanda waliunda timu ya Halmashauri. Aidha, Michezo ngazi ya Kanda na Kambi ya timu ya Halmashauri vilikusudiwa kuanza mapema mwezi Julai na kambi ya wilaya ilipangwa kuwa Shule ya Msingi Itumbiko kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ngazi ya Mkoa.
ii. Kuhesabu vifaa na mali za Halmashauri kwenye Shule zote na Makao Makuu ya Halmashauri kufikia Juni 30, 2022.
iii. Kufanya maandalizi ya Mtihani wa MOCK Mkoa uliotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2022.
Hii ilienda sambamba na uhimizaji wa utoaji wa michango toka shuleni, kupokea risiti za michango hiyo, kuandaa orodha ya wasimamizi watarajiwa na kuwasiliana na uongozi wa Mkoa kwa maelekezo mbalimbali. Watahiniwa 4,925 ikiwa (Wav. 2,384, Was. 2,541) wa Shule za Msingi 60 kati ya 66 za Serikali walitarajiwa kufanya Mtihani huo.
iv. Kujaza na kuingiza Takwimu za wanafunzi na Miundombinu kwenye Mfumo wa ASC (Annual School Censu) maarufu kama Sensa Elimu Msingi.
Fomu za madodoso ya TSM, TSA na TWM zilihusika. Zoezi hilo huanzia ngazi ya Mtakwimu wa Shule, Mwalimu Mkuu, Afisa Elimu Kata, Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Halmashauri na Afisa Elimu wa Wilaya.
v. Kuendelea kupitia na kurekebisha dosari zilizobainika wakati wa uingizaji wa takwimu kwenye mfumo wa Sensa Elimu Msingi na kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na Watakwimu wanaosimamia Mkoa wetu walioko OR – TAMISEMI.
vi. Kupokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wenye Mahitji Maalum kwenye Bweni letu lililoko shule ya msingi Itumbiko.
Vifaa vilivyopokelewa kutoka kwa wadau washirika ni kama inavyoonesha kwenye jedwali hili:
NA
|
JINA LA MDAU
|
AINA YA KIFAA
|
IDADI
|
1.
|
Help Age International
|
-Magodoro
-Vyandarua -Blanketi |
80
80 80 |
2.
|
Save the Children
|
-Magodoro
-Vyandarua -Tenki (1000 Lt) -Ndoo |
30
80 01 40 |
vii. Kufanya kikao na Wasimamizi wa Elimu ngazi ya Shule na Kata kwa lengo la kuhimiza usimamizi na utoaji wa Taaluma shuleni.
Kubaini vikwazo na changamoto zinazokabili utekelezaji wake na namna ya kuzitatua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
viii. Divisheni ilipokea miche ya miti kutoka kwa wadau wawili ambao ni Maliasili na Serikali za vijiji husika na kuzigawa kwenye shule zake kwa lengo la kutunza mazingira kama inavyoonesha kwenye jedwali lifuatalo:
NA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA MICHE
|
MHUSIKA
|
1.
|
Kinonko
|
500
|
Maliasili
|
2.
|
Kasongati
|
30
|
Maliasili
|
3.
|
Luhuru
|
430
|
Maliasili 30, Serikali ya Kijiji 400.
|
4.
|
Kagondo
|
250
|
Maliasili
|
5.
|
Kasuga
|
600
|
Serikali ya kijiji
|
6.
|
Katahokwa
|
250
|
Serikali ya Kijiji
|
7.
|
Kazilamihunda
|
2000
|
Serikali ya Kijiji
|
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa