Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col. Evance Mallasa leo Januari 8, 2025, akiambatana na wajumbe wa Kamati ya Usalama wilaya ya Kakonko, ametembelea na kukakuga Mradi wa ujenzi wa Barabara mpya yenye urefu wa Kilomita 20 kati ya Nyakiyobe-Kaminyimigina-Nyakivyiru iliyopo kata ya Gwarama Wilayani Kakonko, ambapo mradi huo unagharimu kiasi cha Shillingi milioni 421.6.
Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Kanali Mallasa, amemuelekeza mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kutekeleza kwa wakati ili kurahisisha huduma muhimu za usafiri na mawasiliano kwa wananchi wa maeneo hayo ambayo hayajawahi kupata huduma ya usafiri wa Barabara.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilayani Kakonko Mhandisi John Ambrose ameahidi kuendelea kumsimamia mkandarasi Davcha constructors and General Supplies ili kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi waendelee kunufaika na mradi huo.
Vile vile Kanali Mallasa ametemelea na kukagua ujenzi wa Daraja la Ikambi lililopo Kijiji cha Itumbiko kata ya Kakonko wilayani humo lenye urefu wa kilomita 0.77 linalo gharimu Fedha Tsh.milioni 878,501,200.00 linalounganisha Wilaya ya kakonko na Shule ya Sekondari Ikambi.
Aidha mradi huo utakapokamilika utasaidia kuboresha miundombinu ya barabara kwa wananchi wa Kata ya Kakonko na Wilaya kwa ujumla pia kuondokana na adha ya muda mrefu ya kukosekana kwa kivuko cha kudumu katika mto Muhwazi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa