Walimu wa Shule za Msingi na wasimamizi wa Elimu ngazi ya kata wametakiwa kuibua na kutumia Hadithi za Kujifunza za Mafanikio za mfano ili kuleta mafanikio ili kuleta mafanikio chanya katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi katika mafunzo yatakayodumu ndani ya siku (02) ambayo yameanza leo Desemba 04,2022, katika kata ya kiziguzigu Shule ya Msingi Ilela.
Ameyasema hayo Mwezeshaji wa Mafunzo Ndugu Alfan Waziri kutoka chuo cha Ualimu Mandaka wakati akitoa mafunzo kwa Walimu ambao wapo kazini.
Mafunzo hayo yamehusisha Walimu wa Shule za Msingi na Wasimamizi wa Elimu ngazi ya kata ambazo zipo kata ya Kakonko, Kiziguzigu na Kanyonza.
Amesema Hadithi za Mafanikio za Kujifunza za mfano zenye changamoto, Ufumbuzi, Matokeo na utatuzi zitasaidia kuleta uhamasishaji wa ufundishaji kwa Walimu, Kutoa fursa na hamasa ya kujifunza kwa wengine, kukuza ushirikiano baina ya Walimu na Wanafunzi, kuleta ari ya utendaji kazi na kuleta mafanikio chanya kwa wanafunzi,walimu,jamii pamoja na Wadau wa Elimu.
Aidha Hadithi za mafanikio za kujifunza za mfano zinapatikana katika jamii inayotuzunguka, Walimu,Wanasiasa,Wajasiriamali pamoja na taasisi za Elimu
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mradi wa Shule Bora unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wake wa Misaada ya (UKAID).
Mradi wa Shule Bora unatekelezwa katika Mikoa (09) Nchini Tanzania ambayo ni Mkoa wa Katavi,Dodoma,Mara,Pwani,Kigoma,Rukwa ,Simiyu,Tanga na Singida.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa