1.0 UTANGULIZI
Wilaya ya Kakonko ina jumla ya Tarafa tatu (3) ambazo ni Nyaronga, Kasanda na Kakonko ambazo zina jumla ya Kata kumi na tatu (13), vijiji 44 na Vitongoji 355.
Utawala bora na uwajibikaji ni mojawapo ya maeneo muhimu yanayopewa kipaumbele na Serikali kupitia Ilani ya uchaugzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, Dira ya maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Maendeleo Endelevu (SDG) na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/2022 – 2025/2026).
Kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi hutatuliwa kupitia Ofisi za Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji, Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Kata, Mkurugenzi Mtendaji, Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Aidha Halmashauri ina dawati maalumu linaloshughulikia malalamiko mbalimbali yanayoletwa dhidi ya Halmashauri au Watendaji wake na kufanya ufuatiliaji kuhakikisha kila lalamiko la mwananchi linatatuliwa au kuelekezwa kwenye mamlaka inayohusika. Baadhi ya malalamiko ama kero ni kama Migogoro ya Ardhi, Migogoro ya unyanyasaji wa Kijinsia na mingine. Kero nyingi hutatuliwa kupitia dawati la malalamiko kwa kuwasiliana ama kushirikiana na wahusika wa maeneo au idara husika. Pia masanduku ya maoni yamewekwa katika Ofisi ili kubaini kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi mapema.
2.1 Hali ya Watumishi katika Halmashauri
Hali ya watumishi katika miaka miwili iliyopita hadi sasa ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Kwa sasa Halmashauri inauhitaji wa watumishi 1958 sawa na 50% kama ifuatavyo;
Mwaka |
Mahitaji |
Waliopo |
Upungufu |
Upungufu % |
2020/2021 |
1958 |
951 |
1,007 |
49% |
2021/2022 |
1958 |
988 |
970 |
50% |
Chanzo: Idara ya Utawala na Utumishi
2.2 Watumishi wapya walioajiriwa katika kipindi cha miaka miwili .
Katika Kipindi cha miaka 2 Halmashauri imefanikiwa kupata ajira mpya kwa Kada tofauti tofauti kama mchanganuo ufuatao unavyoonesha:
Mwaka |
Idadi ya Watumishi walioajiriwa |
Idara ya Utawala |
Idara ya Afya |
Idara ya Elimu Msingi |
Idara ya Elimu Sekondari |
Idara ya Ujenzi |
2020/2021 |
34 |
1 |
0 |
17 |
16 |
0 |
2021/2022 |
49 |
0 |
23 |
17 |
8 |
1 |
Halmashauri imekuwa ikitenga katika bajeti kwa ajili ya ajira mpya kwa kila mwaka wa fedha ili kuhakikisha Halmashauri iweze kupata watumishi wa kutosha ili kuweza kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
2.3 Ujenzi wa nyumba za Watumishi
Halmashauri imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji na inaendelea na ujenzi wa nyumba 2 za Wakuu wa Idara ambapo hadi kufikia mwezi Septemba 2022 ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa idara umefikia hatua ya umaliziaji kwa ujenzi wa nyumba ya kwanza (moja) na hatua ya msingi kwa nyumba ya pili.
2.4 Ujenzi wa Majengo ya Utawala
Katika kipindi cha 2019/2020 hadi 2021/2022 Halmashauri imeendelea na ujenzi wa jengo la utawala awamu ya III ambapo hadi kufikia Sept 2022 ujenzi upo hatua za mwisho za umaliziaji.
2.5 Mkakati wa kuwabakiza watumishi
Halmashauri ameandaa mkakati wa kuwabakiza watumishi ili kupunguza idadi ya watumishi wanaohama kwa kufanya yafuatayo:
2.5.1 Kutoa motisha kwa watumishi wapya na waliopo.
Kuwepo kwa malazi, chakula na viburudisho wakati wa mapokezi.
Kuwepo kwa mapokezi na usafiri kutoka stendi kuu ya wilaya ya Kakonko.
Uwepo wa nyaraka mbalimbali zinazohusiana na ajira.
Watumishi wapya Kupewa vifaa vya kuanzia kazi kama vile magodoro na mitungi midogo ya gesi.
Matumizi ya lugha nzuri kwa watumishi wapya wakati wa mapokezi.
Fedha za kujikimu kwa watumishi wapya itolewe kwa wakati.
Masuala yahusuyo mishahara yashughulikiwe kwa wakati.
Kutengeneza mazingira rafiki ya upatikanaji wa viwanja vya makazi kwa kuwapunguzia kuanzia aslimia 20-30; iliwahamasike kujenga nyumba zao na hatimaye wayafanye makazi yao ya Kakonko kuwa ya kudumu.
Kuwepo kwa usafiri wa kuwapeleka watumishi wapya kwenye vituo vyao vya kazi.
Mwajiri kutoa lori kwa watumishi wanaojenga ili wao wagharimie mafuta wakati wa kusomba vifaa vyao vya ujenzi.
Watumishi waliopo.
Kutolewa kwa mikopo nafuu.
Kutengeneza mazingira rafiki kati ya watumishi na jamii inayowazunguka kwa kuwepo kwa kikosi kazi maalum kitakachozunguka wilaya nzima.
Kuboresha utoaji wa huduma/utoaji wa huduma kwa wakati.
Kuwepo kwa mabonanza mbalimbali ya michezo ili kuondoa ombwe lililopo kati ya watumishi wa makao makuu na wale waliopo kwenye vituo vya kutolea huduma.
Kuboresha miundo mbinu katika vituo vya kutolea huduma mfano nyumba za kuishi.
Kutengeneza mazingira rafiki ya upatikanaji wa viwanja vya makazi.
Kuwatambua watumishi wanaofanya vizuri katika kazi zao na kuwapa motisha mbalimbali kama vile kupelekwa sehemu za utalii na kupewa madaraka.
Mkurugenzi aandae usafiri wa kwenda na kurudi makao makuu ya Halmashauri kwaajili ya watumishi wa makao makuu.
Mwajiri alipe kwa wakati stahiki za uhamisho kwa watumishi wanaohama vituo ndani ya Halmashauri na wale wanaohamia kutoka nje ya Halmashauri.
Mwajiri kuwapunguzia watumishi bei za viwanja ili wahamasike kujenga nyumba zao na hatimaye wayafanye makazi yao ya Kakonko kuwa ya kudumu.
Mwajiri kutoa lori kwa watumishi wanaojenga ili wao wagharimie mafuta wakati wakusomba vifaa vyao vya ujenzi.
Mwajiri kujenga hosteli/Nyumba ya kulala wageni ya biashara kwaajili ya kuiingizia Halmashauri mapato ambapo pia itatumika kuwapokelea watumishi wapya.
Halmashauri kutengeneza maeneo mbalimbali ya starehe yatakayowafanya watumishi na familia zao kuwanasehemu za kupumuzika na kufurahi kama ilivyo miji mingine.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa