Baraza la Madiwani limewataka Watumishi wa halmashauri kuwajibika na kuwa waaminifu katika usimamizi wa fedha za miradi vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakobainika kwa ubadhilifu wa fedha hizo.
Akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa kipindi cha mwezi Julai-Septemba katika mwaka wa fedha 2022/2023 siku ya ijumaa tarehe 11/11/2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Mwenyekiti wa halmashauri Fidel Chiza Nderego aliwakumbusha Waheshimiwa Madiwani kuwa wanalo jukumu kubwa la kusimamia Halmashauri kwa kuhakikisha Watendaji na Watumishi wanawajibika ipasavyo katika kusimamia miradi inayoendelea kujengwa ndani ya Halmashauri.
”Yeyote atakae bainika katika kipengele cha wizi, Sheria ichukue mkondo wake”, alisema Mhe.Nderego.
Mwenyekiti wa Halmashauri aliongeza kuwa Baraza linahitaji kuona watumishi wanazingatia uwajibikaji unaoendana na uaminifu, uamninifu unaoendana na uwazi na uwazi unaoendana na ukweli.
Aidha kila mtu awajibike ipasavyo ili kuepukana na hoja zinazoibuliwa na mkaguzi wa ndani kutokana na kutokuwajibika ipasavyo na kushindwa kufuta sharia na taratibu.
Akihitisha maelezo yake, Mwenyekiti Nderego alieleza kuwa kwa mwaka 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ilishika nafasi ya 15 kitaifa na nafasi ya 1 kimkoa katika usimamizi na utendaji wake wa kazi, Hivyo alisisitiza watendaji na watumishi wakafanye kazi kwa moyo wa uzalendo na malengo ya kuhakikisha Wilaya ya Kakonko inaendelea kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwani malengo ya Mkurugenzi Mtendaji ni kuona kwa Mwaka 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko inashika nafasi ya Kwanza kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa