Na Cosmas Makalla - Kakonko
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanzisha mifumo miwili ya kidijitali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wake, hususan wastaafu, kwa kurahisisha mchakato wa kuomba na kupata mafao.
Mifumo hiyo miwili PSSSF Portal na PSSSF Kiganjani inamwezesha mwanachama kuwasilisha maombi ya mafao, kuangalia michango yake, kuongeza wategemezi, na kupata huduma nyingine kwa njia ya mtandao au kupitia simu ya mkononi.
Akizungumza katika kikao na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kilichofanyika makao makuu ya halmashauri hiyo leo Alhamisi 29 Mei, 2025, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Kigoma, Bwana Sayumwe Yotham, alisema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kurahisisha huduma na kupunguza adha ya wateja kusafiri hadi ofisi za mfuko.
“Kwa sasa mwanachama anaweza kuangalia taarifa zake binafsi za michango na kuwasilisha maombi ya mafao akiwa mahali popote, muda wowote,” alisema Bw. Sayumwe.
Kwa mujibu wa Bw. Sayumwe, PSSSF Portal inapatikana kupitia tovuti kwa kuingia katika injini ya utafutaji ya Google na kutafuta “PSSSF Portal”, ambapo mwanachama atatakiwa kujisajili ili kuanza kutumia huduma.
Kwa upande mwingine, PSSSF Kiganjani ni programu ya simu inayoweza kupakuliwa kupitia Play Store. Baada ya kupakua, mwanachama anaweza kuanza kutumia mfumo huo kwa shughuli mbalimbali za huduma.
Meneja huyo alitaja baadhi ya faida za mifumo hiyo kuwa ni pamoja na:
PSSSF inatoa mafao mbalimbali ambayo sasa yote yanaweza kuombwa kwa njia ya mifumo hiyo. Mafao hayo ni pamoja na:
Kuanzia tarehe 1 Januari 2025, PSSSF imeongeza mafao mawili mapya:
Aidha, Bwana Sayumwe amewahimiza watumishi wa umma kuhakikisha wanaomba mafao yao miezi sita kabla ya kustaafu, mara tu baada ya kupata kibali cha kustaafu, ili kuhakikisha wanalipwa kwa wakati bila ucheleweshaji.
“Ni muhimu wastaafu wanaotarajiwa wakaanza mchakato mapema kwa kutumia mifumo hii ili kuhakikisha mafao yao yanapatikana mara moja baada ya kuhitimisha utumishi wao,” alisisitiza, Meneja Sayumwe.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa