.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe.Fidel Chiza Nderego, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025.
Ziara hiyo imefanyika kwa muda wa siku mbili ambapo imemalizika leo 13 Mei 2025, Ziara hiyo inalenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inaenda sambamba na mipango ya maendeleo ya halmashauri pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali.
Katika ziara hiyo kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ambapo mwenyekiti wa Halmashauri ameipongeza menejimenti kwa kushirikiana na Mkurugenzi mtendaji kuendelea kubuni miradi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kakonko kwani miradi hiyo inaenda kuwanufaisha wananchi wa Wilaya ya Kakonko. Mbali na hayo amesisitiza kuwa ubora wa miundombinu uendane na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha wajumbe wa kamati ya fedha wamewapongeza wasimamizi wa miradi kwa kuendelea kusimamia miradi vizuri, na kuutaka uongozi wa Halmashauri kuendelea kusimamia mafundi kwa kuwaelekeza waongeze kasi ya ujenzi ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya watumishi kituo cha afya Mugunzu, ujenzi wa jengo la mama na mtoto zahanati ya Mugunzu, ukamilishaji wa vyumba 02 vya maabara shule ya sekondari Rugenge, ujenzi wa vibanda 15 vya biashara soko la Mpakani Muhange, na kukagua ujenzi wa zahanati kijiji cha Kabare.
Miradi mingine iliyotembelewa ni ukamilishaji wa vyumba 02 na ofisi moja ya walimu shule ya msingi mbizi, ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi mtendaji pamoja na ujenzi wa vibanda 34 vya soko kuu la Kakonko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa