CGF (Rtd) Thobias Andengenye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewaongoza Wananchi wa Kigoma kupokea Mwenge wa Uhuru 2023 Katika Wilaya ya Kakonko.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika Shule ya Sekondari Wasichana Kakonko iliyopo katika Kijiji cha Kanyonza Kata ya Kanyonza Agosti 16,2023.
Akipokea Mwenge wa Uhuru CGF (Rtd) Thobias Andengenye amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 999.8 katika Halmashauri (8) za Mkoa wa Kigoma na Mwenge wa Uhuru utaweka Mawe ya Msingi, Kufungua, kuzindua, kukagua na kutembelea miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa na Wananchi, Serikali na Wadau wa Maendeleo waliopo katika Mkoa wa Kigoma.
Mwenge wa Uhuru utatembelea Jumla ya Miradi 66 yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 18.3. Miradi (21) itazinduliwa, Miradi (3) itafunguliwa, miradi (19) itawekewa Mawe ya Msingi, Miradi (21) itatembelewa na kukaguliwa na miradi (2) ni shughuli za kugawa Chakula na Vyombo vya usafiri kwa Watendaji wa Kata na Chakula cha Lishe kwa Watu wanaoishi na VVU.
Ameendelea kusema miradi hiyo inahusisha miradi ya Sekta ya Afya, Elimu, Maji, Ujenzi wa Barabara, Kilimo, Hifadhi ya Mazingira na uwezeshaji wa Vikundi vya Vijawa na Wanawake Kiuchumi.
Aidha Mwenge wa Uhuru Mkoani Kigoma utakagua na kushuhudia kazi na Afua zinazotekelezwa katika Mkoa ili kudhibiti Malaria, VVU na Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya na Rushwa.
Katika Hatua Nyingine CGF (Rtd) Andengenye amesema Mkoa wa Kigoma umetekeleza ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 ambao unasema Mabadiliko ya Tabia ya Nchi Hifadhi ya Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo Vya Maji kwa kupanda Miti Zaidi ya Milioni Kumi (10) na kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Miti Elfu Nne Mia Mbili na Tatu inatarajiwa kupandwa katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Kigoma.
Aidha CGF (Rtd) Andengenye amesisitiza Mwenge wa Uhuru ni Nguzo muhimu na Unachochea Maendelea ya Watanzania kwa kudumisha Haki, Uwazi, Umoja na Mshikamano na Kuwahimiza Watendaji wa Serikali kuendelea kusimamia miradi ya Maendeleo inayoletwa na Serikali kwa kuweka uzalendo mbele kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa