Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa, amewaasa vijana Wilayani Kakonko kuzingatia maadili mema yenye kulinda utu wa mtu na kuzingatia maadili ya kiafrika hususani yale ya Kitanzania.
Ametoka Wito huo Ijumaa Aprili 21, 2023 wakati wa Sherehe za Mahafali ya 1 ya Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, kilichopo Wilayani Kakonko mkoani kigoma.
Akiwahutubia wahitimu hao, Kanali Mallasa, amewataka vijana hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata chuoni hapo kutumia fursa za miradi inayotekekezwa Wilayani Kakonko kupunguza Uhaba wa mafundi katika Fani mbali mbali jambo linalopelekea Wilaya kutafuta Mafundi Kutoka nje ya Wilaya jambo linalo pelekea kudumaza Uchumi wa Watu wa Kakonko.
"Wilaya ya Kakonko tunao uhitaji mkubwa wa mafundi wa fani mbalimbali, hali inayopelekea kutafuta mafundi kutoka nje ya Wilaya yetu, Kwa uwepo wa chuo hiki naiona changamoto hii inakwenda kupungua" Alisema Kanali Mallasa
Aidha Amewasisitiza wahitimu hao Kuwa waaminifu katika maeneo yao ya kazi na kuweka mbele Uzalendo Kwa Nchi yao, na kuto kubweteka na ngazi hiyo ya mafunzo waliyoipata.
"Pamoja na kupata mafunzo katika Fani mbalimbali msibweteke na kuishia hapa jiendelezeni,huku mkiendelea Kuwa wazalendo,..Wilaya yetu inahitaji mafundi waadilifu na wazalendo" alisisitiza Kanali Mallasa.
Wakisoma risala yao Mbele ya Mgeni Rasmi,Wahitimu wameainisha Changamoto zinazo wakabili Wanafunzi wakati wa mafunzo, Kubwa ni uhaba wa vifaa vya kujifunza hasa kwa vitendo jambo linalopelekea kushindwa kujifunza kwa vitendo kwa muda wa kutosha.
Naye Mkurugenzi wa Mafunzo Stadi Kutoka Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Thobias Jackson Ngailo amewatka wahitimu hao wakafanye kazi kwa weledi na Maadili Ili wawe mfano mzuri katika Jamii ukizingatia chuo walichopata mafunzo ni chuo Kilicho Chini ya Jeshi la Kujenga Taifa.
"Vyeti mlivyovipata leo ni kipande tu cha karatasi,tunategemea mkafanye kazi kwa kuzingatia maadili kulingana na taaluma zenu" amesisitiza Luteni Kanali Ngailo.
Vile vile Luteni Kanali Ngailo,ameahidi Kuwa Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa itaendelea kukiongezea Uwezo chuo hicho kwa Kuongeza nyenzo za kufundishia hasa mafunzo kwa vitendo.
"Tunategemea kukiongezea chuo Nyenzo za kufundishia kwa vitendo katika fani za Uchomeleaji,Udereva Ufundi Magari (Mechanics Engineering) na kozi zingine" ameongeza Luteni Kanali Ngailo.
Naye Mkuu wa chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, Meja Benedicto Lubida, akisoma taarifa ya Chuo Mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa ameeleza Chuo Cha JKT Kasanda kinatoa Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Fani za Udereva, Uchomeleaji, Umeme wa majumbani, Kompyuta, Saloon na urembo, Upishi pamoja na ushonaji kwa kozi za muda mfupi na za muda mrefu kwa ngazi 1,2 na 3.
Aidha katika mahafali hayo jumla ya Wanafunzi 22 kati yao Wanawake ni 7 na wanaume ni 15 wamehitimu mafunzo ngazi ya 3 katika fani tofauti, ambapo Udereva wamehitimu Wanafunzi 12, Saluni na mapambo Wanafunzi 4 na Kompyuta Wanafunzi 6.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko
Anuani ya Posta: P.O.BOX 3
Simu: +255(028) 2988881
Simu ya Mkononi: +255(028) 2988881
Barua Pepe: ded@kakonkodc.go.tz
Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa