Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi.Elizabeth Jacobsen amezindua vifaa vya mifugo kwa ajili ya kuhifadhi chanjo, kuisafirisha na kutoa mafunzo katika hafla iliyofanyika siku ya jumatatu Januari 23, 2019 katika ukumbi wa mikutano Wilayani Kakonko alipoanya ziara ya kikazi.
Balozi Jacobsen amekabidhi Jokofu moja, vibeba chanjo, chanjo dozi 70,000 na vitabu vya rejea ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa utekelezaji wa shughuli za mifugo Wilayani kakonko kupitia program inayoitwa Kigoma Joint Program ambayo inatekelezwa katika kata tatu Wilayani Kakonko ambazo ni Kakonko, Nyabibuye na Nyamtukuza.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa Wilaya akiwemo Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri Balozi Elisabeth alisisitiza vifaa hivyo vifanye kazi iliyokusudiwa ili kupunguza magonjwa ya mifugo na kuinua kipato cha wafugaji.
Mafunzo kwa vitendo yatafanyika kwa maafisa ugani Januari 28 juu ya mbinu bora za ufugaji wa kuku na mifugo mingine, uthibiti wa magonjwa na uimarishaji wa kutoa taarifa za magonjwa.
Serikali ya Norway inafadhili program ya Kigoma Joint Program kupitia shirika la la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) ambalo linaratibu utekelezaji wa mradi katika sekta ya kilimo na mifugo pamoja na Wizara ya mifugo kwa kuweka mikakati thabiti ya kuwasaidia wafugaji wadogo.
Afisa mifugo wa Wilaya ya Kakonko bwana Revelian Rushehela ameeleza kuwa Wilaya ya Kakonko ina jumla ya wafugaji 3186 ambapo kuna jumla ya ng’ombe wa kienyeji 25,518 na ng’ombe wa kisasa 53, kuku76,974 na kuna eneo la hekta 45,226.23 la kufugia linalopatikana katika Vijiji 44 vilivyopo Wilayani Kakonko.
Akitoa takwimu Afisa mifugo bwana Rushehela ameeleza kuwa, ‘Shirika la FAO limetoa mafunzo kwa vikundi 45 vyenye wakulima 998 juu ya mbinu bora za ufugaji na teknolojia pamoja na mbinu za kilimo kupitia mashamba darasa na kupatiwa pembejeo ikiwemo mbolea za kupandia 776, nambolea za kukuzia kilo 4330, mbegu za mahindi kilo 858, maharage 212 na Muhogo pingili 21,000.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa