Idara ya maji inalo jukumu la kuhakikisha Wilaya ya Kakonko inapata maji kwa kufanya matenegenezo kwa mifumo ya maji iliyopo, kuongeza mfumo wa maji na kuandaa maadiko kwa ajili ya kupata miradi mipya ya maji.
HALI YA HUDUMA YA MAJI KAKONKO MJINI
Mji wa Kakonko katika kipindi hiki umeendelea kupata majisafi na salama kutoka katika vyanzo vyake ambavyo ni visima virefu 02, Visima vifupi 03 pamoja na Maji ya kusukumwa kwa nguvu za umeme kutoka katika chanzo cha Maji kisima kirefu cha Mbizi.
Maji ya kusukumwa na pampu ya nguvu za umeme yameendelea kupatikana katika maeneo ya Mji wa Kakonko kwa wateja wa majumbani(private connection) ambao kwa sasa idadi imefikia wateja 105 , Vituo vya Kuuzia Maji 11 Pamoja na kituo cha afya cha Muganza. Mradi huu una wezo wa kuzalisha lita za ujazo 160,000 kwa siku sawa na mita za ujazo 160. Kiasi hiki cha Maji kinatosheleza mahitaji ya Maji kwa watu 3570 kwa siku.
HALI YA HUDUMA VIJIJINI
Wananchi wanaendelea kupata huduma ya Maji kutoka katika vyanzo mbalimbali tulivyonavyo kama vile visima virefu na vifupi, Chemichemi, Mabwawa mito na maji kuvunwa kwa mvua.
Aidha wananchi wa vijiji vya Kiga, Kinyinya/Churazo, Rumashi, Kabare, Gwarama, Nyabibuye, Bukirilo na Rusenga wanaendelea kupata huduma za Maji kutoka katika skimu zao za Maji ya bomba chini ya uongozi wa Kamati na jumuiya za Maji.
KAZI ZILIZOFANYIKA
Katika kipindi cha robo ya pili kazi zifuatazo zimefanyika
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa