Kitengo cha TEHAMA kinatoa huduma wezeshi katika matumizi ya Teknolojia ya Kompyuta, Mifumo ya Mawasiliano na masuara yote yanayohusu Habari na Uhusiano ndani na nje ya Halmashauri.
Kwa kufanya hivyo kitengo kinatoa fursa nyingi kwa Idara na Vitengo vya Halmashauri kufanya majukumu yake vizuri hasa katika masuala yote yanayohitaji matumizi ya mifumo ya mawasiliano ya Kompyuta, Habari na Teknolojia kwa kuwezesha mbinu za kisasa za kufanyaa kazi. Hii hufanyika kwa kuzingatia mahitaji ya watumiaji wa mifumo ya mawasiliano, maoni ya wadau na mahitaji ya taasisi ili kufikia Malengo ya jumla ya Halmashauri.
Tabia mbalimbali za watendakazi katika taasisi hukijengea kitengo hatua za mwanzo katika kubuni mbinu mpya na za kisasa za kufanyia kazi, kila mchakato unaweka mahitaji mbalimbali juu ya msaada wa tehama. Kutokana na hali ya sasa ya uhitaji mkubwa wa matumizi ya tekinolojia, kitengo cha TEHAMA kimekuwa msingi mkubwa wa mafanikio katika taasisi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa