Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Lusubilo Mwakabibi ametembelea wachimbaji wadogo wadogo wa madini waliopo eneo la Nyamwironge kata ya Nyamtukuza na kukagua miundo mbinu inayotumika, suala la ulipaji kodi kwa Serikali na kuzungumza na wachimbaji na viongozi wa wachimbaji hao. Katika ziara hiyo Mkurugenzi ameelzwa kuwa mazingira ya machimbo hayo bado ni duni hivyo kuombwa kufikikisha jambo hilo kwa Uongozi wa juu ili kuboresha. Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji amebaini Ukiukwaji wa baadhi ya sheria hasa suala la ulipaji ushuru hivyo kuhimiza wachimbani na viongozi kuanza kulipa kodi kikamilifu kama sheria na taratibu zinavyoagiza.
Pamoja na uwepo wa madini katika Wilaya ya Kakonko, Halmashauri imekuwa haipati mapato yoyote hatua iliyopelekea Mkurugenzi kufikisha kilio hicho kwa Waziri wa Nishati na madini alipofanya ziara mwazoni mwa mwaka huu na kuahidi kutuma timu ya wataalam wa madini kutoka Wizarani ili kutafiti iwapo eneo hilo linafaa kwa uchimbaji madini. Hata hivyo wachimbaji wadogo wadogo wameendelea na shughuli za uchimbaji pamoja na hali iliyokuwepo kwa maelezo kuwa wamepewa vibali na Serikali kuu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa