MAJUKUMU YA IDARA YA FEDHA NA BIASHARA
1. Kuthibiti na kusimamia matumizi bora ya fedha katika Halmashauri
2. Kukusanya na kusimamia mapato kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya serikali.
3. Kutayarisha hesabu za mwaka (annual final accounts)
4. Kuandaa malipo ya mishahara kwa wakati
5. Kuandaa na kuwasilisha orodha ya hati za malipo hazina
6. Kutayarisha bajeti ya Idara
8. Kutoa huduma za kifedha na hifadhi ya vitabu vya kumbukumbu za fedha.
9. Kuandaa kwa wakati taarifa za kifedha za malipo ya pensheni kwa watumishi waliostaafu.
MAPATO
3.1 Mapato ya Halmashauri
Vyanzo vikuu vya mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni kutoka Serikali kuu, Fedha za wadau wa maendeleo, mapato ya ndani na wahisani mbalimbali.
Halmashauri iliibua miradi miwili ya kimkakati ambayo ni soko la mpakani Muhange na Stendi ya mabasi Kakonko ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Mradi wa soko umekamilika na mradi wa stendi unaendelea kutekelezwa.
Mwenendo wa makusanyo ya mapato ya ndani kupitia vyanzo mbalimbali pamoja na mapokezi ya fedha za ruzuku toka Serikali Kuu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 202012022 kwa wastani ni ya kuridhisha kama inavyoonesha kwenye muhtasari hapa chini.
Mwaka
|
Bajeti Kiasi TZS
|
Makusanyo
|
Asilimia
|
2019/2020
|
697,681,000 |
693,455,000 |
99 |
2020/2021
|
1,031,933,256 |
842,746,697 |
82 |
2021/2022
|
1,038,636,000.00 |
1,069,058,023.00 |
103 |
Chanzo: Taarifa ya fedha
3.2 Udhibiti wa matumizi ya Fedha za Serikali
Halmashauri imeendelea kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni katika matumizi ya fedha za Serikali. Kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kipindi cha miaka mitatu (3) iliyopita Halmashauri imeweza kupata hati tofauti kama ifuatavyo:
Mwaka
|
Aina ya Hati
|
2019/2020
|
Hati ya kuridhisha
|
2020/2021
|
Hati yenye mashaka
|
2021/2022
|
Ukaguzi unaendelea
|
Chanzo; Ripoti ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu WA Hesabu za Serikali
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko inayo mikakati mbalimbali ya kuendelea kupata hati safi, ikiwa ni pamoja na:
Ukamilishaji wa utekelezaji wa shughuli na miradi ya maendeleo unaokwenda sambamba na upokeaji wa fedha na matumizi sahihi
Uandaaji wa hesabu kwa kufuata taratibu na kanuni za fedha.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa