Balozi Mwanri amekutana na wadau mbalimbali wa pamba wakiwemo wakulima wa pamba, maafisa ugani, maafisa watendaji wa kata na Vijiji, wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Dr.Godfrey Kayombo, Katibu Tawala Maulid Mtulia na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa katika ukumbi wa mikutano Jumatatu Novemba 27, 2023.
Akitoa mafunzo kwa wadau wa pamba amewasisitiza kusimamia kikamilifu taratibu za ulimaji, umwagiliaji dawa za viatilifu ili kuweza kuongeza uzalishaji wa zao la pamba.
Balozi Mwanri ameambatana na wataalam kutoka bodi ya pamba ambapo wanatembelea wadau wa pamba hususani wakulima na kutoa mafunzo ya namna ya kuzingatia taratibu za ulimaji, upaliliaji na matumizi ya viatilifu kwa zao la pamba.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa