KAMATI YA FEDHA YATEMBELEA MIRADI NA KUSISITIZA KASI IONGEZE ILI IKAMILIKE KWA WAKATI
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imefanya ziara katika robo ya 3 ya mwaka 2022/2023 inayoanzia mwezi Januari hadi machi 2023 na kutembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo na kusisitiza miradi ikamilike kwa wakati na kasi ya ujenzi iongezwe.
Ziara hiyo imefanyika Aprili 18-19,2023 Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Fidel Chiza Nderego na kutembelea ujenzi wa ofisi za Halmashauri na Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri eneo la Kanyamfisi ambapo Tshs.1,000,000,000 imetolewa na ujenzi wa ofisi umekamilika kwa 98% na watumishi wanatumia ofisi hizo wakati ujenzi wa ukumbi msingi umejengwa na jamvi limemwagwa na nguzo zinapandishwa.
Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi wa vyoo shule ya sekondari Kashoza iliyopo Nyabibuye, ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Malenga, ujenzi wa Zahanati Rusenga, Ujenzi wa shule ya sekondari Katanga, ujenzi wa nyumba 2 za wakuu wa Idara kwa milioni 150, ujenzi wa wodi 3 katika hospitali ya Wilaya kwa gharama ya milioni 750 na ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari ya Wasichana kwa gharama ya Tshs.142,934,332 kwa ufadhili wa TEA (Tanzania Education Authority).
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa