Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yamefanyika katika kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye Wilayani Kakonko leo jumanne Desemba 10, 2024 na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko aliyewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Fidel Chiza Nderego.
Mhe.Nderego amewasisitiza wana ndoa kudumisha maelewano na kujikita katika utafutaji wa kipato ili kukuza uchumi na kuepusha migogoro inayotokana na kukosa kipato.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Michael Magese amewasisitiza wana jamii hususani wanaume kuepuka vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto wao na kuacha vitendo vya kutumia nguvu badala yake kujenga jamii yenye upendo na amani.
Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika la World vision kwa kushirikiana na Serikalia ambapo shirika hilo limekuwa likitekeleza shughuli za kijamii katika tarafa ya Kasanda na Nyaronga ikiwemo ujenzi wa zahanati na nyumba za waganga na kuendesha shughuli zinazolenga kutokomeza kukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa