Mkurugenzi wa program ya afya kutoka CCT (Christian Council of Tanzania) Bi.Clotilda Ndezi ametoa wito kwa Halmashauri, wafadhili na wadau mbalimbali kutumia watoa huduma waliopo Vijijini kupata takwimu kuhusiana na watoto wanaoishi mazingira magumu na wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI. Akizungumza na washiriki wa semina iliyofadhiliwa na CCT na kufanyika Wilayani kakonko hivi karibuni ameeleza kuwa CCT inasitisha program ya kuwahudumia watoto na wanawake baada ya kutoa huduma kwa kipindi cha miaka 7 mfululizo hivyo kuomba wadau waendelee kuhudumia watoto na wanawake wenye VVU. Aidha ametoa wito kwa Halmashauri kutenga fedha katika bajeti kwa ajili ya kuhudumia watoto na watu wenye Virusi vya UKIMWI.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii bwana Jabir Timbako amefafanua kuwa Halmashauri imekuwa ikitenga fedha katika bajeti na kuhudumia watoto na watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kipindi kirefu. Hata hivyo kwa sasa changamoto ni upatikanaji wa fedha hivyo kushindwa kuwahudumia baadhi ya watoto na WAVIU.
Semina hiyo imehudhuriwa na wataalam wa afya, wawakilishi wa jamii wakiwemo viongozi wa dini na shirika la UNICEF na kuweka mikakati ya kupata takwimu mapemza za watoto na wanawake ili kutatua changamoto zinazowakabili kwa pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa