Mwenge wa Uhuru 2023 umeangaza Jumla ya miradi 9 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2,648,920,128 na Klabu moja ya Wapinga Rushwa Wilayani Kakonko Agosti 16,2023.
Mwenge wa Uhuru 2023 umekimbizwa kilomita 170.9 ndani ya Wilaya ya Kakonko na Mwenge wa Uhuru umezindua miradi (2), umefungua miradi (2), umeweka Mawe ya msingi Miradi (3), umetembelea miradi (2), umekagua na kutembelea Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Buyungu Kata ya Kiziguzigu.
Miradi hiyo yenye manufaa Makubwa Kwa Wananchi inajumuisha Miradi ya Elimu, Afya, Utawala, Barabara na Biashara.
Miradi hiyo ni Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa (8) na Ofisi (3) za Walimu Shule ya Sekondari Wasichana Kakonko Wenye thamani ya Shilingi Milioni 160,000,000 kutoka Serikali Kuu.
Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Mkaa Mbadala cha kikundi cha Vijana Kijiji cha Itumbiko wenye thamani ya Shilingi Milioni 35,422,141 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi 33,872,142 ni kutoka katika Shirika la kuhudumia Wakimbizi Denmark (DRC) na Shilingi 1,050,000 ni mchango wa Wanakikundi na Shilingi 500,000 ni Mchango wa Halmashauri.
Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kakonko-Itumbiko yenye kiwango cha Lami Kilomita 1.2 wenye thamani ya Shilingi Milioni 950,000,000.
Mradi wa Shamba la Miti Kijiji cha Kiga Wenye Thamani ya Shilingi Milioni 30,886,197 ambapo Shilingi Milioni 29,280,000 ni fedha Kutoka TASAF na Shilingi 1,606,185 ni Mchango wa Halmashauri ya Kijiji.
Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ilabiro Wenye thamani ya Shilingi Milioni 297,711,802 ambapo Shilingi Milioni 295,141,802 ni ufadhili kutoka Shirika la World Vision Tanzania na Shilingi 2,570,000 ni mchango wa Wananchi.
Mradi wa Ofisi ya Afisa Tarafa Kata ya Kasanda Wenye Thamani ya Shilingi Milioni 166,400,000 ambapo Shilingi 165,000,000 ni kutoka Serikali Kuu na Shilingi 1,400,000 ni Mchango wa Wananchi.
Mradi wa Kikundi Azimio Kiziguzigu chenye thamani ya Shilingi 8,500,000 ambapo shilingi 8,000,000 ni mkopo wa asilimia 4 ya mapato ya ndani ya Halmashauri na Shilingi 500,000 ni mchango wa wanakikundi.
Mradi wa ujenzi kituo cha Mafuta Glory to God Oil wenye thamani ya Shilingi Milioni 300,000,000.
Aidha miradi yote imepitishwa na Mbio za Mwenge wa uhuru 2023.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa