Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Tshs.100,800,000 (milioni mia moja na laki nane) ambazo zitawezesha nyumba 46,857 kupata anuani za makazi.
Akizindua rasmi zoezi la anuani za makazi kwa kuweka namba katika nyumba mbili za Wananchi na kibao cha barabara ya Anglikana na Mkakila siku ya Ijumaa tarehe 18.03.2022.
Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi amewasisitiza vijana 200 watakaofanya kazi hiyo kutumia maelekezo na mafundisho waliyopata kuwaelekeza Wananchi umuhimu wa zoezi hili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ndaki S.Mhuli ameeleza kuwa Serikali imetoa Tshs.100,800,000 (milioni mia moja na laki nane) kwa ajili ya zoezi la anuani za makazi ambapo makundi yote yamewezeshwa ikiwemo watendaji wa Vijiji ambao wamepewa elimu kisha kukaa na kupendekeza majina ya Vijiji na mitaa kisha kushiriki zoezi la kuweka namba kwa nyumba ambalo tayari limefanyika.
Mkurugenzi ameeleza kwa sasa zoezi litakalofanyika ni kuchukua taarifa za kila nyumba.
“Tunaomba wananchi watusaidie kutoa ushirikiano wa kubandika vibao kwenye nyumba zao na kugharamia wenyewe vibao hivyo”, Alieleza Mkurugenzi Mtendaji.
Mratibu wa zoezi la anuani za Makazi Gideon Kimaro ametoa taarifa kuwa zoezi hilo linafanyika kwa kuzingatia sera ya Posta yam waka 2003 na Ilani ya Chama cha Mapinduzi yam waka 2020- 2025.
“Wilaya ya Kakonko ina Tarafa 03, Kata 13, Vijiji 44 na Vitongoji 355 ambapo nyumba 48,857 zimesajiliwa na kuandikwa namba kwenye kuta zake”, ameeleza mratibu wa zoezi la anuani za makazi.
Zoezi hilo limehudhuria na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya, Katibu wa Chama, Katibu wa Mbunge, Diwani wa kata ya Kakonko, Wakuu wa Taasisi za Serikali na mashirika , Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Viongozi wa dini na Wananchi.
Zoezi la uchukuaji wa taarifa kwa kila nyumba litaanza tarehe 21.03.2022 na kuchukua siku 10 ambapo mfumo wa anuani za makazi una manufaa makubwa ikiwemo kuchangia kuimarisha ulinzi na Usalama, Kutengeneza ajira, kuwezesha kufanyika biashara Mtandaoni, kuwezesha mipango na tafiti kufanyika kwa tija na kurahisisha utoaji na upelekeaji wa huduma kwa Wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa