1.0 UTANGULIZI
Pamoja na shughuli za ushauri kwa wafugaji, kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na kutoa chanjo,matibabu,huduma ya ukaguzi wa nyama na ushauri juu ya ufugaji bora wa samaki kwa kutumia mabwawa.
1.1 HALI YA MIFUGO
Kwa kipindi chote cha robo hii hali ya Mifugo ilikuwa nzuri kwa baadhi ya Kata ukiondoa Kata za Kasuga, Muhange, Nyabibuye na Nyamtukuza ambapo kulikuwa na ugonjwa wa Chambavu, Kata zingine kulikuwa na matukio machache ya magonjwa yaliyojitokeza.
2.0 KAZI ZILIZOFANYIKA
Ukaguzi wa afya ya Mifugo.
Ukusanyaji wa takwimu mbalimbali za Mifugo na Uvuvi.
Ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya Mifugo,ambapo magonjwa kama vile Chambavu(BQ), Ugonjwa wa kutupa mimba (Brucellosis) na Ndigana kali (ECF) yaligundulika kuathiri mifugo hususani Ng’ombe.
3.0 CHANJO YA MIFUGO
Takwimu za mifugo iliyopatiwa chanjo dhidi ya magonjwa tofauti ni kama ifuatavyo kwenye jedwali hapa chini;-
MIFUGO ILIYOCHANJWA KWA ROBO YA PILI.
AINA YA MIFUGO
|
AINA YA UGONJWA
|
MWEZI |
JUMLA
|
VIFO
|
||
OKTOBA
|
NOVEMBA
|
DESEMBA
|
||||
Ng’ombe
|
Chambavu
|
120
|
583
|
0
|
703
|
113
|
Kuku
|
Mdondo
|
6,509
|
4,720
|
2,730
|
13,959
|
0
|
|
||||||
Mbwa
|
Kichaa cha Mbwa
|
0
|
108
|
0
|
108
|
0
|
4.0 MIFUGO ILIYOCHINJWA NA KUKAGULIWA KWA AJILI YA KITOWEO.
Mifugo aina tofauti kama ilivyoorodheshwa hapa chini ilichinjwa kwenye kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2016/17. Baada ya zoezi la ukaguzi wa nyama, viungo vifuatavo vilitupwa, matumbo 88,Maini 62 na Figo 2 (MBUZI) Ng’ombe maini 33,Nguruwe Figo 2 hii ni baada ya kuoonesha hitilafu na nyama safi iliruhusiwa kwa matumizi ya binadamu bila masharti.
AINA YA MIFUGO
|
MWEZI
|
JUMLA
|
MAPATO Tshs.
|
||
|
OKTOBA
|
NOVEMBA
|
DESEMBA
|
||
Ng’ombe
|
82
|
95
|
79
|
256
|
1,408,000
|
Mbuzi
|
667
|
723
|
517
|
1,907
|
4,767,500
|
Kondoo
|
6
|
11
|
10
|
27
|
67,500
|
Nguruwe
|
42
|
75
|
50
|
167
|
668,000
|
JUMLA YA MAPATO YALIYOKUSANYWA
|
6,911,000
|
4.1 MAPATO YATOKANAYO NA MIFUGO
Ushuru wa machinjio na ada ya ukaguzi wa nyama,mapato hayo yalikusanywa na watendaji wa Kata na Vijiji katika maeneo husika kama inavyoelekezwa na Idara ya Fedha kwa viwango tofauti kwa wanyama waliochinjwa.Hivyo fedha iliyokusanywa tokana na wanyama waliochinjwa ni Tshs. 6,911,000/=
5.0 MATIBABU KWA MIFUGO KWA ROBO YA PILI 2016/17
Matibabu ya mifugo ndani ya Wilaya yalihusisha wanyama tofauti kama ilivyotolewa taarifa toka vijiji tofauti kama inavyoonesha hapa chini kwenye jedwali:-
AINA YA MIFUGO
|
UGONJWA
|
OKTOBA
|
NOVEMBA
|
DESEMBA
|
VIFO
|
||||
OCT.
|
NOV.
|
DES.
|
|||||||
NG’OMBE
|
Ndigana baridi
|
138
|
142
|
65
|
16
|
12
|
02
|
||
Kukojoa damu
|
07
|
0
|
08
|
17
|
11
|
08
|
|||
Ndigana kali
|
59
|
69
|
65
|
0
|
0
|
0
|
|||
Moyo kujaa Maji
|
0
|
45
|
0
|
0
|
0
|
0
|
|||
Ugonjwa wa Kiwele
|
0
|
5
|
5
|
0
|
0
|
0
|
|||
MBUZI |
Ndigana baridi
|
0
|
82
|
61
|
0
|
11
|
11
|
||
Moyo kujaa Maji
|
145
|
140
|
78
|
33
|
29
|
13
|
|||
Ugonjwa ngozi
|
0
|
21
|
38
|
0
|
0
|
0
|
|||
Nguruwe
|
Ugonjwa wa ngozi
|
0
|
31
|
35
|
0
|
0
|
0
|
||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
6.0 KUOGESHA
Kuna jumla ya majosho 5 ndani ya Wilaya na yote hayafanyi kazi kwasababu ni mabovu/yanavuja, hivyo wafugaji hutumia bomba za mkono kuogesha wanyama wao, takwimu ya wanyama walioogeshwa na kutolewa taarifa ni kama ifuatavyo hapa chini;-
AINA YA MIFUGO
|
OKTOBA
|
NOVEMBA
|
DESEMBA
|
Ng’ombe
|
12,870
|
20,969
|
18,791
|
Mbuzi
|
4,577
|
6,428
|
6,393
|
Kondoo
|
0
|
0
|
82
|
Nguruwe
|
0
|
0
|
54
|
7.0 SEKTA YA UVUVI.
Taarifa hii inahusu shughuli zote zilizofanyika katika kitengo cha Uvuvi kwa kipindi cha robo ya pili ni kama ifuatavyo;-
8.0 IDADI YA MABWAWA YA SAMAKI
Kuna jumla ya mabwawa ya samaki 31, kati ya hayo mabwawa 19 yamepandwa vifaranga vya samaki na 12 hayajapandwa kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo chini. Hata hivyo juhudi zinafanywa na Halmashauri kupata wahisani, kuhamasisha wana vikundi na wafugaji binafsi ili kupata vifaranga kwa mabwawa hayo ambayo hayajapandwa.
Na
|
KIJIJI
|
IDADI YA MABWAWA
|
HALI YAKE
|
1
|
Kasanda
|
3
|
1 limepandwa
2 hayajapandwa |
2
|
Kazialamihunda
|
4
|
2 yamepandwa
2 Hayajapandwa |
3
|
Nyagwijima
|
5
|
2 yamepandwa
3 hayajapandwa |
4
|
Kiziguzigu
|
2
|
2 yamepandwa
|
5
|
Kakonko
|
1
|
1 limepandwa
|
6
|
Nyabibuye
|
4
|
3 yamepandwa
1 halijapandwa |
7
|
Nyakiyobe
|
4
|
2 yamepandwa
2 hayajapandwa |
8
|
Gwarama
|
8
|
6 yamepandwa
2 hayajapandwa |
9.0 CHANGAMOTO.
Upungufu wa watumishi unasababisha wafugaji kutofikiwa ili kupata huduma za ugani inavyopaswa.
10.0 MIKAKATI YA KUBORESHA MIFUGO NA UVUVI
Kutoa chanjo kwa mifugo ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza hasa chanjo ya Chambavu na mdondo.
Kuendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vya wafugaji samaki.
Kusimamia mapato yatokanayo na mifugo.
Kuendelea kutoa mafunzo kwa wafugaji ili wafuge kibiashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa