Mafunzo ya kuhamasisha na kuijengea jamii uelewa juu ya umuhimu wa kuwaandikisha watoto wenye umri wa miaka 09-15 wasiosoma Shule kwa sababu mbali mbali, yamefanyika leo Machi 10,2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri eneo la Kanyamfisi lengo ikiwa ni kuwarudisha watoto Shule.
Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na Shirika la UNICEF kupitia Programu ya Elimisha mtoto yamewahusisha Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Waelimishaji wa jamii na Waelimishaji rika kutoka kata ya Kanyonza, Mugunzu, katanga, Gwarama na Nyamtukuza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndugu Ndaki S.Mhuli alipokua akifungua Mafunzo hayo amewahimiza Washiriki kufanya vizuri katika zoezi la utambuzi na uandikishaji wa watoto ambao hawapo Shule.
Ameeleza Elimu ni lazima kwa kila mtoto hivyo jamii isipo Elimishwa kuhusu umuhimu wa Elimu ni tatizo kwa usalama wa taifa kuendelea kuwa na Jamii ya watu wasiojua kusoma na kuandika.
Amesema watoto wasiojua kusoma na kuandika ni tishio kwa usalama wa nchi pia ni hatari sana kuwa na jamii ya watu wajinga. Hivyo tujitaidi kupambana na adui wa umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhakikisha watoto wote ambao hawasomi kutokana na sababu mbali mbali wanarudi Shule.
Kwa upande wake Afisa Elimu watu wazima Halmashauri ya wilaya ya Kakonko Ndugu Majaliwa Tryphone ameeleza washiriki wanatakiwa kuhamasisha jamii , kuwabaini na kuwaandikisha watoto wote wasiosoma ambao wako nje ya mfumo ramsi wa Elimu katika shule zilizo karibu na makazi yao .
Aidha ameeleza lengo la Shirika la UNICEF kufikia Mwaka 2024 kwa Mkoa wa Kigoma unalenga kuandikisha watoto 4959 wavulana wakiwa 2439 na wasichana 2520 na Halmashauri ya Wilaya ya kakonko inatakiwa kuandikisha watoto 602 hivyo jitihada na mbinu mbalimbali zifanyike ili kufikia malengo.
Naye Hafidhi Ramadhan Ntarambe Afisa Mtandaji Kata ya Katanga ameeleza zoezi la kuwatambua na kuwarudisha Shule watoto wasiosoma ni mapango mzuri utakaosaidia kuongeza nguvu kazi yenye Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa