Kitengo cha Ustawi wa Jamii, na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kakonko wametembea kituo cha kulea Watoto yatima Kabare katika kata ya Gwarama na kutoa zawadi mbalimbali.
Wakiongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Kaimu Katibu Tawala, Amani Alexander wamewasilisha zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni, mchele, sukari, unga wa ngano na mafuta ya kupikia siku ya Jumanne Machi 21, 2023.
Hii ni kufuatia uwepo wa maadhimisho ya siku ya taaluma ya Ustawi wa Jamii duniani ambapo Katibu Tawala amewahimiza Maafisa Ustawi wa jamii kuendelea kushirikiana na jamii.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Kuheshimu utofauti kupitia hatua za pamoja za jamii.”
Aidha kupitia hutuba yake amewapongeza Ustawi wa jamii kwa kuadhimisha siku yao kwa kutembelea na kutoa zawadi katika kituo cha kulelea watoto yatima kwani jambo hilo ni la kiimani hivyo kuendelea kuwatembelea mara kwa mara kwani itawasaidia katika kuendeleza ushirikiano kati yao na jamii kwa ujumla.
Afisa Ustawi wa Jamii,Bi Ephata Msiga amesema kuwa lengo la kutembelea kituo hicho ni kupeleka huduma kwa jamii pia kuonesha umuhimu wa kazi zao katika kuadhimisha siku ya taaluma ya ustawi wa jamii duniani.
Imelda Mathias, mlezi wa kituo hicho amewashukuru ustawi wa Jamii kwa kuwapelekea zawadi mbalimbli zitakazowasaidia na kuwaomba kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano katika kuwatunza watoto wao.
Wadau mbalimbali wameshiriki kuchangia zawadi hizo wakiwemo World Vision, CWT, Tanesco, CRDB na TRA.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa