TAARIFA YA KAZI ZA KITENGO CHA SHERIA KATIKA ROBO YA PILI MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Kitengo cha Sheria ni kitengo mtambuka ambacho kinafanya kazi zake kwa kushirikiana na Idara na Vitengo vyote vya Halmashauri katika ujenzi wa miradi ya Maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Pia Wanasheria wa Halmashauri ndio washauri Wakuu wa Mkuu waTaasisi na Halmashauri kwa ujumla wake kwa masuala yote yanayohusiana na mambo ya kisheria na mikataba ya aina tofauti ya Hallmashauri. Hali kadhalika wanasheria wa halmashauri ndio wawakilishi wakuu katika vyombo vya utoaji haki endapo Halmashauri itashitaki au kushtakiwa.
Katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2016/2017 inayoanzia mwezi wa Oktoba mpaka Desemba wataalam wa kitengo cha sheria pamoja na shughuli za kawaida za kiofisi lakini pia imetekeleza mambo yafuatayo:-
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ilitunga sheria ndogo na kanuni za kudumu za Halmashauri na kuziwasilisha Wizarani kwa ajili ya kusainiwa na kuidhinishwa na aliyekuwa Waziri mwenye dhamana kwa kipindi hicho Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda mnamo mwezi Septemba 2015.
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na kuanza kazi yalitolewa maagizo mapya kuwa mwenye dhamana ya kusaini sheria ndogo hizo ni Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli na mabadiliko yalifanyika na kupelekwa kwa ajili ya kusainiwa kwa kutumia barua ya tarehe 15/11/2016 yenye kumb. Na.cab.137/133/01/41.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilitoa maelekezo mapya baada ya kupata barua ya Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Tamisemi ya tarehe 23/11/2016 yenye kumb na.ccc 132/394/01/45 kuwa mwenye dhamana ya kusaini ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa GEORGE SIMBACHAWENE (mb) mabadiliko hayo yameshafanyika na kutumwa tena tarehe 05/12/2016 kwa barua yenye kumb na.HW/KNK/J.10/2. Sasa hivi tuna subiri sheria zisainiwe kumalizia mchakato mzima wa uidhinishaji wa sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jimbo la buyungu katika halmashauri ya wilaya ya Kakonko kulikuwa na kesi ya uchaguzi namba 1/2015 baada ya mgombea wa ccm aliyeshindwa katika nafasi ya ubunge kutoridhishwa na matokeo na kuamua kufungua kesi hiyo katika mahakama kuu kanda ya tabora dhidi ya mwanasheria mkuu wa serrikali,msimamizi wa uchaguzi jimbo la buyunguna mgombea wa chadema aliyetangazwa kuwa mbunge.mheshimiwa jaji wa mahakama iliyosikilia kesi hiyo alitoa hukumu tarehe 08/07/2016na kutupilia mbali malalamiko ya mgombea aliyefungua kesi hiyo na matokeo kubaki kama yalivyokuwa yametangazwa na msimami wa uchaguzi.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeleta kanda ya Tabora imeleta imeleta taarifa kuwa mgombea aliyeshindwa katika katika kesi namba 1/2015 hakuridhishwa na maamuzi ya Mahakama kuu kanda ya Tabora na kuamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu husika.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ikiwa ni msimamizi wa uchaguzi husika na mdaiwa wa pili mpaka sasa bado haijapokea wito (summons) kutoka kwa muomba rufaa au mahakama ya rufaa, kutokana na historia ya kesi hii katika mahakama kuu ya Tabora, Halmashauri imeona ni vyema kuwasilisilisha taarifa hizi kama zilivyopokelewa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi tukisubiri kupata wito ( summons).
Pamoja na maelezo ya hapo juu lakini pia taarifa hiyo imepokelewa tume ya uchaguzi mapema ili iweze kuandaa gharama na pesa zote za uendeshaji wa suala hili la kesi ya Rufaa mara itakapotokea. Taarifa hii imepelekwa kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa barua yenye kumb. Na. hw/knk/j/3 pia mawasiliano ya karibu yanaendelea kufanyika na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujua maendeleo ya shauri hili kwa kipindi hiki ambacho Ofisi ya Mkurugenzi bado haijapata wito (summons).
Halmashauri imeweza kupata nakala ya hukumu ya kesi ya uchaguzi namba 1/2015 iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda Tabora tarehe 08/07/2016. Nakala hiyo ya hukumu imetunzwa kwa ajili ya kumbukumbu za Halmshauri baada ya kuombwa katika mahakama kwa kutumia barua ya tarehe 05/11/2015ya kumb. Na. HW/KNK/J.103.
Kazi hizi zimepangwa kuanza kufanyika na wanasheria wameshatayarisha nyaraka zote za kutendea kazi husika. Wanasheria watapita katika kata zote 13 kukamilisha kazi hii kama ilivyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa