TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA IDARA YA AFYA KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI (OKTOBA - DISEMBA) MWAKA 2016/2017.
Idara ya Afya imeendelea kutoa huduma mbalimbali za afya kupitia vitengo vyake ambavyo ni pamoja na;
Kitengo cha Afya kinga
Kitengo cha Tiba
Kitengo cha Afya ya Uzazi Baba, Mama na Mtoto
Kitengo cha UKIMWI na Magonjwa ya zinaa.
Kitengo cha Afya ya akili.
Kitengo cha Maabara.
Kitengo cha Madawa.
Kitengo cha Kifua kikuu na ukoma
AFYA KINGA
Katika kipindi cha Oktoba - Desemba 2016 hakuna ugonjwa wowote wa mlipuko ulioripotiwa. Hali ya usafi katika vituo vya kutolea huduma ni ya wastani. Aidha ili kuboresha usafi tunawaomba Waheshimiwa Madiwani na wenyeviti wa Vijiji kuendelea kuhamasisha wananchi waweze kupangiana zamu kwa vitongoji ili kushiriki usafi wa mazingira ya vituo vya afya na Zahanati zao hapa Wilayani.
TIBA
Ugonjwa wa malaria bado umeendelea kuwa na wagonjwa wengi miongoni mwa wagonjwa waliohudhuria katika vituo vya huduma wilayani ukifuatiwa na magonjwa ya maambukizi njia ya mkojo (Urinary Tract infections) kama inavyoonekana katika jedwali;
Magonjwa kumi yanayoongoza Wilayani;
Na
|
Ugonjwa
|
Idadi ya wagonjwa
|
|
|
|||
|
|||
1
|
Malaria
|
7,985
|
|
2
|
Maambukizi njia ya mkojo
|
2,400
|
|
3
|
Magonjwa njia ya hewa juu
|
2,399
|
|
4
|
Kichomi
|
1,519
|
|
5
|
Magonjwa ya minyoo
|
1,209
|
|
6
|
Magonjwa ya tumbo
|
542
|
|
7
|
Magonjwa ya dharura
|
492
|
|
8
|
Magonjwa ya macho
|
222
|
|
9
|
Kutoboka meno
|
107
|
|
10
|
Upungufu wa damu
|
51
|
|
AFYA YA UZAZI
MAHUDHURIO YA WAJAWAZITO
Kama inayoonekana katika jedwali hapa chini ni 24% tu ya wajawazito walimaliza mahudhurio manne kama inayotakiwa na Wizara ya afya. Sababu kubwa ni wengi wao kuja kliniki kwa kuchelewa wakiwa na mimba zenye umri mkubwa.
MIKOA/ HALMASHAURI
|
WAJAWAZITO
|
WATEJA WA MARUDIO
|
IDADI YA WAJAWAZITO WALIOKAMILISHA MAHUDHURIO MANNE AU ZAIDI
|
||
|
WALIOTEGEMEWA
|
HUDHURIA
|
IDADI
|
ASILIMIA
|
|
KAKONKO
|
1184
|
1123
|
1699
|
268
|
24
|
|
|
|
|
|
|
IDADI YA WATEJA WALIOFANYIWA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI (VIA)
HALMASHAURI
|
HIV+
|
HIV-
|
HAIJULIKANI
|
JUMLA
|
||||
IDADI
|
%
|
IDADI
|
%
|
IDADI
|
%
|
IDADI
|
%
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KAKONKO
|
0
|
0
|
16
|
0
|
0
|
0
|
16
|
0
|
Waliokutwa na viashiria vya saratani ya kizazi ni 0.
VIFO VYA WAJAWAZITO
Katika kipindi cha Oktoba - Desemba 2016 kulikuwa na kifo kimoja cha mama mzazi (1 maternal death) ambacho kilitokana na kuchanika mfuko wa uzazi (Ruptured uterus).
CHANJO KWA WATOTO
MIKOA/HALMASHAURI
|
IDADI YA WATOTO WALENGWA
|
PENTA 1
|
PENTA 3
|
PCV13-1
|
|||||
|
WAZALIWA HAI
|
MIEZI 0-11
|
IDADI
|
%
|
IDADI
|
%
|
IDADI
|
%
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KAKONKO
|
2460
|
7445
|
3080
|
85
|
3502
|
94
|
3080
|
85
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kiwango cha chanjo kwa watoto hupimwa kwa chanjo ya tatu ya Pentavalent (PENTA-3). Katika kipindi cha Oktoba - Desemba 2016 waliochanjwa ni 94%.
IDADI YA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO WALIOFARIKI NA VISABABISHI
HALMASHAURI
|
KUHARA
|
MAAMBUKIZI YA KOO
|
MALARIA
|
KIFUA KIKUU
|
UTAPIAMLO
|
UPUNGUFU WA DAMU
|
AJALI
|
PUMU
|
JUMLA YA VIFO
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KAKONKO
|
3
|
1
|
5
|
0
|
2
|
4
|
0
|
0
|
15
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
HUDUMA ZA UKIMWI
Katika kipindi cha Oktoba - Decsemba 2016 jumla ya wateja waliopima na kupata ushauri nasaha kwenye Vituo vya huduma ya afya ni 1880. Kati yao, waliokutwa na VVU ni 69 sawa na asilimia 3.6% .Kati ya waliokutwa na maabukizi ya VVU wanaume walikuwa 28 na wanawake 41.
Wateja waishio na VVU 483 wamehudumiwa hapa wilayani ambapo kati yao 379 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) na bado 104 hawajawa na vigezo vya kuanza dawa za ARV.
Vituo vinne hutoa huduma ya VVU (CTC) navyo ni Vituo vya afya vya Kakonko, Nyanzige, Gwanumpu na Zahanati ya Kasanda. Ziara 12 za Huduma mkoba za wateja waishio na VVU zimefanyika kwa wateja waishio mbali na Vituo vya huduma katika maeneo ya Nyagwijima, Bukirilo, Muhange, Mtendeli and Nyabibuye.
DAWA NA VIFAA TIBA
Katika kipindi cha Oktoba - Desemba 2016, hali ya upatikanaji wa dawa na vifaatiba imekuwa ya kuridhisha na hasa dawa za tiba ya malaria baada ya kununuliwa kiasi cha kutosha.
MIRADI YA AFYA
Mradi wa ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume pamoja na maabara moja katika Kituo cha afya Nyanzige unaendelea ambapo umefikia Zaidi ya 85% ili ukamilike.
Utekelezaji wa shughuli/miradi ya BRN pia unaendelea katika vituo 20, na katika vituo vyote utekelezaji huo uko Zaidi ya 85%. Isipokuwa kwa vituo vya Kinonko na Kasuga.
MIUNDOMBINU YA USAFIRI
Katika kipindi cha Oktoba - Desemba idara imefanikiwa kufanyia matengenezo ambulance gari DFP 3157 na kulipeleka kituo cha Afya Gwanumpu na kufanya vituo vyote 3 vya afya wilayani kuwa na magari.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa