• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe |
Kakonko District Council
Kakonko District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Mawasiliano
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Usafishaji Na Mazingira
        • Elimu Msingi
        • Elimu ya Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maji
        • Maendeleo ya Jamii
        • Utumishi na Utawala
        • Fedha na Biashara
        • Maliasili, Ardhi na Mazingira
        • Kilimo cha Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Ujenzi na Zimamoto
      • Vitengo
        • Ugavi na Manunuzi
        • Tehama na Habari
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ufugaji Nyuki
        • Uchaguzi
        • Sheria
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Livestock
    • Fisheries
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Mipango na Usimamizi
      • Elimu Afya na Maji
      • Huduma za Kiuchumi Ujenzi na Mazingira
      • Udhibiti wa UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
        • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayo tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

Maendeleo ya Jamii

UTANGULIZI.

Idara ya Maendeleo ya Jamii ni idara mtambuka ambayo hufanya kazi zake kwa kushirikiana na idara zingine pamoja na mashirika binafsi yanayotekeleza shughuli zake hapa wilayani. Katika robo hii, idara imetekeleza shughuli mbalimbali zifuatazo;-

UTEKELEZAJI WA DHANA YA MAENDELEO YA JAMII

  • Kutembelea vikundi 13 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la Kutoa ushauri na elimu juu ya matumizi sahihi ya mikopo, utekelezaji / uendeshaji wa miradi yao na usimamizi wa vikundi. Vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na;-
  • Vijana harakati – Muhange,
  • Mwendo wa saa – Kiga,
  • Kikundi cha walemavu – Kiga,
  • Vijana Tuinuane – Muganza,
  • Tumaini walemavu CBR Kakonko,
  • Shauri moyo – Muhange
  • Tumaini –Nyamtukuza
  • Uweza – kabare
  • Peace and love – Kakonko
  • Kazi ni kazi – Kakonko
  • Kazi na Maendeleo – Itumbiko
  • Israfil- Kakonko
  • Ubhumwe – Gwarama
  • HALI YA UKOPESHAJI VIKUNDI

Katika robo hii halmashauri imetoa kiasi cha jumla ya mkopo wa Tsh.  47,819,770/= kwa vikundi vya wanawake 2, Vijana 3 na watu wenye ulemavu 1 ambapo Tsh. 20,000,000/= zinatokana na tengo la asilimia 10% ya mapato ya ndani na Tsh. 27,819,770/= zinatokana na marejesho ya mikopo kutoka vikundi vilivyokopeshwa.

Vikundi vilivyokopeshwa katika robo hii ni kama vifuatavyo;-

Na
Jina la kikundi
Aina ya kikundi
Mahali kilipo
Kiasi cha mkopo
1
Ubhumwe
Wanawake
Gwarama
14,819,770/=
2
Ukheri
Wanawake
Gwanumpu
7,000,000/=
3
Umoja wa vinyozi
Vijana
Kakonko
10,000,000/=
4
Vijana tuinuane
vijana
Muganza
6,000,000/=
5
Vijana Harakati
Vijana
Muhange
6,000,000/=
6
Umoja - Kiga
Watu wenye ulemavu
Kiga
4,000,000/=

Jumla kuu
47,819,770/=
  •  
  • HALI YA MAREJESHO YA MIKOPO

Hali ya marejesho ya mikopo kutoka kwa vikundi vilivyokopeshwa na halmashauri ni nzuri na katika robo hii kiasi cha fedha za mikopo kilichorejeshwa kutoka kwa vikundi vilivyokopeshwa ni TZs. 27,110,000/=Vikundi vilivyorejesha mikopo katika robo hii ni kama vifuatavyo;-

Na
Jina la kikundi
Aina ya kikundi
Mahali kilipo
Kiasi kilichorejeshwa

Mtaji ni jembe
Wanawake
Kinonko
1,600,000/=

Uhai
Wanawake
Kabare
1,800,000

Imani Lishe
Wanawake
Kasanda
2,795,000/=

Makini Lishe
Wanawake
Kasanda
1,200,000/=

Songambele ‘’A’’
Wanawake
Itumbiko
860,000/=

Tujikongoje
Wanawake
Bukiriro
500,000/=

Tunaweza
Wanawake
Churazo
2,800,000/=

Mafanikio
Wanawake
Kanyonza
4,000,000/=

Mkapa group
Vijana
Gwanumpu
2,500,000/=

Vijana Bodaboda
Vijana
Itumbiko
1,310,000/=

Vijana bivakule
Vijana
Nyabibuye
1,000,000/=

Bodaboda tunaweza
Vijana
Kanyonza
1,575,000/=

Faraja
Walemavu
Muganza
320,000/=

Ramadhan Adam
Walemavu
Kakonko
700,000/=

Walemavu
Walemavu
Itumbiko
2,900,000/=

Upendo
Walemavu
Kasuga
1,200,000/=

Sawaka
Walemavu
Kakonko
50,000/=

Jumla kuu
27,110,000/=

Aidha vikundi vingine vinaendelea kurejesha mikopo kwa mujibu wa mkataba.

  • UANDIKISHAJI NA URATIBU WA VIKUNDI NA NGOs

Katika kipindi cha robo hii, idara imesimamia na kuratibu zoezi la usajili wa vikundi vya wajasiriamali ambapo jumla ya vikundi 17 vimesajiliwa na kupatiwa vyeti vya utambuzi na vinaendelea na shughuli za uzalishaji mali.

Aidha katika robo hii, idara kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza shughuli zao hapa wilayani ambayo ni shirika la World vision Tanzania, IOM, KIWOHEDE na CRS imeweza kushiriki katika kutekeleza shughuli mbalimbali kama inavyoonesha hapa chini;-

  • Kutoa elimu ya kupinga ukatili kwa watoto ndani ya jamii na mashuleni ambapo kata 3 ambazo ni Mugunzu, Katanga na Kasanda na vijiji 9 na shule za msingi 11 zimefikiwa na takribani watu 6,513 wamefikiwa kati yao me ni 3,204 na Ke 3309.
  • Kutoa mafunzo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama wa wanawake na  Watoto (MTAKUWWA) katika ngazi Kata na Kijiji kutoka Kata za Kasanda, Katanga, Mugunzu, Gwarama, Nyabibuye, Kasuga, Rugenge, Muhange na Nyamtukuza .
  • Kutoa elimu ya afya uzazi na masuala ya jinsia kwa vikundi 3 ambavyo ni Kumekucha – Mugunzu, Chimbuko la Maendeleo – Ilabiro na Makini Lishe – Kasanda.
  • Kutoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto hususani usafirishaji haramu wa binadamu, unyanyasaji unaotendeka majumbani katika Kata za Kanyonza, Kakonko na Kiziguzigu ambapo elimu hii imewafikia jumla ya watu 1,342.

Kufanya bonanza juu ya afya ya uzazi kwa vijana katika Kata ya Muhange ambapo wanafunzi wa shule ya sekondari Ndalichako walifikiwa.

 

URATIBU WA SHEREHE NA MAADHIMISHO MBALIMBALI YA KITAIFA NA KIMATAIFA

Katika robo hii idara kwa kushirikiana na shirika la World Vision Tanzania imeweza kuratibu Maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Afrika ambayo Kiwilaya yalifanyika tarehe 16/06/2022 katika uwanja wa shule ya msingi Maendeleo iliyopo Kata ya Kakonko. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ambaye alimwakilisha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko. Viongozi wengine walihudhuria ni pamoja na;-

  • Wakuu wa idara na vitengo kutoka ofisi ya Mkurugenzi
  • Mwenyekiti wa CCM (w)
  • Mh. Diwani wa Kata ya Kakonko
  • Mh. Diwani wa viti maalum Kakonko
  • Mkuu wa polisi Kakonko
  • Dawati la jinsia polisi
  • Walimu na wanafunzi kutoka shule za msingi Itumbiko, Kakonko, Chelaburo na  Kakonko sekondari
  • Viongozi wa madhehebu ya dini
  • Mkuu wa taasisi ya madini Kakonko
  • Viongozi kutoka shirika la World Vision Kakonko na
  • Viongozi kutoka shirika la Wasaidizi wa Sheria Kakonko (WASHEKA)

Zifuatazo ni shughuli zilizofanyika wakati wa maadhimisho hayo;-

  • Maandamano ya watoto na wazazi waliokuwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga ukatili dhidi ya watoto,
  • Elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ilitolewa kupitia vikundi mbalimbali vya burudani,
  • Kupokea salamu mbalimbali kutoka kwa mashirika yasio ya kiserikali yaliyokuwepo
  • Kusikiliza risala iliyoandaliwa na  kusomwa na wanafunzi (watoto)
  • Kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli ya utoaji wa elimu mashuleni juu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto iliyofanyika wiki moja kabla ya maadhimisho hayo.
  • Kusikiliza Hotuba ya mgeni rasmi iliyokuwa na msisitizo kwa wazazi/ walezi na jamii kwa ujumla juu ya kutimiza wajibu wa kuwalea na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - WAKUSANYA MAPATO January 30, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. June 18, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA YA WAOMBAJI NAFASI YA UKUSANYAJI MAPATO WALIOITWA KWENYE USAILI January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA VITENDO - WAOMBAJI KAZI YA DEREVA II November 17, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WASISITIZWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.

    April 29, 2025
  • UANZISHWAJI WA MFUMO WA UTHIBITI UBORA WA SHULE WATAJWA KUWA CHACHU KATIKA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA KIUTENDAJI..

    April 17, 2025
  • JIMBO LA BUYUNGU LABADILISHWA JINA NA KUITWA JIMBO LA KAKONKO.

    March 13, 2025
  • MHE.KAMAMBA AWAKUMBUSHA WATUMISHI KUWEKEZA KATIKA KILIMO NA BIASHARA PAMOJA NA KUJIENDELEZA KIELIMU.

    March 03, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkurugenzi afafanua mikakati ya kuendeleza zao la parachichi ikiwemo kugawa mashamba kwa wananchi.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tangazo la Nafasi za Kazi za Watendaji
  • Ukaguzi wa Miradi Kakonko
  • Lori jipya la Halmashauri laongeza kasi ya utekelezaji Miradi ikiwemo mradi wa Ufyatuaji tofali
  • TASAF kuibua ajira Kakonko
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko - FACEBOOK account
  • Habari motomoto za magazeti kila siku
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO- INSTAGRAM ACCOUNT
  • WANAFUNZI WILAYA YA KAKONKO WALIOPANGIWA SHULE KIDATO CHA KWANZA
  • MATOKEO YA WANAFUNZI WA DARASA LA NNE WILAYA YA KAKONKO 2022

Viunganishi linganifu

  • Poralg
  • Public Service Management and Good governance
  • Necta
  • Tanzania portal
  • Kigoma Region Website
  • Tangazo la nafasi za kazi
  • Matokeo kidato cha nne 2018/2019 haya hapa
  • Balozi wa Norway akabidhi vifaa vya mifugo kakonko
  • Bunge la Tanzania
  • kakonko tv
  • Mapinduzi sekta ya elimu Kakonko
  • halmashauri ya wilaya ya kakonko - habari na mawasiliano
  • MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA 2 MWAKA 2022

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 3

    Simu: +255(028) 2988881

    Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881

    Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz

Mawasiliano

   

Waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma
    • Kanusho

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa