Mkuu wa wilaya ya Kakonko Col. Evance Mallasa amewasisitiza Watendaji wa Kata kuendelea kudhibiti suala la uchomaji wa moto ndani ya kata kwani kuna baadhi ya maeneo yameathirika na moto ikiwemo Mtendeli hivyo waendelee kushirikiana na kamati za usalama za kata kuwabaini watu wanaochoma misitu ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema hayo Agosti 10, 2023, katika kikao cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Kanali Mallasa ameeleza kuwa suala la uchomaji wa moto sio zuri ndani ya Wilaya hivyo kwa maeneo ambayo yataendelea kuathiriwa na uchomaji wa moto watendaji wa kata ndio watakao wajibika, hivyo waendelea kufuatilia na kuwabaini wahusika wa matukio hayo ili wachukuliwe hatua.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Ndaki Stephano Mhuli ameeleza wamechukua suala hilo hivyo watalifanyia kazi na kuwasisitiza watendaji kila Vijiji kuwa na sheria ndogo ili kudhibiti uchomaji wa moto.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa Wilayani Kakonko Tarehe 16 Agosti 2023 ukitokea Mkoa wa Kagera.
Kauli Mbiu ‘’Tunza Mazingira, okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa’’
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa