TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA PILI KWA MWAKA 2016/17 (JULAI, 2016 HADI DISEMBA, 2016)
UTANGULIZI
Katika mwaka wa fedha 2016/17, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko iliidhinishiwa jumla ya Tsh. 8,252,991,478 /= (Tsh 5,353,073,000/=toka Serikali Kuu, Tsh 2,641,717,074/= toka kwa wahisani na Tsh 258,201,404 toka mapato ya ndani ya Halmashauri 60%) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. Wakati huo, Halmashauri ilikuwa imebakiwa na salio ishia toka mwaka 2015/16 ya kiasi cha TSh. 1,614,009,116/= zikiwa zipo katika akaunti za Halmashauri. Hii inafanya kuwepo nafasi ya kutumia jumla ya TSh. 9,867,000,594/= kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
2.0. UTEKELEZAJI WA MIRADI (JULAI, 2016 – DESEMBA, 2016)
2.1. MIRADI VIPORO KWA MWAKA 2015/2016
Kwa mwaka wa Fedha 2015/2016, Halmashauri ilibakiwa na Fedha Tsh 1,614,009,116/= katika akaunti zilizopo ngazi ya Wilaya. Hadi mwishoni mwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2016/2017 Tsh. 815,460,023/= zimetumika kutekeleza miradi viporo sawa na 50.52% ya bakaa.
Fedha nyingi zilizokuwa hazijatumika zikiwemo fedha za ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri, ujenzi wa wadi na Maabara kituo cha afya Nyanzige, mpango wa maendeleo ya elimu sekondari awamu ya pili (SEDP II), programu ya EQUIP zimeanza kutumika na utelekezaji wake unaendelea kwa kasi isipokuwa uendelezaji wa skimu ya Ruhwiti ambayo fedha zake hazijaanza kutumika kutokana na kuchelewa kupatikana kwa Mkandarasi anayekidhi vigezo, taratibu za kumpata mkandarasi mwenye sifa zipo hatua ya mwisho kukamilishwa.
2.2. MIRADI YA MWAKA 2016/17
Hadi kufikia tarehe 31.12.2016 kwa robo ya pili, Halmashauri ilikuwa imepokea Tsh 2,228,177,416/= kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017, na kutumia Tsh 977,469,460/= sawa 43.87% ya fedha zilizopokelewa. Pia Halmashauri imepokea fedha nje ya bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka 2016/2017 kiasi cha Tsh 260,173,468/= zikiwa ni fedha za mfuko wa barabara (rollover fund) kwa ajili ya kulipa kazi za barabara zilizotendwa 2015/2016 ambazo fedha yake ilikuja kidogo na Tsh 147,193,468/= sawa 56.58% zimekwishatumika kwa kulipa Wakandarasi waliomaliza kazi kwa mujibu wa mkataba.
2.3 CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI
Masharti ya fedha za EQUIP ambayo shughuli zake haziwezi kufanyika mpaka ziruhusiwe na EQUIP – Makao Makuu.
Baadhi ya wakandarasi kuwa na uwezo mdogo hali inayopelekea kuchelewa kukamilika kwa kazi kwa wakati.
Halmashauri inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ikiwemo kuvunja mikataba ya wakandarasi wanaosuasua kumaliza kazi kwa wakati bila sababu za msingi. Halmashauri pia inaendelea kuwasiliana na EQUIP – Makao Makuu ili waharakishe utekelezaji wa shughuli zilizopangwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa