Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko Disemba 14 2023, imefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Taasisi za Serikali zilizomo ndani ya Halmashauri ya Wilaya lengo ni kuona utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Akitoa pongezi Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Wilaya Mhe. Saamoja Ndilaliha, ameupongeza uongozi wa Wilaya ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kwa kutekeleza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuboresha miundombinu ya maendeleo kwa wananchi.
Aidha Ndilaliha, ameendelea kusema chama kipo bega kwa bega na Serikali kuhakikisha kazi ya kuleta maendeleo na huduma nzuri kwa wananchi inafanyika.ameeleza kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo hivyo ametoa rai kwa idara husika kufanyia kazi sehemu zenye mapungufu.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi CCM Wilaya, Christopher Emmanuel, ameeleza kuwa kama chama wanaendelea kuwahamasisha viongozi katika kusimamia miradi ya maendeleo kwani serikali imeleta fedha nyingi sana kutekeleza miradi.
Hata hivyo kamati imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi ya kutosha katika Wilaya ya Kakonko kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi na kuiomba kuendelea kuleta miradi mingine zaidi.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya msingi kavugwe, Shule mpya ya sekondari Lutenga, shule ya msingi Nyamwironge, Mradi wa Maji Nyamtukuza, Mradi wa umeme Nyabibuye, Zahanati ya Luhuru, Shule ya sekondari Katanga na mradi wa taa za barabarani Kakonko - Itumbiko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa