Kamati ya Maadili ina wajibu wa kuhakikisha waheshimiwa mwadiwani wanafuata maadili na kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Kwa mujibu wa Kanuni za sheria ya Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya) (Maadili ya Madiwani za Mwaka 2000)
sehemu ya (9) inahusu uvunjaji wa maadili na kifungu cha 32.
Malalamiko kuhusu uvunjaji wa kanuni za maadili ya madiwani yanaweza kutolewa na mmojawapo kati ya watu wafuatao:
1. Mtu yeyote ambaye ameathiriwa au anaelekea kuathiriwa na kitendo au maamuzi yaliyofanywa na diwani
2. Diwani
3. Mtumishi wa halmashauri
4. Kamati ya maadili kwa kuamua yenye
Hata hivyo mtu yeyote mwingine anaweza kutoa taarifa kuhusu uvunjaji wa Kanuni za Maadili kwa Kamati ya Maadili ili afikiriwe na kutokana na taarifa hiyo kamati inaweza kutayarisha malalamiko kama inafaa kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 33 utaratibu wa kuwasilisha malalamikoni kama ifuatavyo;
i) Lalamiko litakalowasilishwa kwenye kamati ya maadili litatolewa kimaandishi katika fomu inyohusika itakayotolewa na kamati ambayo itakuwa na taarifa zilizotajwa katika kanuni ndogo na kusainiwa na mlalamikaji
ii). Pale ambapo mlalamikaji hawezi kuandika, mlalamikaji atatoa maelezo yake kuhusu uvunjaji wa maadili ambayo yatachukuliwa au kuandikwa na katibu na hatimaye mlalamikaji ataweka alama ya dole gumba mwisho wa maelezo yake.
iii). Aidha lalamiko liwe na jina. Hata hivyo kamati haitalazimika kutaja jina la mlalamikaji
Kamati inapaswa kupata habari za uhakika
Kwa mujibu wa kifungu cha 34 kamati inaweza kushughulikia malalamiko kama ifuatavyo;
Kamati itajiwekea utaratibu wa kusikiliza malalamiko ambao unaweza kuwa pamoja na kuita mashahidi ili kuthibitisha tuhuma au kumwita diwani aliyetuhumiwa ili ajitetee.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa