Kamati ya usimamizi wa miradi Wilaya ya Kakonko kwa kushirikiana na shirika la World Vision imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na shirika la World Vision Mwanzoni mwa wiki hii tarehe 24 Agosti 2023 ndani ya Wilaya ya Kakonko na kuridhishwa na utekelezaji wake.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Watumishi Zahanati ya Chilambo two in one iliyopo kata ya Kasanda Wilayani Kakonko kwa gharama ya Tsh.246,936,362, Ujenzi wa matundu ishirini ya vyoo wavulana na wasichana shule ya Msingi Ilabiro kwa Gharama ya Tsh. 106,153,390.00, ujenzi wa matundu ishirini ya vyoo Wasichana na Wavulana Shule ya Msingi Narubura kwa Gharama Tsh.106,153,390. 00, ujenzi wa matundu ishirini ya vyoo wavulana na wasichana Shule ya Msingi Nyamiaga kwa Gharama ya Tsh.106,153,390.00, ujenzi wa matundu ishirini ya Vyoo wasichana na wavulana Shule ya Msingi Kumuhunga kwa gharama ya Tsh.106,153,390.00 pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba ya Watumishi two in one iliyopo Kijiji cha Churazo kwa Gharama ya Tsh. 221,465,232.00.
Mbali na kutembelea miradi kamati imekagua maeneo mbalimbali yanayotarajiwa kujengwa matundu ya vyoo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika shule mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shule ya Msingi Kasanda iliyopo kata ya Kasanda Wilayani Kakonko ambapo shule hiyo inatarajia kujengewa matundu 10 ya vyoo kwa wavulana na wasichana, Shule ya Msingi Kabingo iliyopo Kata ya Katanga inayotarajiwa kujengewa matundu 12 ya vyoo,Shule ya Msingi Churazo ambapo itajengewa matundu 20 ya vyoo , Shule ya Sekondari Mugunzu ambapo inatarajiwa kujengewa matundu matano na mabafu matano pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto linalotarajiwa kujengwa katika Zahanati ya Rumashi iliyopo kata ya Nyanzige kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Ujenzi huo unatarajia kutekelezwa na shirika la World Vision.
Aidha kamati imeridhishwa na miradi yote na kumuomba Mkandarasi kuongeza nguvu ili kukamilisha kazi kwa wakati kwani mradi unatarajia kukamilika tarehe 30 Agosti 2023 hivyo kuhakikisha kila kitu kinakamilika kwa wakati na kwa ubora unaohitajika pia mapungufu madogo kuyafanyia kazi.
Kwa upande wake Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la World Vision Kanda ya Kigoma Ndg. Ndibalema Josephat, ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kwa kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa Shirika la World Vision hivyo ameomba kuendelea kupewa ushirikiano kutoka kwa Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa