• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe |
Kakonko District Council
Kakonko District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Mawasiliano
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Usafishaji Na Mazingira
        • Elimu Msingi
        • Elimu ya Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maji
        • Maendeleo ya Jamii
        • Utumishi na Utawala
        • Fedha na Biashara
        • Maliasili, Ardhi na Mazingira
        • Kilimo cha Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Ujenzi na Zimamoto
      • Vitengo
        • Ugavi na Manunuzi
        • Tehama na Habari
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ufugaji Nyuki
        • Uchaguzi
        • Sheria
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Livestock
    • Fisheries
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Usimamizi
      • Elimu Afya na Maji
      • Huduma za Kiuchumi Ujenzi na Mazingira
      • Udhibiti wa UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
        • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayo tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

Maliasili, Ardhi na Mazingira

Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira kinatekeleza majukumu yake kupitia sekta za Maliasili na Hifadhi ya Mazingira. Shughuli za Idara ni pamoja na;

  • Kukusanya maduhuli ya Halmashauri. Jumla ya TZS 10,279,000.00 zimekusanywa kama ushuru wa Halmashauri kutokana na mazao ya misitu.
  • Kuhakikisha uwepo wa matumizi bora, endelevu na ulinzi wa kisheria wa maliasili unaimarika kwa kuwajengea uwezo wa kitaasisi katika ngazi za vijiji. Ambapo Kamati za Maliasili za Vijiji vya Kinonko na Kanyonza ziliundwa na kupata mafunzo ya usimamizi wa maliasili.
  • Kusimamia Sera ya ufugaji nyuki ya mwaka 1998 ambapo Ofisi ya Maliasili ilipokea mizinga 24 ya kisasa (topbar hive) kutoka FAO na mizinga hiyo inapendekezwa kutundikwa  katika shamba darasa la Halmashauri ya Wilaya. Ili kuongeza ufanisi katika kujifunza kwa vitendo na kuboresha shamba darasa la Halmashauri.
  • Kudhibiti matukio ya uchomaji moto katika misitu ya Vijiji na mashamba binafsi. Ambapo Vijiji vyote vilielimishwa juu ya sheria Mama na sheria ndogo ya Hifadhi ya mazingira juu ya moto kupitia barua na kufahamishwa kuwa hairuhusiwi kuanzisha moto bila kuwa na kibali ambacho kiliambatishwa kwenye barua hizo kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
  • Kufanya taathimini ya eneo kwa ajili ya kuanzisha shamba la miti la mfano la Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kijiji na wadau wa mazingira DRC. Eneo limepatikana Kijiji cha Mugunzu lenye ukubwa wa hekta 75 kwa kukadria ambapo linaweza kupandwa miti isiyo pungua 120,000 kwa umbali wa (2.5 x2.5)m na Kamati za Maliasili ya kijiji pamoja na kamati ya usimamizi wa bustani ya miti na shamba tayari zimundwa kwa ajili ya kusimmia utekelezaji.
  • Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani(05.06.2022) ambayo ilifanyika Kiwilaya katika hospitali ya Wilaya ya Kakonko kwa kushirirkiana na wadau wa mazingira (DRC, REDESO na World vision Tanzania) shughuli za uhifadhi wa mazingira kama upandaji miti, usafi wa mazingira na maonyesho ya shughuli mbalimbali na mazao yatokanayo na shughuli hizo yalionyeshwa. (asali na nta, mkaa mbadala, majiko sanifu na vifaa vinavyotumika kutengenezea) pamoja na elimu ya uhifadhi wa mazingira ilitolewa kwa wananchi walioudhuria.

Pamoja na majukumu hayo, Kitengo inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo:-

  • Uhaba wa watumishi katika sekta ya Wanyamapori. Kwa upande wa sekta ya Wanyamapori hali hairidhishi kwani sekta haina mtumishi hata mmoja.
  • Uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kama hifadhi za misitu ya Vijiji, misitu ya Halmashauri na maeneo ya umma kwa shughuli mbalimbali hasa kilimo cha kuhamahama.

Kitengo imeandaa mikakati ifuatayo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo:-

  • Kuomba idhini ya watu wanaoomba kujitolea katika kazi ambazo hazitaathiri ufanisi wa Kitengo
  • Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi katika maeneo mbalimbali ya vijiji ikiwemo kushirikisha Idara ya Kilimo na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wakulima wanazingatia kilimo kinachojali hifadhi ya mazingira.
  • Kuhamasisha vijiji viandae mipango ya matumizi bora ya ardhi ambayo itabainisha matumizi mbalimbali na kuhakikisha kwamba maeneo yaliyotambuliwa kama hifadhi kwenye mipango hiyo yanalindwa kwa mujibu wa sheria ndogo za vijiji.
  • Kuendelea kuhamasisha vijiji kutenga misitu yake ya hifadhi.
  • Kuwezesha uandaaji mipango ya usimamizi shirikishi wa misitu ya hifadhi ya vijiji pamoja na mipango ya uvunaji endelevu.
  • Kuanzisha shamba la miti ya kupanda ya halmashauri katika eneo la Mtendeli.

 Ardhi.

4.4.1 Hali ya Upimaji wa Viwanja.

Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo jumla ya viwanja 503 vilikuwa vimekamilika hatua zote za upimaji kama ifuatavyo;


Mwaka

Idadi

2019/2020

123

2020/2021

174

2021/2022

206

2022/2023

7

JUMLA

503


                         Chanzo: Idara ya Ardhi

4.4.2 Umilikishwaji na Uandaaji wa Hati Katika Mji wa Kakonko.

Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo jumla ya hati 624 za kimila na 98 za kisheria zimetolewa kwa wanachi kama ifuatavyo;


Mwaka
Hati zisizo za kimila
Hati za Kimila
2019/2020

18

370

2020/2021

34

104

2021/2022

46

150

2022/2023

17

13

JUMLA

115

637


 

Ardhi.

Katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, Wilaya imefankiwa kukusanya kodi ya ardhi kama inavyo onesha kwenye jedwali hapa chini.


Mwaka
Makadirio TZS
Makusanyo TZS
Makusanyo % 
Isiyokusanywa TZS
2019/2020

35,000,000.00

33,985,602.00

97

1,014,398.00

2020/2021

93,000,000.00

19,668,212.00

20.93

73,331,788.00

2021/2022

40,000,000.00

23,272,716.00

58.18

    16,727,284.00

JUMLA

168,000,000.00

76,926,530.00

 

91,073,470.00


Chanzo: Kitengo cha Ardhi

4.4.4  Migogoro ya Ardhi

Halmashauri imeendelea kutatua migogoro ya ardhi kila inapojitokeza ili kuhakikisha kwamba hakuna mgogoro mkubwa unaojitokeza wa kuhatarisha amani. Hata hivyo Halmashauri inaendelea na juhudi za kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji ili kuzuia kutokea kwa migogoro ya ardhi.

Idadi ya migogoro ya Vijiji

Mwaka 
Idadi ya migogoro
Maelezo 
2019/2020

0

Hakuna
2020/2021

1

Eneo la malisho na makazi – Mgogoro ulitatuliwa
2021/2022

0

Hakuna

 

 4.4.5 Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi

Halmashauri kwa ufadhili wa shirika la ENABEL imeandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji saba (7) ambavyo ni Kazilamihunda, Juhudi, Kabare, Gwarama, Rumashi, Churazo na Nyabibuye. Mpango huu umefanyika kwa ngazi zote za Vijiji, Kata na Wilaya na kupitishwa na Kamishina wa ardhi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - WAKUSANYA MAPATO January 30, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. June 18, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA YA WAOMBAJI NAFASI YA UKUSANYAJI MAPATO WALIOITWA KWENYE USAILI January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA VITENDO - WAOMBAJI KAZI YA DEREVA II November 17, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WASISITIZWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.

    April 29, 2025
  • UANZISHWAJI WA MFUMO WA UTHIBITI UBORA WA SHULE WATAJWA KUWA CHACHU KATIKA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA KIUTENDAJI..

    April 17, 2025
  • JIMBO LA BUYUNGU LABADILISHWA JINA NA KUITWA JIMBO LA KAKONKO.

    March 13, 2025
  • MHE.KAMAMBA AWAKUMBUSHA WATUMISHI KUWEKEZA KATIKA KILIMO NA BIASHARA PAMOJA NA KUJIENDELEZA KIELIMU.

    March 03, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkurugenzi afafanua mikakati ya kuendeleza zao la parachichi ikiwemo kugawa mashamba kwa wananchi.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Watendaji
  • Ukaguzi wa Miradi Kakonko
  • Lori jipya la Halmashauri laongeza kasi ya utekelezaji Miradi ikiwemo mradi wa Ufyatuaji tofali
  • TASAF kuibua ajira Kakonko
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko - FACEBOOK account
  • Habari motomoto za magazeti kila siku
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO- INSTAGRAM ACCOUNT
  • WANAFUNZI WILAYA YA KAKONKO WALIOPANGIWA SHULE KIDATO CHA KWANZA
  • MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WILAYA YA KAKONKO 2022

Viunganishi linganifu

  • Poralg
  • Public Service Management and Good governance
  • Necta
  • Tanzania portal
  • Kigoma Region Website
  • Tangazo la nafasi za kazi
  • Matokeo kidato cha nne 2018/2019 haya hapa
  • Balozi wa Norway akabidhi vifaa vya mifugo kakonko
  • Bunge la Tanzania
  • kakonko tv
  • Mapinduzi sekta ya elimu Kakonko
  • halmashauri ya wilaya ya kakonko - habari na mawasiliano
  • MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA 2 MWAKA 2022

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 3

    Simu: +255(028) 2988881

    Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881

    Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz

Mawasiliano

   

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma
    • Kanusho

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa