Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imeanza kutoa leseni kiditali kwa kutumia mfumo wa Tausi ambapo leo Alhamisi Mei 04, 2023 leseni imetolewa kwa mfanya biashara mmoja aitwaye Raurent Gurand Richard kwa niaba ya wafanyabiashara wengine.
Akiwapongeza divisheni ya biashara na viwanda Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli ameeleza kuwa anawapongeza kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan kutoa leseni zote kupitia mfumo wa kidigatali wa Tausi.
Akizungumzia kuhusu manufaa ya mfumo wa Tausi Afisa biashara wa wilaya Imelda Hokororo ameeleza kuwa matumizi ya mfumo huo yatawezesha wateja kutuma maombi yao wenyewe na kuprint leseni zao wenyewe.
Afisa Mapato wa Halmashauri Luke Leonard Urio amefafanua kuwa mfumo wa tausi unawezesha kuona miamala ya kila siku na kuondoa wale wanaodaiwa yaani (defaulters) na kuonyesha kiasi cha fedha kilichokusanywa na mteja na kiasi alichoweka benki wakati huohuo mfumo huo umeongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa