Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko Maulid Mtulia kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko amefungua bonanza la Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko (wenyeji), watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Watumishi wa Wilaya ya Muleba, leo Jumamosi 26 Julai, 2025 katika viwanja vya shule ya sekondari Kakonko.
Akifungua bonanza hilo, mgeni rasmi amewataka Watumishi kucheza kwa kuzingatia sheria za uwanjani ili mchezo kuwa wa ushindaji na haki na kuepuka mchezo wa kutumia nguvu na kuumizana kwani lengo la bonanza hilo ni kuboresha afya za watumishi, kujenga urafiki na kuboresha ushirikiano wa Halmashauri zilizoshiriki katika michezo hiyo.
Muandaaji wa bonanza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Ndaki Stephano Mhuli amewakaribisha wachezaji wote na kuwaahidi kufurahia michezo yote iliyoandaliwa ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa kikapu na michezo mingine kama kuvuta kamba na mchezo wa riadha ya mbio ndefu na fupi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa