Kitengo kimejikita hasa kwenye Eneo Moja lenye Sehemu Tano,
UTEKELEZAJI.
1. USAFI WA MAZINGIRA NA UKAGUZI WA NYUMBA ZA BIASHARA.
Kazi ya ukaguzi wa Nyumba za kuishi, imefanyika kwa kushirikiana na Maafisa watendaji kata, vijiji pamoja maafisa Afya, ili jamii iishi katika mazingira yaliyo safi na salama.
Katika ukaguzi huo, wakuu wa kaya wamehamasishwa kutunza mazingira yao kwa kuyaweka katika hali Safi muda wote, sambamba na kuzingatia usafi Binafsi.
Wananchi Wote waliopatikana na Adha au Chukizo walipewa Ushauri wa Kiafya, ili kuondoa Machukizo yaliokutwa.
Aidha, ukaguzi huo umehamasisha wafanyabiashara wa soko kuu la Kakonko, kuendelea kutumia Meza kwa ajili ya kuuza Bidhaa zao zikiwa juu, badala ya kuuzia chini, ambapo utekelezaji unaendelea kudumishwa kwa wafanyabiashara wote, Sambamba na kuhimiza wafanyabiashara wote na wananchi kwa ujumla wanao tumia soko hilo, kutunza huduma ya chanzo cha Maji (GATI) lililowekwa na Mamlaka ya Maji (RUWASA) Kakonko, kwa lengo la kuboresha Afya ya Jamii, ili kujikinga na Magonjwa yatokanayo na utumiaji wa Maji YASIO SAFI NA SALAMA. Mfano Kipindupindi, Homa ya Matumbo, Kuhara au Kuhara Damu na Magonjwa mengine kama hayo.
TAKWIMU YA UKAGUZI NA USAFI WA MAZINGIRA NGAZI YA KAYA
Na.
|
WALIO KAGULIWA
|
ILANI TOLEWA
|
ILANI TEKELEZWA
|
ILANI BILA TEKELEZWA
|
HATUA CHUKULIWA
|
1
|
216 (NYUMBA ZA KUISHI) |
19 |
14 |
5 |
Ilani ya siku 14 imetolewa
|
2
|
21 (NYUMBA ZA BIASHARA) |
32
|
30 |
2 |
Nyumba mbili za Biashara zimepewa Iani ya Maandishi, siku 21 kufanya marekebisho
|
Kitengo cha Usafi na Mazingira kimehamasisha wananchi, Wafanya Biashara, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji (Zoezi hili limefanyika Kata ya Kakonko) kutambua umuhimu wa kutunza Taka ngumu, kuweka Mji wetu katika hali Safi na Mandhari ya Kupendeza. kufuatia uhamasishaji huo wananchi.
Aidha, zoezi la uzoaji Taka linaendelea ndani ya robo hii ya Nne, 2021/2022 kwa kuwatangazia wananchi, wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali ili kutambua Ratiba ya Ukusanyaji wa Taka kwenye Vitongoji.
Wananchi wanahamasishwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni (Kibuyu Chirizi) baada ya kutoka chooni na kabla ya kuanza kufanya shughuli yoyote ya kijamii.
Elimu hii hutolewa wakati wa ukaguzi wa nyumba za kuishi kwenye jamii kwa kushirikiana na watendaji Kata, Vijiji na wenyeviti wa Vitongoji, wakiongozwa na Timu ya Maafisa Afya.
Maeneo yaliopewa kipaumbele ni wafanyabiashara na ngazi ya jamii.
Shughuli iliyotekelezwa ni kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya 2004 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2005, Sheria ya Afya ya Jamii namba 1 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.
Ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa vizuri na kafanya maji yapatikane kwa wingi, ili kuendelea kujikinga na Magonjwa mbalimbali yanayoweza kuenezwa kwa kukosa huduma ya Maji ya kutosha na yalio safi na salama na kutunza vyanzo hivyo kuwa na Tija Mazingira na Vizazi vijavyo.
Pia Jamii kwa ujumla, wamepewa elimu ya kutibu maji kwa kutumia njia mbalimbali mfano:-
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa