Division inasimamia ujenzi unaoendelea wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, ujenzi wa Stendi kuu ya mabasi Kakonko, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko, ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakiyobe, ujenzi wa Jengo la Wazazi Gwarama, ujenzi wa Zahanati ya Njoomlole, ujenzi wa Zahanati ya Kihomoka. Ukarabati wa Zahanati ya Rumashi na ukamilishaji wa Zahanati za Luhuru na Rusenga. Kusimamia ujenzi wa vyoo katika zahanati za Kasongati, Nyamtukuza, Kiga, Bukiliro, Kabingo na Rumashi. Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa, maabara, maktaba, jengo la utawala, jengo la tehama na vyoo vya wanafunzi Shule ya Sekondari ya Katanga kupitia mpango wa SEQUIP. Ukamilishaji wa maabara 5 Elimu Sekondari (Mugunzu, Rugenge, Nyamtukuza, Gwanumpu na Muhange), kusimamia ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa Idara. Kusimamia karakana ya kufyatua tofali iliyopo Shule ya wasichana Kakonko kata ya Kanyonza, kusimamia mitambo na magari ya Halmashauri.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA KIPINDI CHA APRILI – JUNI, 2022
Na. |
JINA LA MRADI |
LENGO |
UTEKELEZAJI |
MAELEZO |
CHANZO CHA FEDHA |
% YA UTEKELEZAJI |
||
1. |
Kusimamia ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
|
Kuimarisha na kuboresha mazingira ya kazi.
|
Ujenzi umegawanywa katika majengo 4, majengo 2 ya mwanzo yanaendelea na kazi za umaliziaji isipokuwa eneo la mapokezi wanakamilisha bati, jengo 3 limekamilika kuweka bati, papi za dari, grili, fremu za milango na lipu; lingine la mwisho linaendelea kukamilishwa bati, grili za madirisha, fremu za milango na lipu. Kazi ya ujenzi inafanyika kwa njia ya Force Account.
|
Mradi unaendelea vizuri
|
Serikali kuu
|
68% |
||
2. |
Kusimamia ujenzi wa Stendi kuu ya mabasi Kakonko
|
Kutoa huduma na kuongeza mapato ya Halmashauri
|
Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri.
|
Kazi hii inatekelezwa na Mkandarasi mjenzi SUGWA CONSTRUCTION LTD JV CHIGANDA CONSTRUCTION LTD na Mkandarasi mshauri TBA (Tanzania Building Agency).
|
Serikali kuu |
67% |
||
3. |
Kusimamia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi ya ujenzi wa jengo la wazazi, wagonjwa wa nje, Maabara Mionzi, Stoo ya dawa, jengo la utawala na jengo la kufulia zipo hatua ya umaliziaji. Kazi ya jengo la EMD limekamilika boma na bati baadhi ya maeneo. Jengo la kuishi waganga familia tatu limekamilika hatua ya bati.
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
Serikali kuu |
89% |
||
4. |
Kusimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakiyobe
|
Kuimarisha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi ya ujenzi wa maabara imepauliwa na wanaendelea kuweka grili za madirisha na fremu za milango na Kazi ya ujenzi wa OPD ipo hatua ya kusuka kenchi.
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
Serikali kuu |
58% |
||
5. |
Kusimamia ujenzi wa Jengo la Wazazi Gwarama
|
Kuimarisha na kuboresha huduma za afya.
|
Kazi ya ujenzi ipo katika hatua ya ukamilishaji wa dari, kufunga milango na skimingi.
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
UNFPA |
87% |
||
6. |
Kusimamia ujenzi wa Zahanati ya Njoomlole
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi ya ujenzi ipo katika hatua ya kufunga milango, kuweka dari na marumaru.
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
Mapato ya ndani |
89% |
||
7. |
Kusimamia ujenzi wa Zahanati ya Kihomoka
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi ya ujenzi ipo katika hatua ya kufunga milango, kuweka dari na marumaru..
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
Mapato ya ndani |
92% |
||
8. |
Ukarabati wa Zahanati ya Rumashi
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi ipo hatua ya ukarabati
|
Kazi imepangwa kutekelezwa kwa njia ya force account
|
Serikali kuu |
52% |
||
9. |
Ukamilishaji wa Zahanati ya Luhuru
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi zipo hatua ya ukamilishaji wa boma
|
Kazi imepangwa kutekelezwa kwa njia ya force account
|
Serikali kuu |
35% |
||
10. |
Ukamilishaji wa Zahanati ya Rusenga
|
Kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa jamii.
|
Kazi zipo hatua ya ukamilishaji wa boma
|
Kazi imepangwa kutekelezwa kwa njia ya force account
|
Serikali kuu |
37% |
||
11. |
Kusimamia ujenzi wa vyoo katika zahanati za Kasongati, Nyamtukuza, Kiga, Bukiliro, Kabingo na Rumashi
|
Kuboresha mazingira ya kazi.
|
Kazi zipo katika hatua za ukamilishaji wa majengo na mashimo ya vyoo
|
Kazi hii inatekelezwa kwa Force Account
|
Ufadhili wa World Bank |
80% |
||
12. |
Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa, maabara, maktaba, jengo la utawala, jengo la tehama na vyoo vya wanafunzi Shule ya Sekondari ya Katanga kupitia mpango wa SEQUIP
|
Kusogeza karibu huduma ya upatikanaji elimu kwa jamii.
|
Kazi zipo hatua; Madarasa manne yamekamilika boma; madarasa manne, maabara tatu, jengo la Tehama, jengo la utawala na maktaba wima wa lenta; choo matundu kumi yamekamilika msingi na mashimo; choo matundu kumi wamechimba msingi wa boma na ujenzi wa mashimo.
|
Kazi inatekelezwa kwa njia ya Force Account
|
Serikali kuu |
43% |
||
13. |
Ukamilishaji wa maabara 5 Elimu Sekondari (Mugunzu, Rugenge, Nyamtukuza, Gwanumpu na Muhange)
|
Kuboresha mazingira ya upatikanaji elimu
|
Kazi za ukarabati zinaendelea katika hatua mbalimbali
|
Kazi inatekelezwa kwa njia ya Force Account
|
Serikali kuu |
67% |
||
14. |
Kusimamia ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa Idara
|
Kuboresha maisha ya watumishi
|
Kazi ya nyumba moja ipo hatua ya ukamilishaji wa boma baada ya lenta na nyingine ipo hatua ya ujenzi wa msingi
|
Kazi inatekelezwa kwa njia ya Force Account
|
Serikali kuu |
41% |
||
15. |
Kusimamia ujenzi wa miundombinu wa vyumba vya madarasa, vyoo vya wanafunzi na waalimu na ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19.
|
Kuimarisha na kuboresha mazingira ya kutolea elimu.
|
Kazi za ujenzi wa madarasa 46 vyoo, ofisi za waalimu na bweni la wenye mahitaji maalum zipo katika muda wa uangalizi
|
Kazi hii ilitekelezwa kwa Force Account
|
Serikali kuu |
100% |
||
16. |
Kusimamia karakana ya kufyatua tofali iliyopo Shule ya wasichana Kakonko kata ya Kanyonza
|
Kuwa na uhakika wa upatikanaji wa vifaa bora vya ujenzi na kuongeza kipato kwa Haimashauri
|
Kazi ya ufyatuaji matofali inaendelea vizuri
|
Kazi inatekelezwa na vibarua na fundi wa mkataba chini ya usimamizi wa Afisa mtendaji kata ya Kanyonza na Technician kutoka ofisi ya Mhandisi
|
Mkurugenzi |
100% |
||
17. |
Kusimamia mitambo na magari ya Halmashauri
|
Kuboresha miundombinu ya utendaji kazi za Halmashauri
|
Kukagua na kutathmini uharibifu na matengenezo yanayo hitajika katika gari au mtambo
|
Kazi hutekelezwa kwa kufanya tathmini kupitia mafundi wa nje
|
Mkurugenzi |
100% |
||
|
|
|
|
|
|
|
||
|
UFUATILIAJI NA KUANDAA TATHMINI YA UKARABATI WA MAJENGO YA SERIKALI NA MIUNDOMBINU YAKE |
|
||||||
|
Kuandaa tathmini ya ujenzi, uboreshaji na ukarabati wa majengo na miundombinu ya Halmashauri
|
Kuwa na dira kuhusu gharama za ujenzi, uboreshaji na ukarabati
|
Kazi za tathmini za ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Shule za Msingi, Sekondari, afya na majengo mbalimbali ya serikali.
|
Kazi ya tathmini hufanyika baada ya bajeti kutengwa na Mkurugenzi
|
- |
100% |
||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa