Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu OR-TAMISEMI Ndugu Vicent Kayombo, ametembelea na kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa Wilayani Kakonko kupitia mradi wa BOOST na kusisitiza ifikapo Agosti 13, 2023, miundombinu yote ya madarasa na vyoo iwe imekamilika na kuanza kutumika.
Amesema hayo leo Julai 29,2023 Katika ziara yake Wilayani Kakonko alipotembelea na kukagua miradi ya Elimu inayoendelea kutekelezwa kupitia mradi wa BOOST.
Katika Ziara hiyo ametembelea mradi wa Shule Mpya ya Kazilamihinda yenye ujenzi wa Madarasa (09), Jengo la utawala na matundu ya vyoo (21) kwa gharama ya Tshs. 361,500,000/= na Ujenzi wa Madarasa manne (04) Shule ya Msingi Kigarama Ofisi mbili (02) za Walimu pamoja na Matundu ya Vyoo (05), kwa gharama ya Tshs. 110,600,000/=, aidha ametembelea ujenzi na ukarabati wa Bweni Shule ya Sekondari Amani Mtendeli.
Aidha ndugu Vicent Kayombo, amemuhimiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kusimamia fedha zilizoletwa na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa katika ubora na viwango vinavyohitajika.
Hata hivyo ndugu Kayombo ameridhishwa na namna miradi inavyotekelezwa na katika kikao amewahimiza walimu kufundisha kwa bidii na kusimamia wanafunzi kwa umahili ili kuhakikisha wanafunzi wote wa darasa la kwanza wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu pia kuendelea kusimamia lugha ya kigereza kwa wanafunzi na waalimu shule za Sekondari ili kuwa na ufaulu mzuri.
Kwaupande wake Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Dr.Godfrey Kayombo, amempongeza Mkurugenzi wa Elimu OR-TAMISEMI kwa kutembelea miradi hiyo nakuahidi kutekeleza maelekezo aliyoyatoa na kusimamia miradi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa