Karibu Kakonko Wilaya yenye mazingira mazuri kwa kuishi na fursa mbalimbali kwa wageni na wenyeji. Baadhi ya fursa hizo ni uwekezaji katika ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara. Kwa sasa Halmashauri inajenga stendi mpya eneo la Rukenamaguru hivyo kuna fursa ya kujenga vibanda vya biashara. Aidha tumetenga eneo zuri kwa ajili ya kujenga nyumba za kuishi na biashara lililopo ukanda wa juu na tayari tumechonga barabara na kupima viwanja hivyo . Unakaribishwa kuomba viwanja kwani vipo.
Karibu sana Kakonko- Hongkong'
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: 028-2820137
Simu ya Mkononi: 0757470800
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa