Shirika lisilo la Kiserikali la Help Age limetoa msaada wa fedha Tshs.9,533,148 na mashine ya kutotolesha vifaranga (incubator) yenye thamani ya Tshs.800,000 na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa kwa ajili ya vikundi vya Wazee na Walemavu vilivyopo katika Wilaya ya Kakonko.
Mwakilishi wa shirika la Help age bwana Abdul Issa amefafanua kuwa vikundi vitatu (3) ni vya wazee na vikundi vinne (4) ni vya Walemavu ambapo kila kikundi kimeingizwa kwenye akaunti Tshs.1,588,858 na kikundi kimoja kimepewa msaada wa mashine ya kutotolesha vifaranga yenye thamani ya Tshs.800,000/=.
Bwana Abdul Issa ameushukuru Uongozi wa Wilaya na kuwaahidi kuwa wapo pamoja kuhakikisha jitihada za kimaendeleo za Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan zinafanikiwa kwa vitendo ili kujiletea Maendeleo.
Akipokea msaada huo katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri wiki hii, Mkuu wa Wilaya Kanali Evance Mallasa ameshukuru shirika la Help Age kwa kutoa Misaada kwa vikundi vya Wazee Walemavu na kuwaomba kuendelea kusaidia jitihada za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Afisa wa Ustawi wa Jamii Bi.Marietha Minza amewasihi wanufaika hao kutumia vyema fedha na vifaa hivyo ili viwanufaishe wengi zaidi.
Vikundi vilivyopewa msaada wa fedha ni Sawaka group- Kakonko, Upendo Walemavu -Kasuga, Umoja Walemavu - Kiziguzigu, Nchabhilonda group - Kanyonza, Walemavu Chizero āKasanda na Kikundi cha Pamoja.
Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Diwani wa Kata ya Kakonko Mheshimiwa Leonard Linze na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kakonko Ndugu Samoja Ndilaliha.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
HatimilikiĀ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa