Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Hosea Ndagala amewasisitiza wakazi wa Wilaya ya Kakonko kutunza mazingira na misitu kwa kupanda miti iliyo rafiki na vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji yanaendelea kuwepo. Akihutubia wakazi wa Kijiji cha Kazilamihunda na wakazi wa kata ya Nyabibuye walioshiriki katika maadhimisho hayo amesisitiza suala la utunzaji wa misitu. Aidha amesisitiza wananchi kuhudhuria mikutano ili kutoa kero na shida na kutatua matatizo yao kwa pamoja.
"Nawaomba wananchi mshiriki katika mikutano ili kutoa kero zenu na kujadili matatizo yenu kwa pamoja", alieleza kanali Ndagala. Pamoja na msisitizo huo Mkuu wa Wilaya amewatahadharisha Wanachi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia taratibu za afya na kupunguza kushikana mikono ili kuepukana na ugonjwa wa Ebola ambao unaelezwa kuwepo katika nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kauli mbiu ya mwaka 2017 inasema Hifadhi ya Mazingira ni muhimili kwa Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa