Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Evance Mallasa akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Ndugu Ndaki Mhuri Hundi ya fedha za Kitanzania Millioni Mia Saba na Sitini (Tsh. 760,000,000/=), Oktoba 12, 2022, kwa madhumuni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa thelathini na nane (38) ikiwa ni Maandalizi na Mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha Kwanza kwa Mwaka 2023.
‘’Ikumbukwe kuwa oktoba 2021 Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha Shillingi Billioni moja kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 46 ujenzi wa bweni kwa watu wenye mahitaji maalumu katika sekta ya elimu lengo kubwa la serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuondoa changamoto ya utoro na mdondoko wa Wanafunzi Shuleni, pia fedha hizo ziliweza kupunguza uhaba wa madarasa’’.
Mkurugenzi Mtendaji alimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka Wilaya ya Kakonko, alieleza kuwa Wamelenga kuanzisha Shule nzuri ikiwemo Shule ya Wasichana Kakonko imewekwa kwenye mikakati ya kutoa wanafunzi bora pia wamepewe fursa hasa Watoto wa kike ambao watachukuliwa kwa kila kata wote watakao fanya vizuri kufikia mwakani wawe na wanafunzi 120 -160 kutoka kwenye wanafunzi 80.
Aidha alikemea swala la utoro Shuleni na kutangaza vita kwa wazazi/walezi wanaosababisha Watoto kuacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani na kuwasisitiza watendaji wa kata na vijiji kuwafuatilia wazazi/walezi wanaofanya vitendo hivyo kwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Katibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Viongozi wa Dini, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Watendaji wa Kata na Vijiji, Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa