Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kakonko Ndaki Stephano Mhuli ameongoza kikao cha kamati ya lishe robo ya 04 kuanzia mwezi Aprili-Julai kwa mwaka wa fedha 2022/2023, kilichofanyika katika ukumbi mdogo ofisi ya Mkurugenzi mtendaji Julai,17,2023.
Mkurugenzi Mtendaji amewasisitiza wazazi wasiochangia chakula wabainishwe na barua ziandikwe kwa watendaji wa kata na vijiji kueleza namna walivyoshughulikia wazazi wasiochangia chakula.
Aidha Shule zote zitoe huduma ya chakula shuleni kwa wanafunzi wote bila kupendelea madarasa yenye mitihani. Vile vile Walimu waandikiwe barua ya kusimamia mashamba darasa ya shule na walime mahindi na mboga mboga ili kuwasaidia wazazi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Afisa Lishe wa Mkoa, Mwakilishi kutoka TAMISEMI, Mwakilishi CRS, Afisa ustawi wa Jamii,Maafisa Lishe na Viongozi wa Dini.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa