Kufuatia maadhimisho ya siku ya mazingira yaliyofanyika Jumatano 4 Juni, 2025, Wananchi Wilayani Kakonko wameaswa kuhifadhi mazingira ili kuwa ustawi mkubwa kwa jamii endelevu na kutumia vifungashio vya plastiki vinavyotumika mara moja.
Akihutubia Wananchi katika viwanja vya Mwenge vilivyopo Wilayani Kakonko, Abdallah Mwamacha, mwakilishi wa mkuu wa Wilaya aliyekuwa mgeni rasmi alitoa rai kwa viongozi na wananchi kuhifadhi mazingira ili kuwa ustawi mkubwa kwa jamii endelevu.
Bwana Mwamacha, amewasisitiza wananchi kuwa shughuli mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya za kiuchumi zisipelekee kuwa na ongezeko kubwa la uharibifu wa mazingira na kushindwa kuhifadhi mazingira waliyonayo kwani mazingira yao ni muhimu kwa hiyo wayatunze kwa nguvu zote kwa ushirikiano ambao utakuwa ni wenye tija.
“Tuepuke utupaji wa taka hovyo hasa kwenye maeneo ya misitu na maeneo ya vyanzo vya maji”, Alieleza mgeni rasmi.
Naye mkuu wa kitengo cha Maliasili na Mazingira amewasisitiza Wananchi kuwa Kupitia maadhimisho hayo wananchi wasiendelee kutumia vifungashio vya plastiki ambavyo vinatumiwa mara moja tu, kama kuna ulazima wa kutumia vifungashio vya plastiki, watumie vila vinavyotumika mara kwa mara.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji, Mustapha Mtungwe amewaeleza wananchi kuwa uharibifu wa mazingira unapoelekea wao wenyewe kuharibu ustawi wao, hivyo ili waweze kuishi vizuri wanatakiwa kutunza mazingira pamoja na kujali miundo mbinu waliyoijenga.
“Nitoe wito kwenu viongozi wa Serikali na wananchi baada ya kutoka hapa muelimishane kuwa kuchoma miti sasa basi”, alieleza Kaimu Mkurugenzi.
Justine Constantine Bihemo, Mkazi wa Kakonko alieleza kuwa wameelezwa kuwa watunze mazingira hivyo alitoa wito kwa wananchi wengine kuzingatia kutunza mazingira kwa ufanisi ili yawatunze.
Kila tarehe 05 Juni maadhimisho ya siku ya mazingira yanafanyika kitaifa ambapo Wilayani Kakonko, Madhimisho hayo yalianza 3 Juni, 2025 kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi soko kuu Kakonko, kutoa elimu kuhusu kudhibiti vitendo vya ukataji miti hovyo na uchomaji moto kwani vitendo hivi hushamiri msimu wa kiangazi na kuhitimishwa 4 Juni, 2025 kwa kuhutubia wananchi katika viwanja vya Mwenge.
Kauli mbiu. “Dhibiti Matumizi ya Plastiki”.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa